Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Achana na Vyama vya kwenye makaratasi. Vyama vya Mtungi hakuna vyama hapo
Hahaha Ina maana havina wanachama jomba..?? Unajua Kuna criteria za kuwa Vyama vya siasa..na idadi ya wanachama ni mojawapo
 
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huuuliopita.

Makamu huyo nguli wa sheria na siasa bora Tanzania ametumia nafasi hiyo kuwapongeza watanzania waliokiunga mkono chama hicho kikiwa katika hali ngumu ya kifedha.

" wanachama wetu na wafuasi waliendelea kufanya kazi za chama bure kabisa bila malipo, na hii inaonesha kuwa Chama chetu ni chama cha watu."

Wajenge ofisi sasa, japo tumewaona hawana msimamo.
 
Achana na Vyama vya kwenye makaratasi. Vyama vya Mtungi hakuna vyama hapo
Sasa jomba we unazungumzia chama gani..kwa sababu Chadema Wana Mbunge mmoja tu..wale wengine Covid 19 wametemwa zamani ingawa ruzuku yao inaendelea kuchukuliwa... Hahahah..sijaelewa hapa wajameni
 
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huuuliopita.

Hii ni hatua nyingine ya matunda ya maridhiano yanayoendelea baina ya chama hicho na serikali.
Hatuisifu sirikali ya Mama ila ni haki zetu. Mungu amzidishie afya njema na ulinzi tele. Aliyetembea na kuvukia ngambo akwame huko huko. Period!
 
Makamu Mwenyekiti Mh Tundu Lissu akiwa ktk mtandao wa Club house ameweka wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeanza kupokea Ruzuku Mwezi huuuliopita.

Hii ni hatua nyingine ya matunda ya maridhiano yanayoendelea baina ya chama hicho na serikali.
Swali la msingi ni jee msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi wowote bila Katiba Mpya uko pale pale? Au maridhiano yanawafanya waamini kuwa haki itatendeka?

Amandla...
 
Hahahah jomba ,,Tanzania Ina jumla ya Vyama 23 kama sijakosea..pls correct if am wrong
Chadema ndo chama pekee Cha upinzani hapa nchini... hivyo vingine ni wavuvi na maswahiba wa ccm ... chama hakina wanachama 20 nchi nzima??? Kikitaka kufanya mkutano mkuu kinaazima wanachama kutoka ccm
 
Hahahah jomba ,,Tanzania Ina jumla ya Vyama 23 kama sijakosea..pls correct if am wrong
Kwa majina ubaoni pale Kwa msajili, huku mtaani hakuna anayeiulizia KATIBA au Tume huru ukiacha CDM na UMOJA- wa Bavicha.
Vingekuwepo na kupiga kelele ya KATIBA ingeahapatikana. Wamekaa kimyaaah!!
 
Sasa jomba we unazungumzia chama gani..kwa sababu Chadem Wana Mbunge mmoja tu..wale wengine Covid 19 wametemwa zamani ingawa ruzuku yao inaendelea kuchukuliwa...hahahah..sijaelewa hapa wajameni

Idadi ya kura chama kimepata ktk uchaguzi ndiyo inayo-determine kiwango cha ruzuku, na idadi ya wabunge wa viti maalum.

..wabunge wa viti maalum hawaongezi wala kupunguza kiwango cha ruzuku.
 
Back
Top Bottom