PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Reforms lazima zifanyike ndiyo raia tupige kura kama haiwezekani ni heri ccm ibaki madarakani kuliko watu wafe na kupoteza pesa bure,Hawo watia nia ni heri watafute vyama vinavyoshiriki wakagombee huko vyama ni vingi mbona.Uchaguzi wa ujanja ujanja kwenye sanduku la kura na uhuni ufike mwisho sasa ili mamlaka yarudi kwa wananchi.
Kama hamtaki watu wafe au waumie ina maana hamtaki waingie barabarani. Mkifanya hivyo uchaguzi utakuwa wa wazi kuliko mnavyotegemea kwa sababu mpinzani mkuu hatakuwepo. Kwa kufanya hivyo mtawapa ushindi wa bure CCM.

Amandla...
 
Unfortunately ni hicho hicho ambacho CDM inawafanyia wakina G55.

Njia sahihi ni hiyo inayopendekezwa na G55. Haya ya mikutano ya hadhara na petition UN haziinyimi usingizi CCM.

Unadhani njia ipi mbadala italeta mabadiliko? Tukumbuke kuwa uwezo wa kukataza mikutano ya hadhara bado wanao. Na kuhakikisha kuwa hatoki mtu kuandamana.

Mwenye uwezo wa kufanya hizo Reforms ni CCM na hawana nia hiyo.

Wanachosema G55 ni kuwa badala ya kuwa na mpambano wa kitaifa, mpambano uwe wa jimboni. Hao wanaohamasishwa kuwa No Reforms No Elections wahamasishwe kuhakikisha haki inatendeka katika majimbo yao bila uoga. Na wagombea watakuwa na haki ya kudai hayo ambayo watapoteza kama hawatagombea. Na watakaoshinda hata kama kwa binde wataendeleza mapambano ndani ya Bunge. Watu kama Ruge, Aida, Suzan wameonyesha kuwa ni wapiganaji wazuri kwenye masuala ya haki. Badala ya kuwa frustrate wangesikilizwa.

Amandla...

..G55 watawezaje kuzuia dhuluma wakati wameshindwa 2019, 2020, na 2024?
 
Kama hamtaki watu wake au waumie ina maana hamtaki waingie barabarani. Mkifanya hivyo uchaguzi utakuwa wa wazi kuliko mnavyotegemea kwa sababu mpinzani mkuu hatakuwepo. Kwa kufanya hivyo mtawapa ushindi wa bure CCM.

Amandla...

..kwa hiyo G55 wanataka watu waingie barabarani, au wana offer kitu gani kipya?
 
Kwa hiyo ndio unaona halali kwa mwenyekiti wako kupigwa nao kwa sababu hiyo!!
Hajui safari yao diamond na babu tale walipoitwa kule juu ghorofani na p Diddy halafu wewe na Mwenyekiti wangu mkawa wapi siku hiyo kwenye kupigwa nao?
None sense!
 
..G55 watawezaje kuzuia dhuluma wakati wameshindwa 2019, 2020, na 2024?
Hawatazuia dhulma yote lakini watajitahidi kuzuia sehemu nyingi wawezavyo. Hivi unaamini kupeleka petition UN na EU ndio kutazuia dhulma? Au CCM watatishika mkisema kuwa mtazuia uchaguzi bila kueleza mtauzuia vipi? Safari ya kutafuta haki ni ndefu na ngumu lakini iko siku itapatikana. Hata kama ni baada ya miaka 10 mingine.

Amandla...
 
..kwa hiyo G55 wanataka watu waingie barabarani, au wana offer kitu gani kipya?
Ninavyoelewa mimi ni wakina Lissu ndio wana zungumzia uusi na sio G55. Labda uusi huo ni pamoja na kuingia barabarani.
G55 wanataka mpambano uwe jimboni katika kila hatua ya uchaguzi, kuanzia kushinikiza fomu zitolewe na kupolewe hadi kutangazwa matokeo ya haki. CCM safari hii hawatarudia kosa la kushinda 100%. Na haitaweza kuwanyima kura CDM kiasi cha kukifanya kikose uwakilishi kabisa na kikose ruzuku. G55 wako realistic.

Amandla...
 
Hawatazuia dhulma yote lakini watajitahidi kuzuia sehemu nyingi wawezavyo. Hivi unaamini kupeleka petition UN na EU ndio kutazuia dhulma? Au CCM watatishika mkisema kuwa mtazuia uchaguzi bila kueleza mtauzuia vipi? Safari ya kutafuta haki ni ndefu na ngumu lakini iko siku itapatikana. Hata kama ni baada ya miaka 10 mingine.

Amandla...

..baada ya kilichotokea 2019, 2020, 2024, kwanini unaamini G55 watafanikiwa kuzuia uchaguzi usivurugwe?

..Na sababu za G55 kupinga Reforms na kutaka kwenda kukabiliana moja kwa moja na system wakati wa uchaguzi ni zipi?

..Mantiki ya uamuzi huo ni ipi? Tafadhali tushawishi ili tukuelewe.
 
Ninavyoelewa mimi ni wakina Lissu ndio wana zungumzia uusi na sio G55. Labda uusi huo ni pamoja na kuingia barabarani.
G55 wanataka mpambano uwe jimboni katika kila hatua ya uchaguzi, kuanzia kushinikiza fomu zitolewe na kupolewe hadi kutangazwa matokeo ya haki. CCM safari hii hawatarudia kosa la kushinda 100%. Na haitaweza kuwanyima kura CDM kiasi cha kukifanya kikose uwakilishi kabisa na kikose ruzuku. G55 wako realistic.

Amandla...

..G55 watafanyaje yote hayo bila uasi?

..Hivi tunataka uchaguzi wa HAKI, au kudura za CCM?

..Kwa makadirio yao, G55 wanategemea kupata asilimia ngapi, maana umesema CCM hawana nia ya kushinda 100%.

..Mimi nilitegemea G55 walau waunge mkono harakati za No Reform, na ikiwa tutafika wakati wa kuchukua form na hakuna kilichofanyika basi watoe maamuzi yao.
 
..baada ya kilichotokea 2019, 2020, 2024, kwanini unaamini G55 watafanikiwa kuzuia uchaguzi usivurugwe?
Inawezekana wasifanikiwe lakini wataendelea kupambana. Wewe unaamini kuwa wakina Lissu na watu wa diaspora wataweza kuzuia uchaguzi usivurugwe? Kwamba UN, EU watalazimisha haki itendeke?
..Na sababu za G55 kupinga Reforms na kutaka kwenda kukabiliana moja kwa moja na system wakati wa uchaguzi ni zipi?
Hapo unawaonea G55 hawapingi Reforms. Wanachosema njia sahihi ni kuendelea kudai Reforms wakati mnajipanga kushiriki . Tena wamesema mnajipanga kwa siri. Kukabiliana na system ni kama alivyofanya yule dada wa Dodoma katika uchaguzi uliopita wa serikali wa mitaa. Wakitokea watu wa kutosha kama yeye na wananchi wakiwaunga mkono, ufa utatokea maana itakuwa vigumu kuzima moto kila mahali.
..Mantiki ya uamuzi huo ni ipi? Tafadhali tushawishi ili tukuelewe.
Mbona nimeuzungumzia sana? Kama haunielewi ni sawa tu. Ndio demokrasia inavyopaswa kuwa. Sio hiyo ya visasi na kufukuzana.

Amandla...
 
..sababu za watawala kutokufanya Reforms zitakuwa ni zipi?

..hata nikifikiria kwa haraka haraka sioni sababu yoyote yenye mashiko ya kukataa reforms.

..Reforms ni chaguo bora, na lenye maslahi kwa wadau wote wa uchaguzi.
Nimekuuliza what if reforms hazijafanyika kususia uchaguzi kutaleta suluhu??
 
..G55 watafanyaje yote hayo bila uasi?

..Hivi tunataka uchaguzi wa HAKI, au kudura za CCM?

..Kwa makadirio yao, G55 wanategemea kupata asilimia ngapi, maana umesema CCM hawana nia ya kushinda 100%.

..Mimi nilitegemea G55 walau waunge mkono harakati za No Reform, na ikiwa tutafika wakati wa kuchukua form na hakuna kilichofanyika basi watoe maamuzi yao.
Wamesema wazi kuwa wanaunga mkono Reforms. Shida ni kuwa mmetanguliza suala la wao kupingana na Lissu.

Hilo la asilimia ngapi litajulikana hapo baadae. Nimesema kuwa CCM hawafanya kosa la kuhakikisha wanashinda 100% maana ndicho kilicho walazimisha kuwaingiza wakina Halima Bungeni. Kwa taratibu za Bunge kuna kamati ni lazima ziongozwe na ziwe na wajumbe wa upinzani. Wakishinda 100% kamati hizo zitakosa legitimacy.

Mimi nadhani badala ya kuwananga wakina G55 viongozi wa CDM waseme bayana watafanya nini kama hapatakuwa na Reforms. Na deadline ya uamuzi wa Reforms ni lini.

Amandla...
 
Huyu Mkurugenzi wao wa habari, asaidiwe, The Correct title ya TAL ni Mwenyekiti wa Taifa.wa Chadema na sio Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Niko shocked na taarifa hii
Pre GE2025 - Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Huu ni muendelezo wa udikiteta wa TAL ndani ya Chadema!.

Hii tengua tengua, itafuatiwa na kikao cha dharura cha CC yao kukaa kama a kangaroo court na kuwatimua timua hawa 55!.
Lissu atafukuza wangapi?, Chadema itabakiwa na nani na nini?!
P
Ametengua wangapi? Ccm mbona kila uchwao mnatengua.
 
Lisu Hafiki uchaguzi mkuu akiwa mwenyekiti huyo atakuwa keshapigwa chini uenyekiti

Chadema wanamlia timing tu

Mark my words
ikitokea hivyo, totally chadema itakufa mazima, hakuna wa kuiamini, itakuwa ni genge la wahuni watupu afadhali ya CUF. Hicho kikundi ndani ya chadema ni bora waondoke kama kuwafukuza ni ngumu ili chadema ibaki moja na yenye maamuzi ya kueleweka. Waondoke tu wakaanzishe chama chao kipya au wajiunge na ccm wakafanye siasa zao chafu huko.
 
Back
Top Bottom