Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

Halafu wapigaji wakiwa wanapiga kutokea nyuma ya gari lao
 
Haina uhusiano hii..
 

wahalifu waliotoa kamera CCTV , walioshut risasi , watajulikana tu.
 
Huwezi kuwa shuhuda wa tukio halafu ukadanganya tukio lilivyotokea
Halikuwa tukio la siri japo hawajapatikana wahusika...hili ni tukio la jinai. Wacha polisi waendelee nalo..
 
Wewe inaonekana hata masikio hayafanyi kazi. Habari hii iliongelewa kwa kirefu, na aliyetoa maelezo marefu zaidi alikuwa ni dereva. Sasa wewe labda una tatizo la kutosikia, au una tatizo la kutokuwa na kumbukumbu, au una tatuzo la unafiki.

Dereva alieleza wazi namna alivyojitahidi kumwokoa Lisu. Alimvuta Lisu toka upande wa kushoto mpaka kwenye upande wa dereva, akamshusha chini ambako huwa inakaa miguu ya dereva, ni sehemu ile ambayo ipo brake na accelerator. Dereva alishuka na kutambaa mpaka chini, akaingia kwenye uvungu wa gari bovu lililokuwepo hapo. Halafu wewe bado unaleta maswali yasiyo na vichwa wala miguu.

Yawezekana uovu unakufanya uwehuke.
 

..Lissu amesema risasi zilipigwa " AT AN ANGLE " kuelekea upande wake.

..Hakukuwa na nafasi ya kuegesha gari lakini haimaanishi hakukuwa na nafasi ya washambulia kulenga alipokuwa amekaa Lissu.

..Haiwezekani kumtambua mtu anayekutupia marisasi. Kitendo cha kwanza kitakuwa ni kuepa au kujikinga na risasi hizo.

..Nafasi ya kuwatambua ingekuwa kabla ya kumshambulia, au kama watu hao wangekwenda na kuzungumza na Lissu kabla ya kumshambulia.

..Dereva ameshawahi kuhojiwa na vyombo vya habari. Polisi wanaweza kumhoji wakishirikiana na Polisi wa Ubelgiji.
 
Kweli kuna maswali mengi tu Wananchi wanataka wajuzwe. Shauku ni kubwa. iwe ni kutoka Serikalini- Polisi, na vyombo vingine, au kutoka kwa Mh. Tundu Lissu ambaye mwenyewe alishatoaga kauli na kusema "anayo mengi" atujuze

Sasa kwa avile hili ni suala nyeti(kuna uchunguzi) haina maana haliwezi kujadiliwa humu, walakini kuwa wenye kufanya uchunguzi watakaa pembeni nanlabda kulokota machache yanaoweza kuwasaidia kwa kifikra au kwa vielelezo ambavyo havipatikani sehemu nyingine...

Pili, wale wanaoendeleza kudai kila kukicha wanamjua 'muuaji' basi wasilalame kuona kuna Wananchi walio na shauku ya kujua Ukweli? Yaaani nani anasema Ukweli

Tumechoka, tumechoka kuona Familia zikiumizwa kila kukicha kwa visingizio visivyo na kichwa au miguuu...iwe ni Familia zinazohusishwa na kuyafanya hayo mauaji au Familia zinazokisia, kudhani zimefanyiwa hayo mauaji...udhalimu.

kwakweli....

Hivi kweli ...kiunagaubaga ....umiminiwe 16 zote ziwe za miguuni? alisikika mwanaharakati mmoja

Mnakumbuka kuhusu ' wale hawakoseagi'? au Tunajizima ufahamu?

Kieleweke Kitaeleweka.
 
Aendelee kushuhulika na biashara ugoro
 

..Lissu ameumizwa mwili mzima.

..miguu yote iliumizwa kwa risasi. pia mikono yote na tumboni kulikuwa na risasi.

..mguu wa kulia risasi ilivunja goti ndio maana ulemavu uko upande huo.

..hapa chini utaona video Lissu akielezea majeraha yake, ukisikiliza utaona mkono wa kushoto una ulemavu kuliko wa kulia.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…