Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

Tundu Lissu hebu tueleze vizuri tukio la kupigwa risasi lilivyotokea haya uliyotoa yanaacha maswali mengi sana

Kwa wanaoijua CHADEMA inawezekana kabisa ni inside job!
  1. CHADEMA mabingwa wa mapichapicha, walijitahidi kuhakikisha picha za tukio hilonhazisambai kinyume na utamaduni wao!
  2. Risasi kutoboa upande moja wa gari na yeye kuumizwa upande mwingine. Risasi zitoboe kushoto na muathirika aumie mguu wa kulia!
  3. Dereva aliyeko kulia risasi isimpate hata moja!
  4. Zipigwe risasi 38 na atoke kama alivyotoka!
  5. Dereva kuingia mitini na mpkumficha kwa nguvu zote!
Halafu wapigaji wakiwa wanapiga kutokea nyuma ya gari lao
 
Wala siko huko- kwa alivyoeleza ni sahihi hajapigwa risasi atakuwa aliletwa hapo na dreva wake akiwa majeruhi tayari. Hebu fikiria unachema ulisoma chuo na kuhitimu mwaka fulani ila huwezi kumtaja hata mwanafunzi mmoja uliyesoma naye- maana yake hujawahi soma chuo hicho unachosema
Haina uhusiano hii..
 
Maelezo ya Lissu alipohojiwa na CLOUDS
Nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking. Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao

Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Lissu

MASWALI
1. Je risasi zilipigwa kutoka nyuma yake ?
2. Mbona gari lake lilionekana kuwa risasi zilikuwazimepigwa ubavuni. Kama niko sahihi hii iliwezekana vipi wakati hakukuwa na nafasi ya wao kuegesha gari hapo? Maana yake ni kuwa nafasi kati ya gari na gari kwenye maegesho isIngeweza kumfanya mpigaji atumie bunduki kwa usahihi mpaka asogee karibu sana na hii ingemfanya amtambue aliyemshambulia.
3. Kwa nini dreva wake kama mtu aliyekuwa kwenye tukio anamzuia asitoe maelezo yake?

wahalifu waliotoa kamera CCTV , walioshut risasi , watajulikana tu.
 
Huwezi kuwa shuhuda wa tukio halafu ukadanganya tukio lilivyotokea
Halikuwa tukio la siri japo hawajapatikana wahusika...hili ni tukio la jinai. Wacha polisi waendelee nalo..
 
Kwa wanaoijua CHADEMA inawezekana kabisa ni inside job!
  1. CHADEMA mabingwa wa mapichapicha, walijitahidi kuhakikisha picha za tukio hilonhazisambai kinyume na utamaduni wao!
  2. Risasi kutoboa upande moja wa gari na yeye kuumizwa upande mwingine. Risasi zitoboe kushoto na muathirika aumie mguu wa kulia!
  3. Dereva aliyeko kulia risasi isimpate hata moja!
  4. Zipigwe risasi 38 na atoke kama alivyotoka!
  5. Dereva kuingia mitini na mpkumficha kwa nguvu zote!
Wewe inaonekana hata masikio hayafanyi kazi. Habari hii iliongelewa kwa kirefu, na aliyetoa maelezo marefu zaidi alikuwa ni dereva. Sasa wewe labda una tatizo la kutosikia, au una tatizo la kutokuwa na kumbukumbu, au una tatuzo la unafiki.

Dereva alieleza wazi namna alivyojitahidi kumwokoa Lisu. Alimvuta Lisu toka upande wa kushoto mpaka kwenye upande wa dereva, akamshusha chini ambako huwa inakaa miguu ya dereva, ni sehemu ile ambayo ipo brake na accelerator. Dereva alishuka na kutambaa mpaka chini, akaingia kwenye uvungu wa gari bovu lililokuwepo hapo. Halafu wewe bado unaleta maswali yasiyo na vichwa wala miguu.

Yawezekana uovu unakufanya uwehuke.
 
Maelezo ya Lissu alipohojiwa na CLOUDS
Nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking. Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao

Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Lissu

MASWALI
1. Je risasi zilipigwa kutoka nyuma yake ?
2. Mbona gari lake lilionekana kuwa risasi zilikuwazimepigwa ubavuni. Kama niko sahihi hii iliwezekana vipi wakati hakukuwa na nafasi ya wao kuegesha gari hapo? Maana yake ni kuwa nafasi kati ya gari na gari kwenye maegesho isIngeweza kumfanya mpigaji atumie bunduki kwa usahihi mpaka asogee karibu sana na hii ingemfanya amtambue aliyemshambulia.
3. Kwa nini dreva wake kama mtu aliyekuwa kwenye tukio anamzuia asitoe maelezo yake?

..Lissu amesema risasi zilipigwa " AT AN ANGLE " kuelekea upande wake.

..Hakukuwa na nafasi ya kuegesha gari lakini haimaanishi hakukuwa na nafasi ya washambulia kulenga alipokuwa amekaa Lissu.

..Haiwezekani kumtambua mtu anayekutupia marisasi. Kitendo cha kwanza kitakuwa ni kuepa au kujikinga na risasi hizo.

..Nafasi ya kuwatambua ingekuwa kabla ya kumshambulia, au kama watu hao wangekwenda na kuzungumza na Lissu kabla ya kumshambulia.

..Dereva ameshawahi kuhojiwa na vyombo vya habari. Polisi wanaweza kumhoji wakishirikiana na Polisi wa Ubelgiji.
 
Kweli kuna maswali mengi tu Wananchi wanataka wajuzwe. Shauku ni kubwa. iwe ni kutoka Serikalini- Polisi, na vyombo vingine, au kutoka kwa Mh. Tundu Lissu ambaye mwenyewe alishatoaga kauli na kusema "anayo mengi" atujuze

Sasa kwa avile hili ni suala nyeti(kuna uchunguzi) haina maana haliwezi kujadiliwa humu, walakini kuwa wenye kufanya uchunguzi watakaa pembeni nanlabda kulokota machache yanaoweza kuwasaidia kwa kifikra au kwa vielelezo ambavyo havipatikani sehemu nyingine...

Pili, wale wanaoendeleza kudai kila kukicha wanamjua 'muuaji' basi wasilalame kuona kuna Wananchi walio na shauku ya kujua Ukweli? Yaaani nani anasema Ukweli

Tumechoka, tumechoka kuona Familia zikiumizwa kila kukicha kwa visingizio visivyo na kichwa au miguuu...iwe ni Familia zinazohusishwa na kuyafanya hayo mauaji au Familia zinazokisia, kudhani zimefanyiwa hayo mauaji...udhalimu.

kwakweli....

Hivi kweli ...kiunagaubaga ....umiminiwe 16 zote ziwe za miguuni? alisikika mwanaharakati mmoja

Mnakumbuka kuhusu ' wale hawakoseagi'? au Tunajizima ufahamu?

Kieleweke Kitaeleweka.
 
Mleta mada ni wazi wewe sio mtaalamu wa kupeleleza jambo hili na maswali unayouliza yanaweza hata yasiulizwe na mtaalamu wa uchunguzi. Jaribu kushughulika na mambo uliyo na uwezo nayo!!

Vijana wa nchi hii tutadharauliwa kwa ujumla wetu kumbe dharau ilipaswa kuelekezwa kwako tu.
Aendelee kushuhulika na biashara ugoro
 
Kwa wanaoijua CHADEMA inawezekana kabisa ni inside job!
  1. CHADEMA mabingwa wa mapichapicha, walijitahidi kuhakikisha picha za tukio hilonhazisambai kinyume na utamaduni wao!
  2. Risasi kutoboa upande moja wa gari na yeye kuumizwa upande mwingine. Risasi zitoboe kushoto na muathirika aumie mguu wa kulia!
  3. Dereva aliyeko kulia risasi isimpate hata moja!
  4. Zipigwe risasi 38 na atoke kama alivyotoka!
  5. Dereva kuingia mitini na mpkumficha kwa nguvu zote!

..Lissu ameumizwa mwili mzima.

..miguu yote iliumizwa kwa risasi. pia mikono yote na tumboni kulikuwa na risasi.

..mguu wa kulia risasi ilivunja goti ndio maana ulemavu uko upande huo.

..hapa chini utaona video Lissu akielezea majeraha yake, ukisikiliza utaona mkono wa kushoto una ulemavu kuliko wa kulia.

Back
Top Bottom