Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Hiyo ndiyo kazi ya 'chaguo la mungu' au 'tumaini lililorejea!' Ukweli hayo ndiyo matatizo ya kutoa kazi za kitaaluma kwa mtindo wa kuteua kama inavyokuwa katika vyeo vya kisiasa. Kazi za kitaaluma kama hizo ilipaswa watu waombe kwa kuzingatia vigezo na sifa maalumu zinazohitajika. Nahakika ingekuwa zinaombwa, majaji waliotajwa na Lissu wasingeoomba na wasingekuwa majaji leo. Hata hivyo kasoro hii inaonesha ukilaza kwa wanaohusika na teuzi mbali mbali. Ilitegemewa wajue katiba ambayo ndiyo sheria mama. Tatizo la viongozi wa Tanzania kila kitu wanajibu kisiasa. watu wakiuawa na polisi wao majibu yao ni siasa! Sasa Lissu katoa ushahidi nao wajibu au wakanushe kwa ushahidi. Nchi hii tungekuwa na akina Lissu 10, Zitto 10, Silaa 10, Wenje 10 na Mdee 10 ingenyooka! Usishangae baada ya ushahidi huu akaibuka yule vuvuzela wao ambae hudandia kila jambo bila kujua kama alivyodandia 'magamba' ambayo yamemtokea puani sasa hivi yuko kimya! kasahau kabisa ile mikwara ya barua, siku 90 na 120
 
Angalieni, isije ikawa kama ile issue ya kwamba Zitto na kamati yake waliposhutumiwa kwamba walikula rushwa. Alipoulizwa Lissu akasema ushahidi wake ni wa kusikia tu kutoka kwa huyu yule. Na hoja ikafa kifo cha kawaida! Ametaja majina na taaluma lakini ushahidi kuwa hawana qualifications nyingine anao? Au hata hizo sifa alizozitaja anauhakika nazo? Ushabiki tu huwa hausaidii saana katika mabo ya kitaifa. Nia ni nzuri ila inahitaji umakini keundea mambo!
 
wahusika hawana sifa kweli kwa kuwa madai yake yanahusu public record kwahiyo wahusika kama wangekuwa na sifa basi wangejitokeza kupinga kwa hoja au hata waliofanya nao kazi wangewatetea lakini unapoona Bw.Tundu anatoa hoja na legal community inakaa kimya bila majibu basi ujue kuna kitu ambacho hakijibiki. kwa mfano unaposema fulani hana degree au Bi. Bibie aliyeteuliwa huku akiwa na record ya udanganyifu ambayo ni kosa la jinai kumbukumbu zipo kwanini wahusika wasikanushe jiulize ??
 
By the way, hata Mh. Mulugo, Naibu waziri wa Elimu aliajiriwa ualimu kwa cheti cha Diploma ya Ualimu cha Dr. Dick Mulungu. Dr. Mulungu kwa sasa ni mwalimu wa chuo kikuu Mkwawa. Na kazi hiyo ya ualimu ndio imekuwa mwanzo wa safari yake kwenda Unaibu waziri.

Hii hata Usalama wa Taifa wanajua. Na JK anajua bila shaka.
hapa sijakuelewa mtu wa shamba una maana gani kwani Mulungu si anayo degree kutoka open university kwahiyo anao uwezo wa kufundisha au unazungumzia kabla hajapata degree? je wana share the same first name ? au alibadili baadaye?
please naomba ufafanuzi wako maana huyu jamaa anaonekana kilaza sana
 
wahusika hawana sifa kweli kwa kuwa madai yake yanahusu public record kwahiyo wahusika kama wangekuwa na sifa basi wangejitokeza kupinga kwa hoja au hata waliofanya nao kazi wangewatetea lakini unapoona Bw.Tundu anatoa hoja na legal community inakaa kimya bila majibu basi ujue kuna kitu ambacho hakijibiki. kwa mfano unaposema fulani hana degree au Bi. Bibie aliyeteuliwa huku akiwa na record ya udanganyifu ambayo ni kosa la jinai kumbukumbu zipo kwanini wahusika wasikanushe jiulize ??

That's fair enough, I am a bit sceptical kwa vile hawa wana siasa some times kwa ku twist facts! Ila hii haijakaa vizuri kwa serikali. Unawezaje kupromote incompetence wakati wenye sifa wapo?
 
Mtu wa shamba, inamaana tundu lisu pekee ndiye mwanasheria asiye muoga?au asiye mchumia tumbo?sasa iliwezekanaje kumpendekeza dada yake awe mbunge wa viti maalum kama kweli ye ni muadilifu?
 
Mtu wa shamba, inamaana tundu lisu pekee ndiye mwanasheria asiye muoga?au asiye mchumia tumbo?sasa iliwezekanaje kumpendekeza dada yake awe mbunge wa viti maalum kama kweli ye ni muadilifu?

Kuna nyingin nimeipata leo hii hapa:

- '' Ndesamburo na mtoto wake na mkwe wake, Lissu na Dada yake Christina, Zitto na Mchumba wake, Mtei na Mkwe wake, Slaa na mke wake!! HEBU ONDOA BORITI KWENYE JICHO LAKO KWANZA NDIO UNAWEZA KUTUFUNDISHA CCM!! quoted W.J. Malecela

Inawezekana ikawa ni siasa za mgongano wa kimaslahi hizi! Wanatuzuga wote hawa CCM na CDM mlengo wao ni mmoja. Inawezekanaje chama kinahodhiwa na familia?
 
Hivi jamani tz hakuna manasheria wengine wazalendo wakaungana na kamanda Lissu ili kurekebisha haya madudu anayofanya rais wetu na wasaidizi wake?
 
Mtu wa shamba, inamaana tundu lisu pekee ndiye mwanasheria asiye muoga?au asiye mchumia tumbo?sasa iliwezekanaje kumpendekeza dada yake awe mbunge wa viti maalum kama kweli ye ni muadilifu?

kuna tofauti kati ya nafasi za kuchaguliwa na kuteuliwa.
ingawaje kuna utata kufuatia ukaribu wahusika na wabunge waliochaguliwa lakini wakulaumiwa zaidi ni wale waliowapigia kura huko mikoa walikotoka kama dada yake alishinda kwenye mkutano wa bawata huko singida kihalali hakuna mbaya.
 
Hivi jamani tz hakuna manasheria wengine wazalendo wakaungana na kamanda Lissu ili kurekebisha haya madudu anayofanya rais wetu na wasaidizi wake?

Mijoga, wachumia tumbooo!!!!
 
Tuache kando dhamira ya Tundu Lissu, ambayo watu wanauhuru wa kuitafsiri wanavyoona kama vile, anapiga debe kwa wivu ajili yeye hajateuliwa, ama ana kiherehere cha kutaka aonekane yeye anajua zaidi taaluma ya shieria, ama jamaa ana ubishi wa asili yake, ama ana uchungu wa dhat na wananchi wa Tanzania.

Lakini, tuone umuhimu na uzito wa hoja yake. Ni nin maslahi na nia ya kiongozi mkuu wa nchi, kufanya uteuzi wa nafasi kwa watu wasio na sifa wakati tasnia ina wataalam wenye sifa kibao?

Raisi anapoingia madarakani kwa kura za kuchakachua, na hatimaye ameendeleza wimbi la kuvunja sheria na kukiuka katiba ya nchi, huyu anapata wapi kiburi na dharau kubwa ya kiwango hiki?

Ni kwamba raisi huyu ni mbumbumbu kiasi kwamba haelewi kiwango cha madhara anayolisababishia taifa kwa uteuzi wake wa mawaziri na viongozi usiozingatia sifa na uwezo, na badala yake anazingatia mambo ya ovyo ovyo tu na unasaba na uswahiba?

Ni nini haki ya Watanzania kumdhibiti kiongozi kama huyu? Haki hizo ili wazipate wanahitaji kufuata taratibu zipi? Naona jamaa alishajua ni kelele za chura ndiyo maana ana kiburi na uziwi huku akiendelea kuibomoa nchi pasipo hofu wala aibu.

Najua tumechelewa lakini we can still do something rather than letting this guy to peacefully complete his evil mission. Tuelewe kwamba, usipoziba ufa utajenga ukuta na ukicheka na nyani lazima uvune mabua. Huyu jamaa na hawa washikaji wake, anatumaliza ndugu zangu.

Nawasilisha.

Atakumbukwa km rais aliyetumia madaraka isivyo,mfano kuteua na kuwapa uwaziri wabunge bila kuapishwa alafu kujitahidi kufinyanga katiba ili kutudanganya watanzania kuwa hakukua na makosa ta uteuzi. Ni bora tusiwe na katiba tujue moja
 
"Ni afadhali Dr Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge"-Nimenukuu. Wanaokuja na hoja za kumtetea Rais watuambie ni Chuo gani alisoma Mbaruku Salum Mbaruku...Duh!!! Mwalemi sidhzo!
 
Kuna msemo wa kichina unasema SAMAKI HUANZA ANAPOANZA KUOZA KICHWA NDIO KINAANZA KUOZA KWANZA, tatizo la kukosa umakini halipo tu kwenye kuteua majaji, hivyo ndivyo utendaji wa kazi wa mkuu wetu ulivyo. Kwa ufupi, kiongozi mfanisi anayefanya kazi yake kwa umakini katika serikali ya sasa hivi anaonekana kama wa tofauti kwa sababu sio utaratibu wao. Kwa nini suala nyeti kama hili likose majibu au watu kuwajibishwa? Ndio maana wala rushwa hawafanywi lolote na watu wanaendelea kufanya madudu kwa sababu hakuna kitu kitafanyika, nadhani imefika mahala tufanye kitu cha tofauti kubadili huu muundo wa utendaji usiozingati uwajibikaji.

Ahsanteni
 
Udini hapa unachangia. Chunguza hayo majina wote ni walewaleeeeeeeeee

Udini utawapeleka pabaya watz Lisu kasema sifa na sio jina nyie kwa mpango wa Udini na ukanda utawapeleka pabaya sana upumbavu na ujinga ni kipaji ndio maana kila siku wanatokea wapya🙂 by nyerere
 
Mtu wa shamba, inamaana tundu lisu pekee ndiye mwanasheria asiye muoga?au asiye mchumia tumbo?sasa iliwezekanaje kumpendekeza dada yake awe mbunge wa viti maalum kama kweli ye ni muadilifu?

Issue ni kujadili ukweli wa aliyoyasema.

Katiba imetoa sifa za majaji.

Tundu Lissu ametaja majaji wasio na sifa hizo.

Kama amesema uongo, njoo kanusha, au wenyewe waje wakanushe, au ofisi ya rais ije ikanushe na ushahidi.
 
WildCard, kama kuna kiini macho basi ni haya madudu yaliyomo ndani ya katiba yetu hii. Kwa mfano ibara ya 112 (1) ndio inayounda Tume ya utumishi wa mahakama, ambayo imepewa jina la tume ya ushauri wa uteuzi wa majaji na ajira ya mahakimu wa mahakama Tanzania bara.

Ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo inatamka kuwa:
Wajumbe wa tume hiyo watakuwa;
a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa mwenyekiti Mteule wa Raisi angalia Ibara ya 118(2) ya katiba
b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule wa Rais angalia ibara ya 59(1) ya katiba
c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa
atakayeteuliwa kwa ajili hiyo na Rais Mteule wa Rais angalia ibara ya 118(3) ya katiba na bado anateuliwa
baada ya kushauriana na Jaji Mkuu na Rais kuwa mjumbe wa Tume angalia ibara 112 (2) (c)
d) Jaji Kiongozi Mteule wa Rais angalia ibara ya 109(1) ya katiba
e) Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais Wateule wa Rais angalia Ibara 112(2) (e)

Kwa vile hawa wote wameteliwa na Raisi kutokama na nyadhifa zao lazima kwa hali yoyote hiyo hawatampinga. Mtu yoyote mwenye akili akiona hii lazima atasema uteuzi wa majaji pamoja na kuwa anatokana na mapendekezo ya tume ya mahakama, kiukweli mapendekezo hayo ni ya Rais kwani tume yote ni ya Rais.

Tuache kuwa wabishi bila sababu, tuionee huruma nchi yetu, muundo huu haufai hata kidogo katika kuendeleza utawala wa sheria.

Tatambishia sana Tundu lakini kwa muundo huu wa tume ni vigumu sana kusema vinginevyo.

Kama waungwana tukubali maneno ya Tundu lissu na kutafuta njia mbadala ya kupata majaji kwa uwazi zaidi sio huu utaratibu wa sasa uliogubikwa na umangimeza.

Mkuu wangu nimejiuliza mpaka sasa sipati jibu ilikuaje mtu kama Latifa Mansoor akachaguliwa kuwa jaji?! Ama na hizi nafasi watu wanatoa rushwa kuzipata kama ilivyo Idara nyeti za Serikali? Huyu alifanyiwa vetting na chombo gani? Ingekua nchi nyingine tayari wahusika wametimuliwa na hatua za kisheria kuchukuliwa.
 
Back
Top Bottom