PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu Mkurugenzi wao wa habari, asaidiwe, The Correct title ya TAL ni Mwenyekiti wa Taifa.wa Chadema na sio Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Niko shocked na taarifa hii
Pre GE2025 - Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Huu ni muendelezo wa udikiteta wa TAL ndani ya Chadema!.

Hii tengua tengua, itafuatiwa na kikao cha dharura cha CC yao kukaa kama a kangaroo court na kuwatimua timua hawa 55!.
Lissu atafukuza wangapi?, Chadema itabakiwa na nani na nini?!
P
Kwa mfano tuseme ikatokea ajali hao wote hawapo chadema haitaendelea,na hata muda huu tunaongea wanamchango gani
 
Wamesema wazi kuwa wanaunga mkono Reforms. Shida ni kuwa mmetanguliza suala la wao kupingana na Lissu.

Hilo la asilimia ngapi litajulikana hapo baadae. Nimesema kuwa CCM hawafanya kosa la kuhakikisha wanashinda 100% maana ndicho kilicho walazimisha kuwaingiza wakina Halima Bungeni. Kwa taratibu za Bunge kuna kamati ni lazima ziongozwe na ziwe na wajumbe wa upinzani. Wakishinda 100% kamati hizo zitakosa legitimacy.

Mimi nadhani badala ya kuwananga wakina G55 viongozi wa CDM waseme bayana watafanya nini kama hapatakuwa na Reforms. Na deadline ya uamuzi wa Reforms ni lini.

Amandla...
Muda utaamua
 
Kilewo katia nia kugombea jimbo la kawe 😹😹😹
Hao G55 wanachekesha sana..!!
 
..kina Halima waliingizwa kimagumashi kwasababu Kamati Kuu ya Chadema waliweka mgomo kuidhinisha wabunge wa viti maalum.

..ahadi kwamba 2025 CCM watalainika, inatokana na ushahidi, au viashiria vipi? G55 wanatoa wapi madai hayo?

..kwa maoni yangu G55 wamefanya haraka kupinga " No Reforms No election. " Pia kama hawaamini katika maamuzi ya chama, hawakupaswa kuwa katika nafasi za uongozi. Wangewaachia wenzao wanaoamini ktk kampeni hiyo washike nafasi za uongozi.
Waliingizwa kimagumashi kwa sababu CCM walijua bila wapinzani Bunge litakosa uhalali. Ndio maana walifikia hatua ya kumtoa mtu rumande ili aapishwe.

Hakuna anayesema kuwa CCM watalainika. Kama watafanya hivyo ni kwa sababu ya circumstances tu.

Nashauri ungeenda beyond "headings". Ukisoma waraka wenyewe utaona wazi kuwa hakuna mahali G55 wamepinga Reforms. Wanachopinga wao ni njia ya kulazimisha hizo reforms. Aidha, kiukweli ni kuwa pamekuwa na uhudi za waziwazi za kuwa sideline wale ambao wanadiriki kutofautiana na Mwenyekiti au ambao wanashukiwa kuwa bado ni loyal kwa Mwenyekiti aliyepita. Badala ya kufanya jitihada za kutibu majeraha wengi wameona kuwa huu ni wakati wao na wengine hawana nafasi. Kuanzia Mwenyekiti kumsema vibaya Aida mpaka hii ya Sagrada mwendo ni huo huo. Hawa wamefikishwa ukingoni na jinsi wanavyokuwa treated. kwenye hilo uongozi wa sasa hawezi kukwepa lawama.

Amandla...
 
..siamini kama Raisi Samia anaweza kukataa Reforms, wakati ni moja ya nguzo za 4R.

..Reforms ni chaguo bora lenye manufaa kwa Watanzania wote.
Reforms ambazo zinaweza kumtoa madarakani? Ingekuwa ni hivyo angetoa kauli kuhusu namna uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyofanyika na angewachukulia hatua waliosimamia. Raisi Samia ni CCM damu damu na survival ya chama chake ndio priority yake.

Amandla...
 
Waliingizwa kimagumashi kwa sababu CCM walijua bila wapinzani Bunge litakosa uhalali. Ndio maana walifikia hatua ya kumtoa mtu rumande ili aapishwe.

Hakuna anayesema kuwa CCM watalainika. Kama watafanya hivyo ni kwa sababu ya circumstances tu.

Nashauri ungeenda beyond "headings". Ukisoma waraka wenyewe utaona wazi kuwa hakuna mahali G55 wamepinga Reforms. Wanachopinga wao ni njia ya kulazimisha hizo reforms. Aidha, kiukweli ni kuwa pamekuwa na uhudi za waziwazi za kuwa sideline wale ambao wanadiriki kutofautiana na Mwenyekiti au ambao wanashukiwa kuwa bado ni loyal kwa Mwenyekiti aliyepita. Badala ya kufanya jitihada za kutibu majeraha wengi wameona kuwa huu ni wakati wao na wengine hawana nafasi. Kuanzia Mwenyekiti kumsema vibaya Aida mpaka hii ya Sagrada mwendo ni huo huo. Hawa wamefikishwa ukingoni na jinsi wanavyokuwa treated. kwenye hilo uongozi wa sasa hawezi kukwepa lawama.

Amandla...

..Mwenyekiti katika hotuba yake kwa watia nia amewaasa wawavumilie G55.

..Mwenyekiti alishakwenda jimboni kwa Aida na walishirikiana vizuri.

..Mwenyekiti amekwenda kanda ya Nyasa na amezunguka na Sugu ziara nzima.

..Mwenyekiti alimteua Catherine Ruge pamoja na kwamba alishindwa uchaguzi.

..Sigrada alikuwa katika kikao cha kutibu majeraha lakini there is no clear picture of what really happened.

..G55 wamefanya haraka kupinga " No Reforms No Election. " Walipaswa kuwa na subira kuwapa nafasi wale wanaoamini ktk kampeni hiyo wawafikie wananchi.

..Kitendo cha G55 kupinga " No Reforms No Elections " ni kukididimiza chama, na sio kukijenga.
 
Mwanzoni sikukubaliana na Lissu kugombea uenyekiti ila now naaanza kuelewa kwanini alifanya vile. Nadhani Mbowe kuna kiini macho alikuwa anatufanyia. Bora mnyukano huu umetokea angalau sasa tunajua panapovuja ni wapi
Mbowe ni mtu wa System anakitambulisho chekundu mwisho
Huyu Mkurugenzi wao wa habari, asaidiwe, The Correct title ya TAL ni Mwenyekiti wa Taifa.wa Chadema na sio Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Niko shocked na taarifa hii
Pre GE2025 - Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Huu ni muendelezo wa udikiteta wa TAL ndani ya Chadema!.

Hii tengua tengua, itafuatiwa na kikao cha dharura cha CC yao kukaa kama a kangaroo court na kuwatimua timua hawa 55!.
Lissu atafukuza wangapi?, Chadema itabakiwa na nani na nini?!
P
Tanzania ina watu sio chini ya milioni 60 kufukuza watu 55 ndo Useme chadema itabaki na nani kitu ambacho hujui nikujuze Chadema sasa hivi imerudi kwa wananchi Lissu na Wananchi wanaongea Lugha moja. na ogopa sana chama kikirudi kwa wananchi aisee tulia CCM Gia zilishakataa kuingia hata uwambie nini CCM hawezi kukusikiliza CCM huwambii chochote wakakuelewa na Lisuu ni Mteremko mkali wenye kona kali sana
 
Hiyo timua timua inasubiri yeye kutimuliwa
Lisu ni dikteta uchwara huwa hana kifua cha kuhimili critics wake wawe waandishi wa habari au ndani ya chama au nje huwa ana loose temper haraka mno

Anataka tu watu wa kumuabudu na kumsifu wakati yeye hiyo tabia hana ya kuabudu na kusifu wengine akiweno bosi wake Mbowe akiwa bosi wake

Sasa Wanachadema wameshamuelewa kama dikteta uchwara ndio maana wameshaanza lumwashia taa za hazard bila woga
Lisuu yupo sana Mzee Uongo hauwezi kushinda na Ukweli ukatoboa nakwambia Lissu kwenye hii hoja yangu ni mtu mkweli kwa hiyo yupo yupo sana
 
Huyu jamaa ana
Umekuja kuwapa sapoti G55 Ila Lissu ni Tsunami amekuondolea uwezo kabisa wa Developing Story zako na kufikiri kwa kina hakika Mzee umezeeka sa

Kwani umesahau Mbowe alisema atastaafu akifika umri wa Miaka 68 kama alivyofanya Mzee Mtei?Lakini kwa Mziki wa Lissu alistaafu kabla ya muda aliojipangia.
Lissu ni muujiza unaoishi leo Magufuli na Mkapa wako wapi ila Lissu yupo
 
..Mwenyekiti katika hotuba yake kwa watia nia amewaasa wawavumilie G55.

..Mwenyekiti alishakwenda jimboni kwa Aida na walishirikiana vizuri.

..Mwenyekiti amekwenda kanda ya Nyasa na amezunguka na Sugu ziara nzima.

..Mwenyekiti alimteua Catherine Ruge pamoja na kwamba alishindwa uchaguzi.

..Sigrada alikuwa katika kikao cha kutibu majeraha lakini there is no clear picture of what really happened.

..G55 wamefanya haraka kupinga " No Reforms No Election. " Walipaswa kuwa na subira kuwapa nafasi wale wanaoamini ktk kampeni hiyo wawafikie wananchi.

..Kitendo cha G55 kupinga " No Reforms No Elections " ni kukididimiza chama, na sio kukijenga.
Amewaasa wawavumilie halafu baada ya waraka kutoka anamtimua Ruge! Tunaangalia vitendo sio matamshi.

Ali apologise kuwa hakumtendea haki? Au ni yale kiongozi hakosei?

Angeachaje kuzunguka na Sugu wakati dio Mwenyekiti wa Kanda? Hata yeye anajua isingeleta picha nzuri.

Alimteua Ruge kwa sababu ya weledi wake na sio favor. Ila inaelekea alitegemea pengine ingemyamazisha. Amesahau kuwa huyu ni mmoja wa wachache katika uongozi wa Bawacha waliokataa kuwaunga mkono wakina Halima. Ana msimamo na hanunuliki.

Haujui kuwa Sagrida alipigwa na mlinzi wa Heche? Au na wewe unaamini propaganda kuwa yalikuwa na maigizo? Alitolewa nje baada ya kung'ang'ania apewe nafasi ya kutosha kuzungumzia jinsi anavyoonewa. Kitu ambacho hawakuwa tayari kusikia maana aliishapatikana na hatia na kilichokuwa kinasubiriwa ni hukumu tu.

Ulitaka wasubiri mpaka lini ndio watoe dukuduku zao? Wakati dirisha ndio hilo linaelekea kufungwa.

Narudia tena, G55 hawajapinga Reforms. Hata hiyo ya "No elections" hawajaipinga. Wao wanatofautiana na njia inayofuatwa kufikia hapo. Wanachodai ni kusikilizwa na kutendewa haki. Katika waraka wao wamesema wazi wako tayari kukubaliana na maamuzi yeyote ya kikao ili mradi wasikilizwe.

Amandla...
 
Kiongozi wa upinzani asiye dalali awezi kuwa you bwatu bwatu. Anayefanya udalili wa nchi yetu kwa akina Amsterdam.
Sasa hivi wananchi tuna uwezo wa kuchuja, dalali wa kisiasa anajulikana kwa matendo yake na wachumia tumbo wanajulikana kwa matendo yao.ukimsema TAL bwatu bwatu tunakuona kama na wewe ni miongoni mwa madalali hao, kwa sababu anachozungumza TAL kina ukweli kabisa kuhusu uchaguzi, tumejionea wenyewe chaguzi kadhaa
 
Amewaasa wawavumilie halafu baada ya waraka kutoka anamtimua Ruge! Tunaangalia vitendo sio matamshi.

Ali apologise kuwa hakumtendea haki? Au ni yale kiongozi hakosei?

Angeachaje kuzunguka na Sugu wakati dio Mwenyekiti wa Kanda? Hata yeye anajua isingeleta picha nzuri.

Alimteua Ruge kwa sababu ya weledi wake na sio favor. Ila inaelekea alitegemea pengine ingemyamazisha. Amesahau kuwa huyu ni mmoja wa wachache katika uongozi wa Bawacha waliokataa kuwaunga mkono wakina Halima. Ana msimamo na hanunuliki.

Haujui kuwa Sagrida alipigwa na mlinzi wa Heche? Au na wewe unaamini propaganda kuwa yalikuwa na maigizo? Alitolewa nje baada ya kung'ang'ania apewe nafasi ya kutosha kuzungumzia jinsi anavyoonewa. Kitu ambacho hawakuwa tayari kusikia maana aliishapatikana na hatia na kilichokuwa kinasubiriwa ni hukumu tu.

Ulitaka wasubiri mpaka lini ndio watoe dukuduku zao? Wakati dirisha ndio hilo linaelekea kufungwa.

Narudia tena, G55 hawajapinga Reforms. Hata hiyo ya "No elections" hawajaipinga. Wao wanatofautiana na njia inayofuatwa kufikia hapo. Wanachodai ni kusikilizwa na kutendewa haki. Katika waraka wao wamesema wazi wako tayari kukubaliana na maamuzi yeyote ya kikao ili mradi wasikilizwe.

Amandla...
Acha kutetea ujinga, wao si ndo walipitisha before TAL hajawa mwenyekiti, leo kwa njaa za madaraka wanataka kugombea ubunge kwa malengo ya kupandiwa dau,maana hawawezi kushinda kwa mfumo huu wa uchaguzi wa kuenguana
 
Back
Top Bottom