PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Part of process wala usihangaike kijana, waganga njaa watakubali with time, consistency matters
 
Mbowe alishindwa Kwa kura halali japo namuunga mkono kwa kuasisi No reform no Election . Kazi ya TUNDU nikusimamia maamuzi halali ya chama yaliyoungwa mkono na hao wapenda pombe na nyama za bure a.k.a G55.
 
Kwani chaguzi za 2005,2010,2015 zilikua za sheria zipi kutofautisha na 2020?

Hizo reforms zitakuja kwa kususia chaguzi? Maana wa kuzuia chaguzi zisifanyike simuoni!!


..mashinikizo yanatokana na ukweli kwamba CCM na SERIKALI wanaonekana kupuuza kilio na malalamiko ya wenzao.

..kwa mwenendo huu wa CCM na serikali labda tungeshauri Chadema watumie njia gani ili wasikilizwe tukiacha haya mashinikizo wanayoyaweka.

..hata hao wanaotaka kugombea wanadai wanao uwezo wa kuzuia dhuluma katika uchaguzi. Je, kwa kilichotokea 2019,2020,2024, upo uwezekano wa kuzuia dhuluma za uchaguzi kwa njia za amani?

..mimi nadhani busara ni Reforms kufanyika sasa hivi, ili tusifike kwenye " No elections ", au tusifike huko wanakotaka G55.

..G55 basically wanadai kwamba wanayo mabavu ya kupambana wakati wa uchaguzi kuzuia dhuluma.
 
Lissu nae ni dikteta? Tena uchwara?

Hivi ni kususia uchaguzi au kuzuia uchaguzi? Kiingereza kigumu sana. No reforms no election.
 
Lisu Hafiki uchaguzi mkuu akiwa mwenyekiti huyo atakuwa keshapigwa chini uenyekiti

Chadema wanamlia timing tu

Mark my words
Kumbe kuna mfukuto wa volcano,sikujua ndani ya Chadema kuna.makundi ya kupanga mapinduzi.
Hawa watu sio eti ni wakeleketwa wa kushiriki uchaguzi tu.Wana agenda kubwa,hadi wakaandikia uongozi petition, siyo bure.

Naiyona Chadema imegeuka Yanga Raizoni vis Yanga Kandambili enzi hizo za viatu vya Raizoni.

Pili nadhani Mh Mbowe ndio mwenye password ya Chadema,yaoenekana Lissu hajapewa password.
Kwani huko nyuma **** akina Wangwe, Profesa Kitila Mkumbo,Zitto,n.k walitaka mapinduzi,wengine wakafukuziwa mbali.Na Chama kimesafiri kwa muda mrefu bila hawa soft criminals.
Sio bure kuna mkono wa Tanzanite.
 
Jee alipewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa na kuadhibiwa? Jee kamati ya nidhamu ya chama ilikaa kusikiliza kosa alilotuhumiwa nalo? Mamlaka yake ya nidhamu ni ipi? Hiyo tumbua tumbua ya Tundu Lissu ina tofauti gani na ile ya JPM mliyoiita udikteta?


View: https://youtu.be/SjKH0C4_BMU?si=_FJ4qsl7W891qOZS
 
Naam bado hamjasema... Zidumu fikra za lisu..mwenye kupinga .. anashughulikiwa.. narudia tena lissu anakwenda kuivuruga chadema
 
Reforms lazima zifanyike ndiyo raia tupige kura kama haiwezekani ni heri ccm ibaki madarakani kuliko watu wafe na kupoteza pesa bure,Hawo watia nia ni heri watafute vyama vinavyoshiriki wakagombee huko vyama ni vingi mbona.Uchaguzi wa ujanja ujanja kwenye sanduku la kura na uhuni ufike mwisho sasa ili mamlaka yarudi kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…