PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Watapata wapi ubavu wa kuwanyoshea kidole CCM? Ruge na wenzake walikuwa wanawapima, na wameingia mkenge. Mwanzo tu walitaka kumfukuza Mrema wakastuka. Majuzi kapigwa binti wa Bawacha. Leo hilo. Msimamo wa it's my way or the highway. Halina afya kwa chama.

Amandla...

Part of process wala usihangaike kijana, waganga njaa watakubali with time, consistency matters
 
Watapata wapi ubavu wa kuwanyoshea kidole CCM? Ruge na wenzake walikuwa wanawapima, na wameingia mkenge. Mwanzo tu walitaka kumfukuza Mrema wakastuka. Majuzi kapigwa binti wa Bawacha. Leo hilo. Msimamo wa it's my way or the highway. Halina afya kwa chama.

Amandla...
Mbowe alishindwa Kwa kura halali japo namuunga mkono kwa kuasisi No reform no Election . Kazi ya TUNDU nikusimamia maamuzi halali ya chama yaliyoungwa mkono na hao wapenda pombe na nyama za bure a.k.a G55.
 
Kwani chaguzi za 2005,2010,2015 zilikua za sheria zipi kutofautisha na 2020?

Hizo reforms zitakuja kwa kususia chaguzi? Maana wa kuzuia chaguzi zisifanyike simuoni!!


..mashinikizo yanatokana na ukweli kwamba CCM na SERIKALI wanaonekana kupuuza kilio na malalamiko ya wenzao.

..kwa mwenendo huu wa CCM na serikali labda tungeshauri Chadema watumie njia gani ili wasikilizwe tukiacha haya mashinikizo wanayoyaweka.

..hata hao wanaotaka kugombea wanadai wanao uwezo wa kuzuia dhuluma katika uchaguzi. Je, kwa kilichotokea 2019,2020,2024, upo uwezekano wa kuzuia dhuluma za uchaguzi kwa njia za amani?

..mimi nadhani busara ni Reforms kufanyika sasa hivi, ili tusifike kwenye " No elections ", au tusifike huko wanakotaka G55.

..G55 basically wanadai kwamba wanayo mabavu ya kupambana wakati wa uchaguzi kuzuia dhuluma.
 
Lissu nae ni dikteta? Tena uchwara?

Hivi ni kususia uchaguzi au kuzuia uchaguzi? Kiingereza kigumu sana. No reforms no election.
 
Lisu Hafiki uchaguzi mkuu akiwa mwenyekiti huyo atakuwa keshapigwa chini uenyekiti

Chadema wanamlia timing tu

Mark my words
Kumbe kuna mfukuto wa volcano,sikujua ndani ya Chadema kuna.makundi ya kupanga mapinduzi.
Hawa watu sio eti ni wakeleketwa wa kushiriki uchaguzi tu.Wana agenda kubwa,hadi wakaandikia uongozi petition, siyo bure.

Naiyona Chadema imegeuka Yanga Raizoni vis Yanga Kandambili enzi hizo za viatu vya Raizoni.

Pili nadhani Mh Mbowe ndio mwenye password ya Chadema,yaoenekana Lissu hajapewa password.
Kwani huko nyuma **** akina Wangwe, Profesa Kitila Mkumbo,Zitto,n.k walitaka mapinduzi,wengine wakafukuziwa mbali.Na Chama kimesafiri kwa muda mrefu bila hawa soft criminals.
Sio bure kuna mkono wa Tanzanite.
 
Siyajui ya Hilda lakini huyu Catherine Ruge alikuwa Katibu Mkuu wa Bawacha, anafahamu malengo ya No Reform No Election, na anajua kwamba hili lilipitishwa na Chama yeye akiwa kiongozi wa kitaifa na alishiriki kulipitisha, sasa leo anapolipinga ana maana gani?

Lingine ni hili, unataka kushiriki uchaguzi kwa sheria hizi ili iweje, unataka watekwe watu wangapi au unataka wauawe watu wangapi?

Japo sikutaka atenguliwe, nilitaka aonywe na kuelimishwa
Jee alipewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa na kuadhibiwa? Jee kamati ya nidhamu ya chama ilikaa kusikiliza kosa alilotuhumiwa nalo? Mamlaka yake ya nidhamu ni ipi? Hiyo tumbua tumbua ya Tundu Lissu ina tofauti gani na ile ya JPM mliyoiita udikteta?


View: https://youtu.be/SjKH0C4_BMU?si=_FJ4qsl7W891qOZS
 
Naam bado hamjasema... Zidumu fikra za lisu..mwenye kupinga .. anashughulikiwa.. narudia tena lissu anakwenda kuivuruga chadema
 
Tundu Lissu, Mwenyekiti wa chama Taifa CHADEMA leo 5.4.2025 ametengua uteuzi wa mjumbe wa sekretarieti na mtalamu wa dawati la jinsia Catherine Ruge.

Catherine Ruge ni mmoja ya Kikundi cha ndani ya CHADEMA cha G55 chenye Malengo ya kukwamisha Kampeni ya no reforms no Election. Pia wanadaiwa kuhujumu au kuangusha Uongozi uliopo madaraka chini ya Tundu Lissu.

Kundi hilo linadaiwa kudhaminiwa na Freeman Mbowe aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa madhumuni ya kuonesha Umma kwamba Tunddu Lissu na Uongozi wake haukubaliki. Wengine walio kwenye hilo kundi la G55 ni John Mrema naa Mwita

Operesheni #NoReforms NoElection

inaendelea kuchanja mbuga kanda ya kusini.
John Mrema nayedaiwa kuwa Mwasisi wa kutaka kupindua Uongozi wa Tundu Lissu wa Kikundi cha G55. John Alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje kwenye Uongozi wa Freeman Mbowe
View attachment 3294204
Mapema wiki hii Watia nia ya Ubunge mwaka 2025 na waliokuwa watia nia mwaka 2020, (G55) wakiongozwa na Vigogo Adv. John Mallya, Catherine Ruge, John Mrema na Julius Mwita wamechapisha waraka kwenda kwa Katibu Mkuu Chadema, wakieleza kuwa wadau wengi wa Demokrasia nchini hawaungi mkono Mpango wa kuzuia uchaguzi mkuu unaotaka kufanywa na Chama cha Chadema kwani hali hiyo inatafsiriwa na wadau hao kuwa ni sawa na karibu na matendo ya uasi.
Waraka huo ulioandikwa na G55 na kuwakilisha watia nia wengine zaidi ya 200 pamoja na Maafisa wa juu wa Chadema na kushuhudiwa na JamboTv, umesema kuwa Wadau wengi wanaunga mkono harakati za kupigania mabadiliko ya sheria na mfumo wa uchaguzi, wakisita kujiingiza kwenye kuunga mkono mpango wa kutaka kuzuia uchaguzi kwani pia linaenda kinyume na Katiba na sheria za nchi.
Kwa Upande wake Hilda Newton ameishukuru Mungu kwa kuwaepusha CHADEMA na Catherine kwani Alikuwa anagombea UKatibu Mkuu wa BAWACHA akashindwa.

Chini kabisa nitaambatanisha Meseji za WhatsApp za G55 Wanaodaiwa kutaka kupindua uongozi uliopo.
Catherine Ruge akiwa amevaa Mawigi. CPA Catherine Ruge alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA #BAWACHA kipindi cha Uongozi wa Freeman Mbowe. Huyu Ruge na Freeman Mbowe ndo Walimpa Rais Samia Tuzo ya Malidhiano huko Arusha.

Na Hilda Newton Chadema

Mungu fundi sana

Imagine leo story ingekuwa isomeka Katibu Mkuu wa Bawacha Taifa apinga Azimio la Chadema la #NoReformsNoElection.

Mungu awabariki sana Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Bawacha Taifa ni Kama tulikuwa mbele ya muda.😂

Ukipitia orodha ya watu waliosaini petition ya kupinga #NoReformsNoElection wote ni watu ambao kwenye Uchaguzi wetu wa ndani walikuwa wanamuunga mkono Mhe. Mbowe.

Wengine ni Wajumbe wenzangu wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama Taifa wakati tunapitisha hili Azimio la #NoReformsNoElection chini ya Mwenyekiti Mbowe na wao walipiga kura ya Ndiyooo tena kwa sauti kubwa sana.

Sasa hivi baada ya Mhe. Lissu kuwa Mwenyekiti wale wale waliopitisha Azimio hili kwenye Vikao halali sasa wametoka dharani kulipinga.

Nakumbuka siku tunapitisha Azimio hili cha Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Januari 2025 kwenye Kikao Mhe. Mbowe aliuliza kuna mtu yeyote mwenye maoni au swali lolote kwenye Azimio hili wote tulinyamaza Kimya kuonyesha kwamba tunaunga mkono.

Najiuliza, haya maswali ambayo wanauliza leo kwanini hawakumuuliza Mwenyekiti Mbowe wakati anaendesha kikao kilichopitisha Azimio hili?

Au walipitisha hili Azimio kwasababu walijua Mhe. Mbowe angeshinda asingetekeleza.?

Mwisho, Kama wao kiu yao ni kushiriki Uchaguzi kwanini wasiende kujiunga na akina NCCR ambao mawazo yao na wao yanafanana ili wapewe nafasi ya kugombea huo ubunge watimize hiyo kiu yao ya kuwagombea bila Reforms?
View attachment 3294232View attachment 3294231 View attachment 3294230
Reforms lazima zifanyike ndiyo raia tupige kura kama haiwezekani ni heri ccm ibaki madarakani kuliko watu wafe na kupoteza pesa bure,Hawo watia nia ni heri watafute vyama vinavyoshiriki wakagombee huko vyama ni vingi mbona.Uchaguzi wa ujanja ujanja kwenye sanduku la kura na uhuni ufike mwisho sasa ili mamlaka yarudi kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom