Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wameshaumbuka.unajua Lissi kawashika kweli kweliMgombea urais wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba kama Tume ya Uchaguzi ikishirikiana na vyombo vya dola kupika matokeo au kuhujumu zoezi la uchaguzi usiwe wa haki wala huru, basi akasema tutaingiza watu barabarani. Akasisitiza kwamba CDM wanataka uchaguzi huru na wa haki.
Baadaye nikamsikia msemaji wa CCM ndugu Simon Sirro akisema “wamesema wataingiza watu barabarani” Sirro ilifanya kitu tunaita cherry picking of words. Aliacha maneno Uchaguzi huru na uchaguzi wa haki.
Natambua kwamba Simon Sirro ni IGP, lakini wanasema
“if it looks like a duck, swims like a duck, and quacks like a duck, then it probably is a duck”
CCM wameanza kampeni tokea 2016 mtukufu akigawa pesa anafanya mikutano huku kazuia vyama vingine kufanya mikutano ya siasa na juzi juzi kafanya kampeni kabla ya wakati kule Rufiji kamtafutia mama yake mzazi mchumba na kununua jogoo kwa laki moja ikiwa ni Rushwa ya wazi kabsa.Vigezo na masharti kuzingatiwa, kama hatimizi atakatwa, wote tunapitia hayo kwenye maisha yetu, tusipotimiza vigezo vilivyowekwa aidha kwa kujua au kutokujua tunakatwa, ...
Siro hana kinga ya kutoshitakiwa lakini magufuli ana kinga, siku magufuli hayupo madarakani kumlinda siro ataishia kushinda mahakamani ale kiinua mgongo akiwa kizimbani mda wote wa uzeeniSirro ana copy kila neno analoongea Magufuli na yeye analirudia, japo Magufuli ni bosi wake lakini akumbuke kwa nafasi yake (Sirro) anatakiwa awe makini sana na maneno anayozungumza, kwasababu kukopi kila neno toka kwa Magufuli yule ni mwanasiasa asije akajiingiza kwenye huo mtego.
Hicho kigezo chako ni cha kibwege sana hutumii hata Akili yako ndogo ya kufua chupi? Hujui kuwa binadamu akishambuliwa hujitahidi kuficha kichwa? Acheni maswali ya kijinga jingaZote hizo hakuna hata moja iliompata usoni?
Week yote hii kumekuwa na vikao kati ya IGP Siro, Jaji kaijage wa NEC, Shibuda kubwa jinga na Lipumba ni vikao vya kuivuruga kuihujumu kuidhoofisha chadema na kumzuia Tundu lisu kugombea Urais 2020Kwa maana nyingine Zirro anatuambia kwamba NEC na vyombo vya Dola vitapora ushindi wa CHADEMA...!!
Matatizo ya kuongea bila kufikiri
Walaaniwe!Week yote hii kumekuwa na vikao kati ya IGP Siro, Jaji kaijage wa NEC, Shibuda kubwa jinga na Lipumba ni vikao vya kuivuruga kuihujumu kuidhoofisha chadema na kumzuia Tundu lisu kugombea Urais 2020
Alificha kichwa kwenye mchanga?alikificha na viganja?Hicho kigezo chako ni cha kibwege sana hutumii hata Akili yako ndogo ya kufua chupi? Hujui kuwa binadamu akishambuliwa hujitahidi kuficha kichwa? Acheni maswali ya kijinga jinga
CCM wameanza kampeni tokea 2016 mtukufu akigawa pesa anafanya mikutano huku kazuia vyama vingine kufanya mikutano ya siasa na juzi juzi kafanya kampeni kabla ya wakati kule Rufiji kamtafutia mama yake mzazi mchumba na kununua jogoo kwa laki moja ikiwa ni Rushwa ya wazi kabsa.
risasi mmchape halafu kuzungumza mmkataze. akili za wapi hiziLissu hawezi kuzungumza bila kuongelea risasi zakeHawezi kwenda ikulu kwa kuwaeti alipugwa risasi 100 hakufa
We endelea kupiga kelele, ukipata akili Magufuri atakuwa tayari ameapishwa na yupo ikulu ya Chameino!Muda huu Lissu anazungumza na Vyombo vya Habari nchini
Update zaidi kuwafikia
====
Mgombea Urais kupitia chama cha CHADEMA ameelezea ziara yake kwenye mikoa 16 na kufanya mikutano mikubwa na wananchi, amesema vyombo vya habari hasa televisheni hazijaona mikutano hiyo kwa hivyo haikonyeshwa mahali popote.
Lissu amesema lakini mtandaoni unaweza kuona mamia na maelfu ya watanzania wamehudhuria mikutano hiyo. Mikutano inayoonyesha kwamba watanzania wako tayari kwa mabadiliko makubwa kwenye nchi.
Lissu ameendelea kusema watu hawakwenda kumshangaa mtu aliepigwa risasi 16 bali wameenda kumuona kiongozi wanaemfahamu licha ya matatizo aliyopitia amesimama imara kutetea maslahi ya Wananchi na hawakwenda kumshanga kama alivyosema mtu ambae hajamtaja jina.
Lissu amesema Watanzania hawatakuwa tayari kufanyiwa mchezo mchezo kwani ni ujumbe uliotolewa na wananchi kwenye mikutano hiyo.
Lissu amesema anasikia kelele kelele kwamba wanafanya kampeni kabla ya wakati na watawekewa pingamizi. Amesema hayo ni makelele na kwenye sheria ya uchaguzi hamna kosa la kufanya kampeni kabla ya wakati.
Amesema neno kampeni maana yake ni kampeni baada ya kuteuliwa wagombea ambayo amefanya Magufuli kwa miaka mitano kuonyesha anavyofaa hivyo makelele yanaweza kupuuzwa.
Lissu amezungumzia ofisi ya Arusha kuchomwa moto na watu wanaodaiwa wasiojulikana ambao wao tayari wamewajua ni CCM kwani amedai ofisi hiyo imekodishwa kwa mtu ambae ana mahusiano na mgombea udiwani wa CCM na huyo mgombea amesema waliochoma ni viongozi na wanachama wa CCM kata ya Kimandolwa, Arusha Mjini na wamezipeleka polisi kutimiza wajibu kwani hawatafanya lolote.
Pia Lissu amezungumzia barua za mawakili wake ambao wamemuandikia Rais na Jaji Mkuu na kusema mwaka huu hakuna rafu ya watu wasiojulikana tena kwani dunia inatazama na hakuna kujificha. Amesema yeyote ambae atajaribu kuvuruga uchaguzi mwaka huu kutakuwa na 'consequences' ndani ya nchi na nje ya nchi.
Ameendelea kusema kuwa wanataka kushindwa kwenye sanduku la kura na ushindi wa mezani haukubaliki kwa mujibu wa sheria za Tanzania na kimataifa na wao hawatakubali.
Amesema kutakuwa na 'consequences', nchi hii ni tegemezi sana, watoto hasomeshwi bila hela za benki ya dunia na haiwezakani kwenda popote bila misaada ya nchi za nje na nchi hizo zinafuatilia uchaguzi huu kwa karibu kwelikweli.
Mwisho ameviongelea vyombo vya habari, amesema tumekuwa kichekesho cha dunia, ukifungua ITV, Star TV, Channel ten, Uhuru, Jamvi la habari na gazeti lolote mziki ni uleule, CCM CCM, Magufuli Magufuli. Amesema ukitaka uthibitisho ni coverage.
Lissu amesema waandishi waliofika anaamini wakifika wanapeleka kwa wahariri wanaoamua kitu gani kiandikwa na kirushwe. Amesema ni wahariri na Abbas ambae amekuwa mhariri mkuu katika vyombo vyote vya habari nchini.
umeamua kuwa upande Wa madikteta? Yaani MTU atoe hotuba halafu usiirushe live mpaka ukamuulize upande Wa pili? You must be joking! Kama stori haiko sawa jibu, kama unaona umeonewa nenda mahakamani! Hii sheria ya hovyo kabisa, TCRA na Waziri Wa habari wamepewa rungu na sheria kuua Uhuru Wa habari, Jiwe anapita na kuropoka hovyo hatujasikia hatua zozote toka kwa wanafiki wakubwa hawa!Issue ni balanced story mfano anauhakika gani ulikuwa ni mkakati wa CCM Arusha kuchoma ofisi za CDM.
Walau angesema anadhani ni wafuasi wa CCM sio kushutumu chama kizima kwa uhakika. Kwakuwa vyombo vya habari vimerusha kama Lissu alivyosema na jamii inaweza amini kilichotamkwa ndio ukweli wenyewe upande wa pili lazima upewe nafasi kwa mujibu wa kanuni.
Anadai polisi awato peleleza unajiuliza wamepeleka majina ya suspects au anataka viongozi wa juu wa CCM Arusha waitwe kutoa maelezo bila ya ushahidi kama walikuwa wanajua huo mkakati.
Tuache kutetea kila kitu ifike hatua tuone kushutumu watu bila ya ushahidi ni tatizo tofauti na ilivyozoeleka ndani ya Tanzania. Mtu anaweza jitungia uongo tu na kupotosha jamii nzima na wengi wetu tusione ilo swala ni tatizo.