Ambiente Guru
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 2,605
- 1,085
Sijawahi ipenda nchi yangu baada ya Nyerere kama kipindi hiki cha Samia.
Salaam Wakuu,
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu yupo njiani anarudi
Hapa chini nimeweka nukuu alipokuwa anaongea na EATV
"Nimeambiwa niandike barua ili kudai gharama za matibabu, nimekusanya nyaraka zote zilizotumika kwenye matibabu kuanzia Dodoma, Nairobi hadi Ubelgiji, matibabu niliyoyapata baada ya Juni 2019 hayo hayahusiki kwa sabbau nilikuwa nimefutiwa ubunge,"
"Kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa Tanzania, Mbunge ana haki ya kupata kiinua mgongo ambacho ni asilimia 40 ya mishahara yake kwa kipindi alichotumikia, pale Ubunge wake unapofikia ukomo iwe kwa kifo, kufukuzwa, kuachishwa, kujiuzulu,"
"Haya mafao yangu ya kisheria yalipaswa kulipwa Juni 29, 2019 nilipofutiwa ubunge na Job Ndugai, kama mnavyofahamu zama zile Mungu alikuwa hajaamua, kwahiyo nilinyimwa hayo mafao,"
"Rais @SuluhuSamia alipokuja Ubelgiji na nikapata fursa ya kuzungumza naye na kumuambia kwamba nisipolipwa mafao yangu sasa itakuwa ni kwa sababu yako, na akasema atalifanyia kazi, nimelipwa miezi kama miwili iliyopita.
"Leo Waziri Msauni amezungumza wale wote waliokimbia Tanzania kwa sababu za kisiasa warudi watakuwa salama, hiyo ni kauli ya serikali iliyotolewa Bungeni, hiyo ni hatua nzuri sana, sasa kitakachofanyika ni mimi na wenzangu kuandaa safari ya kurudi,"
Chanzo: EATVSaa1