Tundu Lissu, hana mapenzi mema na Watanzania

Mwenye mapenzi mema na tanzania ni yule aliyempoteza ben saanane,aliyemuua mwangosi, aliyemuua mawazo, aliyempoteza azory gwanda, aliyempiga risasi tundu lissu na aliyekuwa anatupa watu kwenye viroba mto ruvu
Ambaye ni nani?
 


Hakuna mtu anajua uchungu wa risasi hivyo kama kweli ana amini Magu ndiye alitoa maelekezo ya yeye kupigwa hatuwezi kulazimisha mapenzi yake kwa hao wawili. Wewe na mimi hatujawahi kupigwa risasi hivyo haya hayatuhusu tuache umbeya
 
Asante Mkuu!!!! Mwambie huyo mjinga..
 
Umeandika ujinga.

Nilidhani utaweka hoja ya mambo aliyoyafanya au kunena, kumbe ni porojo za hisia.

You must be among the very low IQ creature.
 
Wew ni mgeni hapa nchini?
 
Kwa mapenzi ya JPM kwa watanzania wote akiwemo Tundu Lissu hili unalosema ni hakika kabisa.
Tundu Lissu anamchukia mtu anayewapenda Watanzania wote pamoja na yeye.
Hakika umenena!
 
Kwa mambo ambayo Magufuli amemtendea Tundu Lissu unapaswa kukaa kimya au kufuta huu upuuzi ulioweka hapa.
 
Kwani yeye ndie aliyemuambukiza corona jomba!!?

Angekufa kama mlivyotaka mngemtaja nani leo??

Kimeumanaaaa. Na Viwanda vizalishe bia kwa wingi tukijiandaaa kufurahi
 
Ulichoandika hapa ni takataka.

Huyo unayemtetea alishaonesha wazi hampendi Lissu. Unataka Lissu ampende kinafiki? Hapana kwa kweli.
 
Hana mapenzi mema na Watanzania kwasababu kaonesha chuki binafsi, mwanzo nilijua ni siasa tu hampendi magufuri kisa uongozi lakini imedhihilika wazi kuwa hampendi personal.

Kwa taarifa yako hata magufuli hampendi Lissu,, wale ugomvi wao ni personal so usihusishe wananchi kwenye hilo..

Kumchukia magufuli sio kuichukia Tanzania.. Acha kueneza chuki zisizo na msingi..

Lissu akimchukia magufuli haifanyi wewe ukose huduma za kijamii so Ugomvi hautuhusu wananchi.

Only God knows
 
Unamtuhumu TAL bure kabisa !!. Akiwa mahututi hajitambui kitandani baada ya jaribio la mauaji dhidi yake. Wabunge wenzie wasio wa chama chake walizuiliwa hata kumjulia hali. Wananchi walipojaribu kumfanyia ibada walisambaratishwa. Hata fulana za kumtakia heri zilikuwa jinai !!

Na mpaka leo hakuna uchunguzi ulioendelea . Mtu kama huyu unamlaumu kwa lipi ?! Mwache atapike nyongo. Dunia hii ndivyo ilivyo
 
We kama ulishiriki kumtungua Lisu jiandae naona wasiojulikana mnahaha.Wasiojulikana mtatuelezea tu ndugu zetu mmewaficha wapi tunasubiria tu kivuli kitoweke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…