Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema pingamizi ya kufanya kampeni kabla ya wakati ni kelele za kupuuzwa, awananga wahariri wa Vyombo vya Habari

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu asema pingamizi ya kufanya kampeni kabla ya wakati ni kelele za kupuuzwa, awananga wahariri wa Vyombo vya Habari

"SISI ni watu wa AMANI, SISI ni watu wa AMANI. Hatutapiga mtu, hatutaibia mtu, hatutamfanyia mtu vurugu. Hatutakubali KUPIGWA. Hatutakubali kufanyiwa VURUGU. Hatutakubali KUIBIWA. Hatutakubali KUONEWA. Tunataka UCHAGUZI HURU na wa HAKI. Tutakubali, tutakubali tukishindwa kwa HAKI".

Haya ni maneno mazito sana; na yaliyojaa busara hekima na ujasiri aliyoyasema Lissu akiwa katika ziara ya kutafuta wadhamini huko Tunduma, Watanzania tuzingatie haya, tusijesema hatukuambiwa.

Sent from my H8216 using JamiiForums mobile app
 
Nimemsikiliza mpaka ilipokatika na nahisi kuna ujumbe mzito.Jambo la kwanza siamini kama kweli JPM ana hofu kubwa ya kushindwa kiasi hicho ila kuna watu ndani ya CCM na serikali (rogue elements) ambao wanataka kumfurahisha JPM kwa kudhulumu haki za wengine.hili linatakiwa JPM mwenyewe alikemee la sivyo linamtia doa na kumpaisha Lissu bila sababu.

Jambo la pili ni kesi zinazomkabili Lissu,busara itumike amalizane na uchaguzi then apambane na kesi zake za uchochezi na hapo hata akienda Segerea sympathizers watakuwa wachache kuliko ikifanyika leo.

Jambo la tatu ni vyombo vya dola,kukwepa double standard na kuzipa tuhuma zote uzito sawa na tayari mfano Tulia Ackson na Sugu umeshaingia ndani ya records.

Jambo la nne ni tume ya uchaguzi ionyeshe anagalu kuwa iko concerned na yaliyotokea angalau hata kwa uwaondoa katika usimamizi wa uchaguzi wale wote wanaoonekana kwenda kinyume na kanuni hasa hao ambao wamenyima wapinzania fomu au kutoa fomu kwa mtu mwingine.

Jambo la tano ni kauli ya Lissu kuwa watakubali kushindwa katika uchaguzi huru na wa haki.Angalau NEC itusaidie kuonyesha kuwa mchakato ulikuwa huru na wa haki ili Lissu akishindwa tusaidiane na CCM kumzomea.

Kama tulivyopata habari za msiba wa Mkapa na tukahuzunika na tukamzika ndivyo uchaguzi utakavyopita,tutafurahi/kuhuzunika lakini mwisho wa siku maisha ni lazima yaendelee.
IGP na mkurugenzi wa NEC jaji kaijage wapo kwenye uchunguzi mkubwa wa siri na vyombo vya uchunguzi vya kimataifa zikiwemo taasisi za haki za binadamu na mahakama ya uhalifu The Hague
 
Kumetokea nini?

Maana hii video yako imefika dakika ya 36:38 ikaanza kupiga honi mfululizo na video kukata moja kwa moja....

Kama kuna iliyo njema mpaka mwisho, turushie tafadhali...

Binafsi nina shauku kubwa mno kumtazama na kumsikiliza Mh. Rais wetu, Ndg Tundu A.M. Lissu...

Yaani nina bajeti maalumu ya bando kwa ajili ya kufuatilia chochote kumhusu Tundu Lissu...!
Wamezingua sana kwenye maswali wa kazima kabisaa
 
Lipumba na shibuda wamechukua pesa toka CCM juzi kwa ajili ya kwenda kumwekea pingamizi Tundu lisu ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi

Kama ni hivi na wagombea wote mapingamizi na hasa huyu mzee ambaye anakesha akiwachulia CDM.

Kama vipi tukashindanie na mapingamizi pia.
 
Lissu ameendelea kusema watu hawakwenda kumshangaa mtu aliepigwa risasi 16
Ashikilie hapahapa!!! Mimi mwenyewe nilienda kushangaa hikihiki anachobisha, na Kura yangu haipati, Maana Kwa picha ni Lisu lakini ndani yake sivyo tumwonavyo
 
Akiacha kutumia lugha za matusi mbele ya cyombo cya habari watamrusha tu hewani tena MUBASHARA 🧐🧐🧐
 
Lissu hawezi kuzungumza bila kuongelea risasi zake​
Hawezi kwenda ikulu kwa kuwaeti alipugwa risasi 100 hakufa​
MKUU HAAKUPIGWA RISASI YULE HAYAWANI ILA ALIPARAZWA PARAZWA TU ZILE
 
Awe makini tu, nakumbuka hata kipindi kile alituambia Ndugai wala nani hawezi kumvua ubunge wake na vifungu kibao tu vya sheria akatutajia ila mwisho wa siku wote tuliona nini kilitokea.

Hata kwenye ubunge wa Nasari pia alituambia mambo hayohayo ya Sheria this sheria that.

BTW:Miaka yote dunia inafuatilia chaguzi za nchi hii kupitia mifumo rasmi ya mabalozi na waangalizi wao wa uchaguzi na miaka yote hiyo toka 1995 hizo kelele za rough zinasikika tu.

Hao Amsterdam & Partners ndo dunia anayoizungumzia?
 
Sasa wakate jina la TL kwa vigezo vya ccm ndipo watajua hasira za wananchi zimefukuliwa wapi, maana walizoea kuwachukulia watanzania kama mazombi kwamba lolote wanaloamua wao kwa maslahi yao linafuatwa... Watanzania wasasa sio wa 2010 wala 2015 kimtazamo na kiuthubutu
Dawa ni kuwapa kichapo cha mbwa koko kubwa jinga Shibuda na Profeselii Lipumba waliotumwa na CCM kwenda kufanya ushetani wao.
 
Ashikilie hapahapa!!! Mimi mwenyewe nilienda kushangaa hikihiki anachobisha, na Kura yangu haipati, Maana Kwa picha ni Lisu lakini ndani yake sivyo tumwonavyo

Basi utakuwa ni mshamba fulani, maana kama ni kumuona hata kwenye media anaonekana sana tu. Halafu ww unaoonekana utakuwa ni jizee fulani ambaye umejua kutumia mitandao hivi karibuni, ndio maana unashoboka na stori za kipuuzi.
 
Back
Top Bottom