Katika Kampeni Kuna propaganda siku zote!
Kuna kutengeneza taswira za uongo kuonesha kuwa fulani anakubalika nk!
Mojawapo ya mbinu inayotumika Sana hapa kwetu Ni kutengeneza picha au video za kudanganya macho au chombo Cha habari kupiga picha inayopotosha!
Mbinu hii hivi Sasa inatumiwa na Vyama vyote,hususani CCM na CHADEMA!
Lakini hili la Tundu Lissu kupokelewa na kushangiliwa na maelfu ya watu kila Kona linafikirisha Sana kuelekea Oktoba 28.
Kama wanaomsikiliza huko viwanjsni na kumkubali Ni asilimia 70 basi iko kazi Mwaka huu!
Aidha Kuna kundi kubwa la watu wasioenda kwenye mikutano,kundi hili si la kudharau na hapo ndipo Siri ilipo!
Mtaani kwangu Kuna nyumba Kama kumi hivi ambazo ktk uchunguzi nilifanya hawaendi kwenye mikutano ,Ila Kati yao 70% watampigia kura Tundu Lissu,Hawa nakutana nao vijiweni ,kanisani na jumuia !
Kati yao karibu 50% Ni wastaafu!
Kwa ujumla Uchaguzi huu Ni mgumu kinyume kabisa na ilivyotarsjiwa!
Mimi naishi mji ambao inasemekana Ni ngome Imara yaCCM!
Ni lazima tuukabili ukweli kuwa Tundu Lissu kabidili upepo wa Siasa Mwaka huu ktk Hali ambayo haikutegemewa!
Bila Shaka kwa wapunzani wake Hali hii inawapa wakati mgumu mno!
Ndio maana wenye Dini zao wanasema hii Ni NGUVU YA MUNGU!