Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Ingependeza kama wewe ungeweka vipengele vinavyozuia Tume ya Uchaguzi kutomfungia Lisu kufanya kampeni kwa Siku saba
Yaani utoe we malalamiko afu mzigo wa kuthibitisha unipe mimi?
 
Hapo ndio anaingia kwenye kumi na nane,akiendelea na kampeni wanamtoa kabisa, jeuri haina faida yeyote tena unae mfanyia jeuri ndio ana ubavu zaidi yako. Hivi jina likikatwa kwenye list ya wagombea atafanya nini?
Wewe naye bwa tu kwani sisi tunaishi mbinguni situko wote mitaani muengueni muone tutamalizana uku uku.
 
Kufuatia mgombea Urais kupitia Chadema Mhe.Tundu Lissu kufungiwa kufanya kampeni kwa siku 7 kuanzia leo hadi tar.9 Oktoba, atatumia nafasi yake kama Makamu Mwenyekiti wa Chadema kufanya ziara ya siku 7 (kuanzia kesho) kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini. Sheria ya vyama vya siasa no.5 ya mwaka 1992 inatoa ruhusa kwa viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kuzunguka majimbo yote kuwanadi wagombea ubunge na udiwani. Hivyo kwa kutumia sheria hiyo Lissu ataanza ziara rasmi kesho kuwanadi wagombea ubunge na udiwani, kisha tar.10 ataendelea na ratiba yake kama mgombea urais.! #Mwamba #AkiliKubwa #NiYeYe
Tukisema hii ni akili kubwa, makada wa CCM wenye vichwa vigumu kwa kushupaza shingo zao hawatuelewi.
 
Ameambiwa ana nafsi ya kkukata rufaa,sasa hayo ya kuendelea na kampeni ni kutafuta shida nyingine!!Tunajua ameshapata momentum lakini ni lazima amkumbuke Mungu,Kila jambo lina sababu!!
akate rufaa kwa hukumu ipi? hukumu gani isiyo na mshtaki na mshtakiwa?
 
Anachokitafuta na Amsterdam wake wanakaribia kukipata. Niliwahi kusema Lissu ana akili nyingi sana za darasani Ila Elimu ya Dunia ni ZERO. No wonder anatembea kwa kuchechemea kwa kutofunzwa na ***** na kufunzwa na ulimwengu. Sasa acha ulimwengu uendelee kumfundisha zaidi.
Kaka faida kubwa dunia ya watu wenye upeo mkubwa uwa hawaogopi. Haki huwa inapiganiwa haijileti (justice doesnt come on silver plate) hupiganiwa. Nyerere alikuwa aggrisive kuliko LISSU tena katika mateso makubwa kutoka Pugu secondari kwa miguu mpk magomeni kukutana na akina Paul Rupia. Kwenye vitabu vyake anasema kuanzia Pugu mpk magomeni mwaka 1956 kulikuwa ni pori mpk simba, na ilimbidi apite usiku ili utawala wa kikoloni usimuone. Wew mleta post kwa mguu magomeni mpk pugu hauwez nenda na ni lami tupu. Lissu anapita kwenye UVULI wa mauti, ila kuna cku apata anachopigania. Anatuangaikia sie tusiokuwa na sauti wala ujasiri wa kumkabili Magufuli. Lissu ni mwanaume, sio kazi ndogo kumlegeza mzee baba ambaye aliifanya nchi kama shamba lake. Kajaza nafasi za hela ndugu zake. Wala hata aibu hana.
 
Anachokitafuta na Amsterdam wake wanakaribia kukipata. Niliwahi kusema Lissu ana akili nyingi sana za darasani Ila Elimu ya Dunia ni ZERO. No wonder anatembea kwa kuchechemea kwa kutofunzwa na ***** na kufunzwa na ulimwengu. Sasa acha ulimwengu uendelee kumfundisha zaidi.
Jahahahhaahaa umeandika kwa mbali ka vile huna akili ila ukisogeleea nikweli huna akili.


Unadhan lissu kwa aloyapitia, kuna kitu kitakachomuondoa kwenye mstari wa kile anavhokisimamia???
 
Wewe naye bwa tu kwani sisi tunaishi mbinguni situko wote mitaani muengueni muone tutamalizana uku uku.
Hii mikwara yenu mbuzi pelekeni kwa beberu wenu Amsterdam, kinukisheni sasa si kasimamishwa siku 7?kinukisheni sasa
 
Mpira ni Dk 90 lakini NEC wanataka kumaliza mechi dk ya 30 Hatutakubali kamwe.
 
Lisu sio kondoo kama watanzania wengi walivyo.
Hili taifa wote tunalielewa..... Tunajua matokeo ya kutokutii sauti za mamlaka.
Swali ni nani anamlinda Lisu? Kwann mamlaka zinapata shida kumdhibiti?
 
Salaam Wakuu,

Muda wowote kuanzia sasa, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa anaongea na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Tegeta.

Nitawaletea kila kinachojiri Kutokea hapa Tegeta.

Agenda kubwa ni kusimamishwa kufanya Kampeni

======

UPDATES:

1654HRS: Waandishi wa Habari wameshafika eneo la tukio.

1704HRS

Tundu Lissu anasema
View attachment 1588251
Karibuni Nyumbani kwangu.

Mchana huu tume ya maadili imenisimamisha kufanya kampeni kuanzia kesho.

Uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo.

Naomba nizungumze juu ya utaratibu ambao umefanyika.

1. Hadi sasa sijapatiwa tuhuma yoyote ya malalamiko ya mgombea yoyote au chama chochote kuhusu ukiukaji wa maadili yoyote. Sina taarifa yoyote ya maandishi kinyume cha utarsti6.

2. Sijapewa fursa yoyote ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Maadili yanasema ikitokea kuna malalamiko, anatakiwa apeleke kwa tume na mtuhumiwa apewe nakala na apewe masaa 42 ya kujibu.

3. Hadi sasa hakuna wito wowote wa kwenda kwenye kikao cha tume ya Maadili.

4. Nimepokea kama ninyi mlovyopokea kwa kupitia vyombo vya habari ambayo ni kinyume cha utaratibu.


HII HAISHANGAZI

Ukifuatilia Mikutano ya CCM, Tume ya Uchaguzi hasa Mahera, Magazeti ya Msiba, Ukiangalia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM au wapambe wao, ADUI NAMBA MOJA NI TUNDU LISSU.

Uamuzi huu unathibitisha kwamba hatuna tume ya Uchaguzi bali tume ambayo inahakikisha CCM inabaki madalakani. Tangu 21 Septemba 2020, CHADEMA tumepeleka Malalamiko Matatu ya vitendo vya ukiukwajo ya maadili ya Uchaguzi dhidi ya Magufuli yanayohusiana na Rushwa.

Anapiga simu Waziri apeleke hela, jenga barabara hapa. Zote zile ni rushwa kwa mjibu wa gharama za Uchaguzi. Ni matendo yaliyokatazwa na sheria kwa sababu ni Rushwa.

Tumepeleka malalamiko hayo hayo kwa msajili wa vyama vya siasa.

Tume haijawahi kusema kwamba wamepokea Malalamiko ya vitendo vya Rushwa. Hakuna nliposikia.

Mnakumbuka Mahera alisema nini wiki iliyopita. Hata kabla sijalalamikiwa. Sijui barua walipeleka wapi.

NINI MSIMAMO WANGU?

Lengo halisi la msimamo huu sio kuniadhibu sababu nimekiuka maadili, bali ni kuhakikisha sifanyi Kampeni kipindi ambacho Magufuli hafanyi Kampeni. Hiivyo wamenisimamisha kipindi Magufuli akiwa Gereji.

Hoja nlizozitoa kwenye Kampeni hakuna Majibu hata moja.

Ujenzi wa Uwanja wa ndege wenye hadhi ya Kimataifa kijijini kwake. Na mlipaji mkuu ni Mtoto wa Kaka. Yote hayana majibu na mengine mengi.

Uamuzi huu sio wq haki, ni uamuzi wa kinyume na Sheria, na Uamuzi huu haukubaliki.
View attachment 1588258
Kamati kuu ya chama chetu inakutana kesho kujadili jambo hili.

Msimamo wangu Binafsi ni kwamba) Kampeni zinaendelea siku ya Jumapili kama ratiba ya tume ya Uchaguzi inavyosema. Huku nikisubiri Maamuzi ya Kamati kuu.

Ya kwangu kwa leo ni hayo.

Majaliwa anafanya Kampeni Maadili yanakataza

Magufuli anafanya Kampeni kwa kutumia Ratiba yake ambayo sio ya tume na hakuna anayehoji
Lisu anajitoa ufahamu tu
Tume imepeleka balua ofisini kwenu, Mnyika kapokea, kawajibu kwamba hiyo haiwahusu, wampe mgombea mwenyewe!
Kama vile wewe ni mgombea binafsi siyo wa chadema!
Juzi umesikika ikiwa Tarime kwamba huendi kwa kuwa hukapewa balua!
Sasa je
Huna mawasiliana na chama chako?

Ikiwa hili ,wenzio wanajua lile!
Ikifanya ukaidi utaumia
Polisi watakufungua hivyo vyuma ulivyofunga mwilini kwako
 
Back
Top Bottom