Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nadhani huna kumbukumbu. Kumlinda mhalifu ni kazi sana.1. Kama parking ilikuwa imejaa wenye magari walikuwa wapi? Kikawaida kungekuwa na mayoress na watu wengi.
2. Alienda lunch, kwa nini wenzie hawakwenda lunch? Na hayo magari kujaa yangejaa vipi kama wenyewe hawakuenda lunch?
3. Walinzi wa parking walikuwa wapi? Walijuaje kama atakuja lunch siku hiyo? Walinzi wa hao wenye magsri yaliyojaa walikuwa wapi?
4. Kwa nini wauaji risasi 16 wakuvunje miguu, si wangepiga tumbo au kichwa?
5. Mlinzi hakukimbia alisema alilala kwenye kiti chake ambako ndiko risasi ziltokea. Aliponaje? Yuko wapi?
6. Uhusiano wa Tundu na majirani ulikuwaje wasimsaidie hadi leo, kikawaida husaidiana kwenye Iddi na Ubatizo na maziko. Tundu alikuwa adui wa kila mtu?
Maelezo ya dereva ni kwamba alipoona mshambuliaji anatoka na bunduki, alimvuti Lisu na kumpeleka upande wa dereva na kumshusha chini eneo ambalo kuna accelerator na brake pedals. Yeye dereva alitambaa kushuka chini na kwenda kulala kwenye uvungu wa gari lililokuwa hapo karibu. Dereva anasema alishuhufia na kumwona mshambuliaji aliyekywa amevaa cap na mask. Wakati shambulizi linaendelea alimsikia Lisu anapiga kelele, akajua atakuwa amefikiwa na risasi. Gari lilipoondoka tu, ndiyo alienda kumwona akiwa amejeruhiwa vibaya. Dereva alishuhufia tukio lote, na hiyo ndiyo sababu ya wauaji kumtaka sana dereva kwa sababu wanajua alishuhufia shambulizi lote.
Ifahamike kuwa kwa kuwa nafasi ile aliyowekwa Lisu ni ndogo, huwezi kuwa na uhakika kwa kujibana kwenye nafasi ile, alilala kwa namna gani. Huenda kiwiliwili na kichwa vilikuwa chini, na miguu ilikuwa juu.