Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema pingamizi ya kufanya kampeni kabla ya wakati ni kelele za kupuuzwa, awananga wahariri wa Vyombo vya Habari

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema pingamizi ya kufanya kampeni kabla ya wakati ni kelele za kupuuzwa, awananga wahariri wa Vyombo vya Habari

Natamani NEC walikate jina lake nione nyie vikaragosi mtafanyaje.

Kama hamataishia kulalama mitandaoni kwa taarifa yako jina tunakata na hakuna lolote mtakalifanya.

Wewe unafikiri mtaleta vurugu muangaliwe tu ...Kwani mkipotezwa watu elfu nchi ikaendelea kuwa salama kuna tatizo.

Jaribuni kuleta vurugu muone na jina tunalikata.
Tusubiri tuone, unaongea as if wewe ndiwe decision executor
Hunijui sikujui don't dare to call me kikaragosi. Alafu wanaopenda maneno kama haya huwa wanamsongo wa mawazo kutokana na kupigwa na maisha mpaka kujubali kuramba viatu kwa buku 7.
Sio mwanachama wa chama chochote ila nasema hivi kutokana na upepo ninaouona wa upinzani na hali halisi nchini
 
BBC wameshajifunza siku hizi kuheshimu kanuni za kurusha maudhui Tanzania story yako lazima ipate upande wa pili.

Hotuba za Lissu ndio zitafanya vyombo vya habari vimkimbie au kuwapelekea kwenye matatizo na TCRA wakiamua kutimiza wajibu wao.

Leo tena ameshutumu watu wengi kwa makosa mbali mbali bila ya ushahidi, ametaja jeshi la polisi kutochunguza mlipuko wa ofisi za CDM Arusha na kuwataja CCM kama wahusika na kudai anao ushahidi.

Sasa hapo waliotajwa upande wao usiposikika kwa wale waliorusha hiyo habari TCRA wakiamua kufanya yao ivyo vyombo vijilaumu vyenyewe.

Kwa utaratibu wa hoja za Lissu atakuwa anavipa vyombo vya habari kazi ya ziada kila wanapoenda msikiliza.
Mkuu huo ndio uhuru wa vyombo vya habari uliomezwa,kama yeye kasema,wao watangaze tu na serikali nayo itafute platform ikanushe...Ndio ustarabu wa dunia.Ila sababu TCRA imekuwa kama kitengo cha CCM kweli wengi wataogopa.Mbona nchi ilikuwa upande mmoja tu,miaka 5 yote JPM kazunguka nchi nzima akiwananga wapinzani na kujipa sifa,hizi siku 21 za Lissu ndio zinawatetemesha hivi?Something is wrong somewhere
 
Issue ni balanced story mfano anauhakika gani ulikuwa ni mkakati wa CCM Arusha kuchoma ofisi za CDM.

Walau angesema anadhani ni wafuasi wa CCM sio kushutumu chama kizima kwa uhakika. Kwakuwa vyombo vya habari vimerusha kama Lissu alivyosema na jamii inaweza amini kilichotamkwa ndio ukweli wenyewe upande wa pili lazima upewe nafasi kwa mujibu wa kanuni.

Anadai polisi awato peleleza unajiuliza wamepeleka majina ya suspects au anataka viongozi wa juu wa CCM Arusha waitwe kutoa maelezo bila ya ushahidi kama walikuwa wanajua huo mkakati.

Tuache kutetea kila kitu ifike hatua tuone kushutumu watu bila ya ushahidi ni tatizo tofauti na ilivyozoeleka ndani ya Tanzania. Mtu anaweza jitungia uongo tu na kupotosha jamii nzima na wengi wetu tusione ilo swala ni tatizo.
 
Issue ni balanced story mfano anauhakika gani ulikuwa ni mkakati wa CCM Arusha kuchoma ofisi za CDM.

Walau angesema wafuasi wa CCM sio kushutumu chama kizima. Kwakuwa vyombo vya habari vimerusha kama Lissu alivyosema na jamii inaweza amini ukweli ndio kilichotamkwa upande wa pili lazima upewe nafasi kwa mijibu wa kanuni.

Anadai polisi awato peleleza unajiuliza wamepeleka majina ya suspects au anataka viongozi wa juu wa CCM Arusha waitwe kutoa maelezo bila ya ushahidi kama walikuwa wanajua huo mkakati.

Tuache kutetea kila kitu ifike hatua tuone kushutumu watu bila ya ushahidi ni tatizo tofauti na ilivyozoeleka ndani ya Tanzania. Mtu anaweza jitungia uongo tu na kupotosha jamii nzima na wengi wetu tusione ilo swala ni tatizo.
Ok
 
Muda huu Lissu anazungumza na vyombo vya habari nchini
Update zaidi kuwafikia
====

Mgombea Urais kupitia chama cha CHADEMA ameelezea ziara yake kwenye mikoa 16 na kufanya mikutano mikubwa na wananchi, amesema vyombo vya habari hasa televisheni hazijaona mikutano hiyo kwa hivyo haikonyeshwa mahali popote.

Lissu amesema lakini mtandaoni unaweza kuona mamia na maelfu ya watanzania wamehudhuria mikutano hiyo. Mikutano inayoonyesha kwamba watanzania wako tayari kwa mabadiliko makubwa kwenye nchi.

Lissu ameendelea kusema watu hawakwenda kumshangaa mtu aliepigwa risasi 16 bali wameenda kumuona kiongozi wanaemfahamu licha ya matatizo aliyopitia amesimama imara kutetea maslahi ya Wananchi na hawakwenda kumshanga kama alivyosema mtu ambae hajamtaja jina.

Lissu amesema Watanzania hawatakuwa tayari kufanyiwa mchezo mchezo kwani ni ujumbe uliotolewa na wananchi kwenye mikutano hiyo.

Lissu amesema anasikia kelele kelele kwamba wanafanya kampeni kabla ya wakati na watawekewa pingamizi. Amesema hayo ni makelele na kwenye sheria ya uchaguzi hamna kosa la kufanya kampeni kabla ya wakati.

Amesema neno kampeni maana yake ni kampeni baada ya kuteuliwa wagombea ambayo amefanya Magufuli kwa miaka mitano kuonyesha anavyofaa hivyo makelele yanaweza kupuuzwa.

Lissu amezungumzia ofisi ya Arusha kuchomwa moto na watu wanaodaiwa wasiojulikana ambao wao tayari wamewajua ni CCM kwani amedai ofisi hiyo imekodishwa kwa mtu ambae ana mahusiano na mgombea udiwani wa CCM na huyo mgombea amesema waliochoma ni viongozi na wanachama wa CCM kata ya Kimandolwa, Arusha Mjini na wamezipeleka polisi kutimiza wajibu kwani hawatafanya lolote.

Pia Lissu amezungumzia barua za mawakili wake ambao wamemuandikia Rais na Jaji Mkuu na kusema mwaka huu hakuna rafu ya watu wasiojulikana tena kwani dunia inatazama na hakuna kujificha. Amesema yeyote ambae atajaribu kuvuruga uchaguzi mwaka huu kutakuwa na 'consequences' ndani ya nchi na nje ya nchi.

Ameendelea kusema kuwa wanataka kushindwa kwenye sanduku la kura na ushindi wa mezani haukubaliki kwa mujibu wa sheria za Tanzania na kimataifa na wao hawatakubali.

Amesema kutakuwa na 'consequences', nchi hii ni tegemezi sana, watoto hasomeshwi bila hela za benki ya dunia na haiwezakani kwenda popote bila misaada ya nchi za nje na nchi hizo zinafuatilia uchaguzi huu kwa karibu kwelikweli.

Mwisho ameviongelea vyombo vya habari, amesema tumekuwa kichekesho cha dunia, ukifungua ITV, Star TV, Channel ten, Uhuru, Jamvi la habari na gazeti lolote mziki ni uleule, CCM CCM, Magufuli Magufuli. Amesema ukitaka uthibitisho ni coverage.

Lissu amesema waandishi waliofika anaamini wakifika wanapeleka kwa wahariri wanaoamua kitu gani kiandikwa na kirushwe. Amesema ni wahariri na Abbas ambae amekuwa mhariri mkuu katika vyombo vyote vya habari nchini.
Hakuna wa kumzuia Lissu Huu mwaka tumepata Mgombea sio yale makapi ya ccm
 
Lissu hawezi kuzungumza bila kuongelea risasi zake​
Hawezi kwenda ikulu kwa kuwaeti alipugwa risasi 100 hakufa​
We wewe ungepigwa risasi moja tu,Tena ya Bastola saa hizi ungeshakua skeleton tu huko kaburini.
Mwache aongelee risasi bana.
 
Mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba kama Tume ya Uchaguzi ikishirikiana na vyombo vya dola kupika matokeo au kuhujumu zoezi la uchaguzi usiwe wa haki wala huru, basi akasema tutaingiza watu barabarani. Akasisitiza kwamba CDM wanataka uchaguzi huru na wa haki.

Baadaye nikamsikia msemaji wa CCM ndugu Simon Sirro akisema “wamesema wataingiza watu barabarani” Sirro ilifanya kitu tunaita cherry picking of words. Aliacha maneno Uchaguzi huru na uchaguzi wa haki.

Natambua kwamba Simon Sirro ni IGP, lakini wanasema

“if it looks like a duck, swims like a duck, and quacks like a duck, then it probably is a duck”
 
Hivi Sirro atastaafu lini? maana naona age yake haina tofauti na ya JK
 
Hivi Sirro atastaafu lini? maana naona age yake haina tofauti na ya JK
Siro alishafikisha umri wa kustaafu tokea mwaka 2016 lakini mtukufu kaamua kwenda nae kienyeji tu mpaka siku akiona kazeeka sana ndipo atamruhusu kwenda kulea wajukuu wake
 
Mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba kama Tume ya Uchaguzi ikishirikiana na vyombo vya dola kupika matokeo au kuhujumu zoezi la uchaguzi usiwe wa haki wala huru, basi akasema tutaingiza watu barabarani. Akasisitiza kwamba CDM wanataka uchaguzi huru na wa haki.

Baadaye nikamsikia msemaji wa CCM ndugu Simon Sirro akisema “wamesema wataingiza watu barabarani” Sirro ilifanya kitu tunaita cherry picking of words. Aliacha maneno Uchaguzi huru na uchaguzi wa haki.

Natambua kwamba Simon Sirro ni IGP, lakini wanasema

“if it looks like a duck, swims like a duck, and quacks like a duck, then it probably is a duck”
.....a duck all day long!
 
Back
Top Bottom