Amewaasa wawavumilie halafu baada ya waraka kutoka anamtimua Ruge! Tunaangalia vitendo sio matamshi.
Ali apologise kuwa hakumtendea haki? Au ni yale kiongozi hakosei?
Angeachaje kuzunguka na Sugu wakati dio Mwenyekiti wa Kanda? Hata yeye anajua isingeleta picha nzuri.
Alimteua Ruge kwa sababu ya weledi wake na sio favor. Ila inaelekea alitegemea pengine ingemyamazisha. Amesahau kuwa huyu ni mmoja wa wachache katika uongozi wa Bawacha waliokataa kuwaunga mkono wakina Halima. Ana msimamo na hanunuliki.
Haujui kuwa Sagrida alipigwa na mlinzi wa Heche? Au na wewe unaamini propaganda kuwa yalikuwa na maigizo? Alitolewa nje baada ya kung'ang'ania apewe nafasi ya kutosha kuzungumzia jinsi anavyoonewa. Kitu ambacho hawakuwa tayari kusikia maana aliishapatikana na hatia na kilichokuwa kinasubiriwa ni hukumu tu.
Ulitaka wasubiri mpaka lini ndio watoe dukuduku zao? Wakati dirisha ndio hilo linaelekea kufungwa.
Narudia tena, G55 hawajapinga Reforms. Hata hiyo ya "No elections" hawajaipinga. Wao wanatofautiana na njia inayofuatwa kufikia hapo. Wanachodai ni kusikilizwa na kutendewa haki. Katika waraka wao wamesema wazi wako tayari kukubaliana na maamuzi yeyote ya kikao ili mradi wasikilizwe.
Amandla...
..G55 walipaswa kutoa nafasi kwa " No Reforms No Elections " kutekelezwa, lakini wao wanaipinga wakati kampeni hiyo imefanyika ktk kanda moja tu ya chama.
..Suala la Sigrida siwezi kusema amepigwa, au hajapigwa. Nasubiri lifike mahakamani ndipo nitakapoweza kutoa mtizamo wangu.