PreGE2025 Tundu Lissu atengua uteuzi wa CPA Catherine Ruge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwanzoni sikukubaliana na Lissu kugombea uenyekiti ila now naaanza kuelewa kwanini alifanya vile. Nadhani Mbowe kuna kiini macho alikuwa anatufanyia. Bora mnyukano huu umetokea angalau sasa tunajua panapovuja ni wapi
Wala usiumize kichwa siku nyingine elewa hili mbogamboga wametengeneza mfumo wa matawi ambayo viongozi wake wote ni vibaraka. Usipokuwa kibaraka watakujazia pandikizi mpaka uonekane hutakiwi,TAL hanunuliki kwenye gulio hivyo ni tatizo
 
Tundu lisu anatangaza uasi anafaa kushikwa nakuhojiwa atajaleta vita huyu nayeye akimbilie marekani waliko wanawe ama Belgium kwawapendwa wake
 
Hivi umesoma lugha wanazotumia kwenye kutoa msimamo wao? Mtu unamuita kiongozi wako "hawa wajinga" tena aliyekupa uteuzi kama na wao ni wanademokrasia kweli sio mapandikizi walitakiwa wajiuzulu kuonyesha kwamba walishauri viongozi wao na kuona viongozi wao hawashauriki
 
Wapi katika waraka wao wamemuita mtu mjinga? Unapata wapi ubavu wa kujilinganisha na Ruge katika masuala ya kupigania demokrasia?
Kwa hili mmechemsha.

Amandla...
 
Mna tafauti gani na CCM, Kagame, Museveni and dictators wengine! Lifikirie hilo! Ni kuwa hamna uwezo wa kumpoteza, kwa mwendo huu mgelikuwa na uwezo mngelimpoteza....
 
Dikteta Lissu aendeleza udikteta wake. Mpaka mkome!!
 
Wapi katika waraka wao wamemuita mtu mjinga? Unapata wapi ubavu wa kujilinganisha na Ruge katika masuala ya kupigania demokrasia?
Kwa hili mmechemsha.

Amandla...
Kumbe naongea na chawa. nakuambia angalia hizo screenshot wewe unaniletea habari za waraka
Nimekueleza habari za kama wao wanatofautiana mtazamo na viongozi wao na hili hali wanazitumikia nafasi zao walizoteuliwa ni vyema wangejiuzulu wewe unaniletea habari ya mimi kushindana na ruge
Mambo mepesi kama haya yanakushinda kung'amua je hiyo No reform no election kwa uelewa wako si ni rocket science
 
Kwanini mnakandamiza uhuru wa watu kujieleza ndani ya chama? Je mkipata nchi tutakua huru au ndo mtatuteka na kutuua kama majizi ya Ccm?
 
Vipi reforms zisipofanyika na watawala?
 
Wewe unaangalia personal communications kama ushahidi wa hujuma zao? Lissu, Heche, Lema na Msigwa walimfanyia hujuma za chini chini kiongozi wao na hata siku moja hamkulalamiki. Hamna cha ajabu kwa wanachama kutumia lugha kama hizo kwa viongozi wao katika mazungumzo yao binafsi. Tunachoangalia ni kilichopo hadharani. Kiongozi anaetaka apendwe na akubalike na wanachama wote ana chembe chembe za udikteta. Alichokifanya hakina tofauti na kile ambacho JPM alimfanyia Nape. Na wote tunakumbuka jina ambalo Lissu alimbatiza.

Amandla...
 
Vipi reforms zisipofanyika na watawala?

..sababu za watawala kutokufanya Reforms zitakuwa ni zipi?

..hata nikifikiria kwa haraka haraka sioni sababu yoyote yenye mashiko ya kukataa reforms.

..Reforms ni chaguo bora, na lenye maslahi kwa wadau wote wa uchaguzi.
 
..mashinikizo yanatokana na ukweli kwamba CCM na SERIKALI wanaonekana kupuuza kilio na malalamiko ya wenzao.
Unfortunately ni hicho hicho ambacho CDM inawafanyia wakina G55.
..kwa mwenendo huu wa CCM na serikali labda tungeshauri Chadema watumie njia gani ili wasikilizwe tukiacha haya mashinikizo wanayoyaweka.
Njia sahihi ni hiyo inayopendekezwa na G55. Haya ya mikutano ya hadhara na petition UN haziinyimi usingizi CCM.
..hata hao wanaotaka kugombea wanadai wanao uwezo wa kuzuia dhuluma katika uchaguzi. Je, kwa kilichotokea 2019,2020,2024, upo uwezekano wa kuzuia dhuluma za uchaguzi kwa njia za amani?
Unadhani njia ipi mbadala italeta mabadiliko? Tukumbuke kuwa uwezo wa kukataza mikutano ya hadhara bado wanao. Na kuhakikisha kuwa hatoki mtu kuandamana.
..mimi nadhani busara ni Reforms kufanyika sasa hivi, ili tusifike kwenye " No elections ", au tusifike huko wanakotaka G55.
Mwenye uwezo wa kufanya hizo Reforms ni CCM na hawana nia hiyo.
..G55 basically wanadai kwamba wanayo mabavu ya kupambana wakati wa uchaguzi kuzuia dhuluma.
Wanachosema G55 ni kuwa badala ya kuwa na mpambano wa kitaifa, mpambano uwe wa jimboni. Hao wanaohamasishwa kuwa No Reforms No Elections wahamasishwe kuhakikisha haki inatendeka katika majimbo yao bila uoga. Na wagombea watakuwa na haki ya kudai hayo ambayo watapoteza kama hawatagombea. Na watakaoshinda hata kama kwa binde wataendeleza mapambano ndani ya Bunge. Watu kama Ruge, Aida, Suzan wameonyesha kuwa ni wapiganaji wazuri kwenye masuala ya haki. Badala ya kuwa frustrate wangesikilizwa.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…