Hapana kwa kweli, Lissu alisema tutashtakiwa kutokana na kuvunja sheria na tutadaiwa fidia kutokana na kumsababishia hasara kubwa mwekezaji
Magu akakataa akasema tupo sawa kwa sababu wamefanya udanganyifu wa kile kilichomo kwenye makinikia kwani kina thamani zaidi ya kile kinachotajwa
Wakatishia we lakini badala ya kujua kuwa wameyumba, wakaomba mazungumzo na wakalipa dola milioni 300 pia ikatumika sheria mpya ambayo serikali ikawa na uwakilishi ndani ya bodi na asilimia kadhaa katika kila uwekezaji katika maliasili ikiwemo hayo madini
Kuhusu sheria hiyo inafahamika ilisema kuwa migogoro yote isikilizwe katika mahakama za ndani, mpaka juzi hapa baada ya kuja dp world umeona sekeseke la kutaka sheria hiyo ibadilishwe na ikasikilizwe nje
Kuhusu hizo kesi unazosikia zilifunguliwa kabla ya sheria mpya na zile baada ya sheria mpya, waliakisi makubaliano waliyoyaingia wakati wanasaini mkataba