Hebel Mlagala
Senior Member
- Aug 4, 2012
- 134
- 49
Hiyo ndiyo kazi ya 'chaguo la mungu' au 'tumaini lililorejea!' Ukweli hayo ndiyo matatizo ya kutoa kazi za kitaaluma kwa mtindo wa kuteua kama inavyokuwa katika vyeo vya kisiasa. Kazi za kitaaluma kama hizo ilipaswa watu waombe kwa kuzingatia vigezo na sifa maalumu zinazohitajika. Nahakika ingekuwa zinaombwa, majaji waliotajwa na Lissu wasingeoomba na wasingekuwa majaji leo. Hata hivyo kasoro hii inaonesha ukilaza kwa wanaohusika na teuzi mbali mbali. Ilitegemewa wajue katiba ambayo ndiyo sheria mama. Tatizo la viongozi wa Tanzania kila kitu wanajibu kisiasa. watu wakiuawa na polisi wao majibu yao ni siasa! Sasa Lissu katoa ushahidi nao wajibu au wakanushe kwa ushahidi. Nchi hii tungekuwa na akina Lissu 10, Zitto 10, Silaa 10, Wenje 10 na Mdee 10 ingenyooka! Usishangae baada ya ushahidi huu akaibuka yule vuvuzela wao ambae hudandia kila jambo bila kujua kama alivyodandia 'magamba' ambayo yamemtokea puani sasa hivi yuko kimya! kasahau kabisa ile mikwara ya barua, siku 90 na 120