Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema ataendelea na Kampeni. Adai Sheria ya Maadili imevunjwa kumsimamisha Kampeni

Tumemwona ndani ya miaka 5, Magufuli hafai.

............watu waliwekwa ndani kwa kutamka tu neno "vyuma vimekaza"!!.
 
Mkwara mbuzi.

Unakatwa na hakuna litalotokea.
 
Tume hii ya Uchaguzi Mkuu 2020 ijitafakari sana kabla haijaleta machafuko makubwa nchini. Mpaka sasa haijapokelewa vizuri na Watanzania.

Imeonyesha udhaifu mkubwa sana kuanzia kushughulikia mapingamizi ya wagombea walioenguliwa kijinga na mpaka leo kusimamia mwenendo wa kampeni. Mnufaika mkubwa wa madhaifu haya na ukosefu wa weledi katika utendaji ni CCM.

Mwenyekiti wa CCM ndiye aliyeiunda Tume hii. Tume yenyewe, bila ya kujiongeza kiakili, imejivubaza kukariri vifungu vya maandiko mbalimbali hewa na ya kinadharia ikijiita kipumbavu eti ipo huru.

Watanzania wanawaangalia tu kwa jicho baya na lenye ufahamu mkubwa kuwa Tume haipo huru. Sasa zimebaki siku chache sana kabla ya uchaguzi.

Wajirekebishe na watende haki. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Wasije wakajuta kuwa hawakujua. Zama zimebadilika. Hii ni dunia ya watu wenye weredi kupita wao. Zama za kuchumia tumbo bila kutenda HAKI zimeisha.
 
Bora afanye kampeni na wajaribu kumzuia ili dunia ione na ikusanye vizuri ushahidi juu ya hawa wauaji na watu wenye roho mbaya

Ingawa hili tu la kumzuia kufanya kampeni kwa siku 7 ni ushahidi tosha

Tumuunge mkono mgombea wetu kwa nguvu zote kuendelea na kampeni zake.

Hawa jamaa si wa kukubalia kucheza ngoma yao kwa mipango yao wanataka jiwe ashinde kwa namna yoyote hata kwa wizi ikibidi.

Sheria, kanuni, taratibu nk zote zimewekwa ili kumwezesha jiwe kwenye hilo.

Kitu cha kufahamu ni nguvu zetu wanazoziona kwenye majukwaa ya kampeni ndizo zinayomuweka Lissu salama hadi sasa. Vinginevyo kisutu na hata mamboleo wangeshafanya yao.

Wao ndiyo wameitisha vurugu. Kama mbwai na iwe mbwai!
 
Tume yetu haina tofauti na ya Uganda. Washenzi watupu wamejazana pale hawajui hata nguvu waliyonayo wanasubiri kusikia jiwe linasema nini. Ningekua naongoza tume jiwe asingegombea mwaka huu kwa uvunjaji wa sheria anaoufanya kwenye kila kampeni.

Inashangaza jiwe anaweza fanya chochote anachojisikia na mtu asimwambie chochote kile, unajua madikteta hua ni madikteta kwa sababu gani? Nchi ya Tanzania vilaza mmezidi duh
 
Tume yetu haina tofauti na ya Uganda. Washenzi watupu wamejazana pale hawajui hata nguvu waliyonayo wanasubiri kusikia jiwe linasema nini. Ningekua naongoza tume jiwe asingegombea mwaka huu kwa uvunjaji wa sheria anaoufanya kwenye kila kampeni. Inashangaza jiwe anaweza fanya chochote anachojisikia na mtu asimwambie chochote kile, unajua madikteta hua ni madikteta kwa sababu gani? Nchi ya Tanzania vilaza mmezidi duh

Katika nukuu za baba wa taifa kulikuwa na hizi:

"Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na sasa tunataka mapinduzi. Mapinduzi yatakayo maliza kupuuzwa kwetu, kuonewa kwetu na kunyanyaswa kwetu ..."

Tukutane Tahrir square yote yataeleweka.
 
Back
Top Bottom