Tundu Lissu: CHADEMA haijapokea ruzuku hata senti 5, Baraza Kuu kukaa Machi au Aprili

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Ndg Tundu Lissu amesema, chama hakijapokea ruzuku yeyote toka serikalini na kama kuna mtu ana ushahidi kuwa wamepokea basi auonyeshe, kaongeza kusema, fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa ni chanzo kimoja tu cha mapato ya chama, kuna vyama havina ruzuku lakini vinaendesha shughuli zao. Chadema kina wanachama 6,700,000 hao wanachama ndio watakaoendesha shughuli za chama.

"Hatujapokea ruzuku yoyote. Katibu Mkuu wa @ChademaTz aliandikiwa barua na Msajili wa Vyama vya siasa aende kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ruzuku. Katibu mkuu alikataa, kama wanasema tumepokea ruzuku, waoneshe ni sehemu gani tumepokea na kusaini" Ndg. @TunduALissu.

Kuhusu wanachama 19 waasi waliofukuzwa Lissu kasema, kazi ya Kamati Kuu ni kusimamia katiba na misingi ya chama na wala sio kusimamia kanuni za Bunge, kama wanakwenda bungeni sio kosa letu ni kosa la aliyewapokea.

"Kamati Kuu ya @ChademaTz imeketi na kuamua kuwa wabunge 19 ambao wameasi na kukiuka maamuzi ya chama tuliwafukuza uanachama, kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu tangu 1965 tulipoingia rasmi katika mfumo wa chama kimoja mpaka leo, Mbunge akipoteza uanachama wa chama cha siasa anapoteza na ubunge, kama wanakwenda bungeni sio kosa letu ni kosa la wanaowapokea na kuwapa fedha za umma wakati si wabunge”.

"Ni kweli wabunge 19 tuliowafukuza wamekata rufaa. Kwenye kikao cha kamati kuu wiki iliyopita tumefanya maamuzi kuwa, kikao cha Baraza Kuu kitaitishwa kati ya mwezi Machi na Aprili, hatuwezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu eti tu kwa ajili ya kuwasikiliza hao waasi" @TunduALissu.
Excellent and mature information. Alluta continua. Members are ever ready to finance the party activities.
 
Baada ya kushambuliwa na watu inaosemekana hawajulikani na CCTV camera zilizonasa tukio, zikaondolewa na watu wanaojulikana halafu upelelezi ukakwama kisa aliyekua mgonjwa hayumo nchini, nadhani kwa mazingira hayo ndiyo maana akaona akae sehemu salama zaidi kuliko nchini ambako wewe na baadhi yenu mko salama na hamna sababu za kuondoka.
Au mkuu na wewe umewahi pigwa risasi japo mbili tu humuhumu nchini, halafu upelelezi wa tukio haukufanyika na umeamua kukaa salama salmini japo unapokea vitisho vya kuuawa na TCRA wala hawahangaiki na wale wanaokutishia?
Mkuu achana na hawa watu. Akili zao hazina akili. Unajisumbua bure kuwaeleza. "Just ignore them".
 
Baada ya uchaguzi wa 2020 kuna mengi chadema imeyapitia kiasi kwamba hakuna ruzuku iliyopaswa kwenda chadema.

Je, chama cha chadema kinapewa ruzuku? kama ndiyo kwanini na nani inaipokea?
 
Kwa nini ina wabunge
nani anapokea mwenye chama nafikiri unamjua.
 
Mbunge mmoja tu?
sasa hata kama chadema watapewa ruzuku kupitia mbunge mmoja ni bora awe anaichukua tu yeye huyo mbunge
 
Baada ya uchaguzi wa 2020 kuna mengi chadema imeyapitia kiasi kwamba hakuna ruzuku iliyopaswa kwenda chadema.

Je, chama cha chadema kinapewa ruzuku? kama ndiyo kwanini na nani inaipokea?
Chadema haipokei ruzuku kwa sababu haijawahi kupeleka namba ya akaunti kwenye ofisi ya msajili kama ilivyotakiwa kufanya baada ya uchaguzi wa 2020
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Ndg Tundu Lissu amesema, chama hakijapokea ruzuku yeyote toka serikalini na kama kuna mtu ana ushahidi kuwa wamepokea basi auonyeshe, kaongeza kusema, fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa ni chanzo kimoja tu cha mapato ya chama, kuna vyama havina ruzuku lakini vinaendesha shughuli zao. Chadema kina wanachama 6,700,000 hao wanachama ndio watakaoendesha shughuli za chama.

"Hatujapokea ruzuku yoyote. Katibu Mkuu wa @ChademaTz aliandikiwa barua na Msajili wa Vyama vya siasa aende kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ruzuku. Katibu mkuu alikataa, kama wanasema tumepokea ruzuku, waoneshe ni sehemu gani tumepokea na kusaini" Ndg. @TunduALissu.

Kuhusu wanachama 19 waasi waliofukuzwa Lissu kasema, kazi ya Kamati Kuu ni kusimamia katiba na misingi ya chama na wala sio kusimamia kanuni za Bunge, kama wanakwenda bungeni sio kosa letu ni kosa la aliyewapokea.

"Kamati Kuu ya @ChademaTz imeketi na kuamua kuwa wabunge 19 ambao wameasi na kukiuka maamuzi ya chama tuliwafukuza uanachama, kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu tangu 1965 tulipoingia rasmi katika mfumo wa chama kimoja mpaka leo, Mbunge akipoteza uanachama wa chama cha siasa anapoteza na ubunge, kama wanakwenda bungeni sio kosa letu ni kosa la wanaowapokea na kuwapa fedha za umma wakati si wabunge”.

"Ni kweli wabunge 19 tuliowafukuza wamekata rufaa. Kwenye kikao cha kamati kuu wiki iliyopita tumefanya maamuzi kuwa, kikao cha Baraza Kuu kitaitishwa kati ya mwezi Machi na Aprili, hatuwezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu eti tu kwa ajili ya kuwasikiliza hao waasi" @TunduALissu.
Lissu anampango wa kuwapiga tena hela wanyonge
 
Angeongea Mbowe au Mnyika waweza kuamini CHADEMA haijapokea ruzuku, Ila mtu yupo Ulaya tena kwenye LOCKDOWN aje kujua ya account za chama bongo!?.. au wanacheza na akili za NYUMBU wa ufipa wakamtumia Lissu kuwatuliza. Mchaga kwenye shilingi hajawahi kuniangusha
 
Mwanasheria Lissu anakiri Mdee & co wamekata rufaa inayotakiwa kusikilizwa na baraza kuu, lakini mwanasheria huyohuyo anasema hawawezi kuitisha kikao cha baraza kuu kujadili rufaa ya hao anaowaita waasi!

Kuna kitu hakipo sawa kichwani kwake.
Yaani bila hata rufaa za mdee baraza kuu lingeketi March/April kwahyo Lissu anadai kwamba hawawezi itisha Baraza kuu February kwa emergency eti kisa tu kuna rufaa za hawa wasaliti.

More so Rufaa imekatwa latter days za december hivyo mpaka March itakua haijazidi siku hizo 90 toka appeal iletwe.

Unajiita great thinker alafu unashindwa kuelewa simple explanations?
 
Back
Top Bottom