Tundu Lissu ashauriwe ajisalimishe kwa serikali atoke magereza, anateseka bure tu

Tundu Lissu ashauriwe ajisalimishe kwa serikali atoke magereza, anateseka bure tu

Mkuu, kama watu wangekua wanasikiliza ushauri wako kusingekua na mabadiliko ya aina yeyote duniani.
Hakuna mabadiliko yatakayopatikana Tanzania miaka ya karibuni bila ridhaa ya CCM, CCM kugawanyika au nguvu kubwa zaidi ya CCM, soma alama za nyakati wafahamu watu wa nchi yako vizuri.
 
Hiki ndicho wanachotaka waliomfikisha pale.
Back breaking (demoralizing).
Break him and his supporters emotionally.
Lengo yeye au wafuasi wake wakate tamaa asitokee tena shujaa wa kujaribu hayo mapambano.
 
Watu walio karibu na Tundu Lissu wamshauri ajisalimishe kwa serikali ya CCM atoke magereza tu, hakuna atakachofanikisha kwa Tanzania ya sasa kwa kuendelea na msimamo wake huo, hakuna watu wengi walio tayari kupambania sambamba naye kwa vitendo kile anachopambania yeye.
Sasa mkuu kwenye mapambano seriously mkiwa wengi hamwezi kufanikisha , maana kuna ma snitch humo humo bora muwe wachache , wenye nia moja , msimamo mmoja .

Hakuna sababu ya kuendelea kushikilia huo msimamo na kutesekea gerezani wakati haitaleta utofauti wowote.
Hii ni probability mkuu labda kama umeanza kufuatilia haya mambo baada ya magufuli kushinda u_rais .
Unakumbuka kipind cha Arabic spring Muamar ghadaf na mwanae seif al Islam ghadaf walikuwa wanawaita waandamanaji panya lakini
Mwishoe ilijulikana panya nani .

Hata wakina maendelo inawezakan kuna waliokuwa na mtazamo kama wako ya kwamba hataleta utofauti wowote ila mwisho tunaujua
Je harakati za . Aung San Suu Kyi kule burna [Myanmar] ulizifuatilia kipindi hicho hadia anakuja kufanikisha kuwa state counsellor ,
Mifano ni mingi tusibeze anachofanya LISU kama ana nia njema.
 
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa..-Muhubiri 3:1-8
Yes, I agree with these scriptures

Ni kazi kwako, kazi kwao na kazi kwa yeyote kuwa akili na ufahamu wa rohoni kutambua, tuko kwenye majira na nyakati gani sasa!

Kazi kwako na kwa yeyote kuweza kuona kwa macho ya rohoni ili kujua tuko kwenye majira na nyakati za kuzaliwa, kufa, kupanda, kulia, kucheka au kung'oa
 
Watu walio karibu na Tundu Lissu wamshauri ajisalimishe kwa serikali ya CCM atoke magereza tu, hakuna atakachofanikisha kwa Tanzania ya sasa kwa kuendelea na msimamo wake huo, hakuna watu wengi walio tayari kupambania sambamba naye kwa vitendo kile anachopambania yeye.

Hakuna sababu ya kuendelea kushikilia huo msimamo na kutesekea gerezani wakati haitaleta utofauti wowote.
Ni lazima unaowatetea au kuwapigania wakupambanie? Thawabu ya kujitoa kwako kwa ajili ya watu hutolewa kwa nani..kwako peke yako au keako na wale wanakupambania..mbona Lissu alipojeruhiwa kwa risasi hakuna aliyesema km haya unayosema? Una uhakika Lisu anaumia sana kuwa gerezani zaidi ya maumivu ya risasi alizopigwa wakati ule? Acha unafiki..mwache Lisu atimize kile dhamira yake inamuongoza kufanya!
 
Watu walio karibu na Tundu Lissu wamshauri ajisalimishe kwa serikali ya CCM atoke magereza tu, hakuna atakachofanikisha kwa Tanzania ya sasa kwa kuendelea na msimamo wake huo, hakuna watu wengi walio tayari kupambania sambamba naye kwa vitendo kile anachopambania yeye.

Hakuna sababu ya kuendelea kushikilia huo msimamo na kutesekea gerezani wakati haitaleta utofauti wowote.
Maneno haya ungemshauri mandela wakati ule ungeuliwa sekunde tu.
Mwacheni huenda tukaona Tanzania anayoiwaza
 
Hakuna mabadiliko yatakayopatikana Tanzania miaka ya karibuni bila ridhaa ya CCM, CCM kugawanyika au nguvu kubwa zaidi ya CCM, soma alama za nyakati wafahamu watu wa nchi yako vizuri.
Unamkumbuka aliyeita raia wake wanaompinga panya..yupo? Nini kilimtokea..! ccm ya wanawake unaona kuna kitu hapo..punguani ndio hawezi kuona kile kinakuja kuwapata ccm muda si mrefu!
 
Mifano ni mingi tusibeze anachofanya LISU kama ana nia njema.
Ndugu Tachu hano mpaka sasa una doubt na nia ya Tundu Lissu ktk mapambano haya?

Huyu ndugu Tundu Lissu kama nia yake ingekuwa kupata personal benefits kupitia harakati zake hizi, angekushakuwa tajiri wa pesa za damu za Watanzania na dhuluma kitambo sana

Za ndani kabisa, zinasema huko huko aliko gerezani timu za watu maarufu kadhaa zimeshamfuata kumtaka abadili au alegeze msimamo ili ale mema ya nchi, AMEKATAA KATA KATA!

Unamkumbuka Dr Ulimboka aliyetekwa na kupigwa sana na utawala wa Kikwete kwa kuongoza mgomo wa madaktari miaka ya 2011?

Yuko wapi? Aliufyata na hajawahi kuonekana tena.

Huyo alipata kipigo cha mateke na fimbo tu. Huyu Tundu Lissu ni survivor wa risasi 16 zilizichakazwa mwili wake. Lakini hajawahi kuogopa wala ku - back-down mapambano haya

Huyu jamaa ni very unique creature

Sisi wengine tusioweza kuhimili mateso hayo ya kimwili, tunaweza kushirikiana naye ktk namna nyingine most importantly kumpa moral and emotional support, financial support, kupiga magoti na kumwombea kila siku kila wakati ili akibebe na kukinywea salama kikombe alichonacho kwa ajili ya wengi

Ni kazi ngumu sana anayofanya. Lakini kwa msaada wa Mungu Jehovah, yote yanawezekana. Amina🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Hawatamnyonga kwa kamba ila watamnyonga kwa kuhakikisha anaozea gerezani huku watu wakiendelea na maisha mengine bila kujali.
Jamaa Nilikuwa nakuheshimu lakini leo nimekuona bonge la kilaza. Kwani mtu anapokuwa na harakati zake wewe unaathirika na nini?
 
Hakuna mabadiliko yatakayopatikana Tanzania miaka ya karibuni bila ridhaa ya CCM, CCM kugawanyika au nguvu kubwa zaidi ya CCM, soma alama za nyakati wafahamu watu wa nchi yako vizuri.
Ni kweli unaongea uhalisia, lakini hapa kuna mawili either ccm kugawanyika yenyewe au kugawanywa. Inawezekana ikatumika nguvu ya ndani yake au ikatumika nguvu ya kutoka nje na zote zinazweza kuwa na matokeo au zisiwe nayo.
Kwa kinachoendelea sasa kuanzia viwango vya uchaguzi wa ndani wa cdm, hadi wengine wanakimbia, viongozi waliokuwepo wanaenda mahakamani kuwashitaki viongozi ambao hawajakaa ofisini hata mwezi kulinganisha na wao waliokaa miaka 15+, vyote hivi ni eye opener jinsi siasa za nchi zilivyojaa utapeli na ujinga.
Lakini ukigeukia upande wa mwananchi wa kawaida yeye anaonyesha wazi kutaka mabadiliko.
NOTE: Kwenye historia ya hii nchi miaka 60+ jumuiya za kimataifa hazijawahi kuiangalia negatively kiasi hiki na wanashangaa kitu kama kutopinga matokeo ya uchaguzi mahakani!

Uhaguzi huru na haki walau kwa 70% ni takwa la kijamii na la muda mbali na hapo watatekwa na kuumizwa watu wengi pamoja na ccm wenyewe.
 
Watu walio karibu na Tundu Lissu wamshauri ajisalimishe kwa serikali ya CCM atoke magereza tu, hakuna atakachofanikisha kwa Tanzania ya sasa kwa kuendelea na msimamo wake huo, hakuna watu wengi walio tayari kupambania sambamba naye kwa vitendo kile anachopambania yeye.

Hakuna sababu ya kuendelea kushikilia huo msimamo na kutesekea gerezani wakati haitaleta utofauti wowote.
akili ya wafu hii
 
Hata wewe?!
 
inasikitisha sana, upo sahihi kwa asilimia 100. Ila tarajia matusi kutoka kwa vijana wa Chadema wenzio.
 
Back
Top Bottom