Zanzibar 2020 Tundu Lissu: Hatuna maslahi na Urais Zanzibar, tutatangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif

Zanzibar 2020 Tundu Lissu: Hatuna maslahi na Urais Zanzibar, tutatangaza rasmi kumuunga mkono Maalim Seif

Katiba haijazuia waziri kuteuliwa kutoka chama ambacho hakijashinda. Inataka ili uwe waziri uwe mbunge tu.

Pia, sheria ya uchaguzi haijalazimisha chama kilichoshinda kitekeleze ilani yake. Ndo maana ccm haijatekeleza ahadi nyingi na haijafutwa. Na Mengine yametekelezwa hayapo kwenye ilani na hakuna tatizo kwa mujibu wa sheria.

Kilichopo, ofisi ya msajili na NEC wanajivua nguo kujionesha ni watupu kichwani
 
Kila jambo na wakati wake,hawajachelewa hata sasa mabadiliko yanapoenda kutimia ni suala la muda muafaka.Hakikisha Mh.Lissu anapata kura yako,rafiki,familia na jamaa wote walio katika ushawishi wako ili Mh.Lissu apate ushindi wa kimbunga.Yangu na wanaonizunguka anayo tunasubiri siku ifike tufanye yetu.
Ukitaka kushindwa uraisi wa Tanzania uwe wa muungano au wa Zanzibar ni kazi ndogo mno

1.Tukana Nyerere ;Wote waliowahi tukana Nyerere uraisi hawakupata wawe ndani ya CCM au nje ya CCM
2.Pinga muungano huu uliopo na pania kuuvunja na ujiunge na wapinga muungano na wavunja muungano wote wapinga huu muungano uliopo hawajawahi shinda uraisi wawe ndani ya CCM au nje ya CCM

Mifano mizuri ni Aboud JUMBE alifukuzwa hadi uraisi mwingine Ni Seif SHARIFF Hamad na ,Edward Ngoyayi Lowasa

Lisu anaunga foleni ya washindwa kushika uraisi sababu alimtukana marehemu Nyerere bungeni Live !!! na pili hataki muungano huu uliopo na kaenda kujiunga na wapinga muungano akina Seif Sharrif Hamad!!! hiyo ni tiketi ya moja kwa moja ya kushindwa uraisi wote yeye Lisu na Seif Sharrif Hamad wake.
 
Lissu yuko bold, angekuwa Lowassa leo angekuwa Dodoma kwenye maadili.
Wakati wa Bwana ndio huu.


JESUS IS LORD.
Ujasiri wa kipuuzi na yeyote anayeunga mkono upuuzi wake ajiandae kwa lolote litakalomtokea iwapo atatakiwa kuingia barabarani.

Hadi ninapoandika kujibu vioja vyenu hivyo, badala ya hoja, huyo mgombea Urais anatangaza na kuchochea vurugu tu. Sina sababu ya kunukuu baadhi ya vioja vyake vyenye utata.

Tanzania ilikuwepo na itaendelea kuwepo kwa uongozi ulio thabiti kuleta maendeleo na siyo uwongo wa "nitafanya hiki au kile".
 
Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu kwa ulevi tu wa madaraka wanadhani ile Mahakama ya The hugue ni pambo tu, wawaulize wenzao Kwanza.
Marekani wamepiga marufuku afisa yeyote wa ICC asikanyage kwao

Nchi kibao zimejitoa ikiwemo Burundi,Afrika ya kusini ,Ghambia nk

Nchi nyingine hawataki hata kuisikia hiyo mahakama na marufuku kwao nazo ni Urusi,India,Japan ,China, Iraq, Israel, Libya, Qatar, the United States, na Yemen.

Hiyo mahakama is not a big deal hata sisi tunaweza sepa tu kuwaambia kaeni na kimahakama chenu hatukitaki tunajitoa na hawana cha kutufanya

Mnnatishia nyau nani?
 
  • Thanks
Reactions: len
Kwa misimamo hii ya Lissu, nashauri Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi watimize wajibu wao tu;

Kutangaza kwa haki Mgombea aliyepata kura nyingi na Kulinda Raia na Mali zao.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki watanzania.

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
Nawaache kutu ika kwa mslahi ya upande Fulani.
 
Amechemka kwenye kampeni anatafuta sababu za kuenguliwa sasa!
Siyo hilo tu, anatafuta pia mahali pa kuanzia, pa kuichokonoa hii Serikali, kwani kwa mawazo yake na ubishi wake usio kuwa na maana, anadhani anamkoa yoyote kwa kutimiza matakwa na maelekezo ya hao mabeberu waliomtuma. Kama ambavyo huwa anasema Rais mmoja wa nchi moja jirani yetu kuwa "anasubiri the right time and right time to place to strike". Ndivyo itakavyo kuwa.
 
Sometimes muwage na akili ata kdg, safari hii hila na maovu yenu yanatazamwa kwa dunia nzima, wauaji na watesaji saa yenu yaja.
Mumfundishe huyo jamaa yenu kwamba urais siyo umonitor wa darasa la nne!

Huna maslahi na Zanzibar alafu unataka uwe rias wa jamhuri ya Muungano,.

Hata chizi atakuona hujielewi maana hakuna chombo chochote cha usalama kitakuunga mkono.

Mwambie urais ni kuwa amiri jeshi mkuu na mtoa amri wa maslahi ya nchi na mipaka yake siyo kwa ajili ya kumfurahisha Amsterdam.
 
Hao wengine Mrema na Cheyo matamko yao yaidhinishwa na kamati kuu zao na mikutano mikuu yao

CHADEMA hilo halipo ni Lissu kujiropokea mwenyewe kwenda mbele
Wewe huna shule kichwani. Umeambiwa ACT na CDM hazijaungana, ndiyo sababu hakuna maamuzi ya hizo kamati kuu.
 
"Lissu ananipa raha Sana yeye uwa aongelei Jambo bila reference"
Yaani anakufurahisha kupotosha du chadema mna matatizo makubwa, sikiliza; mrema alipeleka mapendekezo mkutano mkuu ukaridhia na hata Cheyo alifanya hivyo na akatangaza hadharani. Lissu ni janga la taifa, amewashika masikio hadi mnamuita jembe lenu. Jaribuni muone sheria inavyofanya kazi.TLP na UDP wana muhitasari wa maamuzi ya mikutano mikuu. Chadema janga la Taifa
 
Hii CHADEMA iwekwe pembeni kwanza hadi itakapo kuja na agenda ya Muungano. Tanzania haiwezi gawanwa kama vipande vya mandazi. Huyu Lissu hana aibu na watanzania waliolinda Umoja uliopo. Lake ni kuingia ikulu tu kitu ambacho hatoona Maisha yake yote.
 
Waliokaribu na TAL, tafadhali mshaurini kuwa kila anapoulizwa swali kuhusu ubeberu, kabla hajalijibu amuulize muulizaji iwapo hata anajua maana ya 'ubeberu'. Ubeberu ni nini? "ubeberu" ni msemo/dhana inayotumiwa na serikali dhalimu za Afrika (ikiwemo hii ya CCM) kuwapumbaza wananchi waliowanyongeyesha (zinaposhindwa kutimiza wajibu wao) kuwa unyonge wao umesababishwa na 'watu fulani kutoka nje' (mabeberu) na sio wao. Miaka 60 ya uhuru bado unawaaminisha watu kuwa matatizo yao yanasababishwa na 'mabeberu'!!! TAL awajibu kwa kifupi hao wanaomuuliza kuwa 'ubeberu' ni msamiati ama propoganda ya kuendelea kupumbaza wananchi.
 
Back
Top Bottom