Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Huyo mwanaharakati aache kugeuza tukio Lake kuwa mtaji wa kisiasa, mtu yoyote akitendewa kinyume na sheria hasa kijinai anajukumu la kutoa taarifa kituo cha polisi cha jirani yake na pia ana jukumu la kutoa ushirikiano wa kutosha kuwezesha upelelezi na kumpata aliyemtendea uhalifu huo.

Pamoja na kuwa alikuwa akijiuguza huko nchi jirani baadae Ulaya lakini baada kupata nafuu hakurudi nyumbani kutoa ushirikiano na polisi lakini akawa anapiga misele kwenye vyombo mbali mbali vya habari akihubili kuhusu kupigwa risasi ili aonewe huruma na aje kugombea uraisi na uchaguzi ulipo karibia alirudi na hakwenda kulipoti polisi akafanya kampeni na baada ya kushindwa uchaguzi alisingizia anatishiwa

bila kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na wala hakusema anatishiwa na nani na kwanini na matokeo yake alikwenda kutunga uwongo kwenye ubalozi wa nchi fulani ya ulaya akasafirishwa kwenda huko alipo na wakati alifanya kampeni takribani miezi mitatu huku akikorofishana na polisi mara nyingi.
 
..Igp hasemi ukweli.

..angekuwa anamtafuta dereva wa Lissu na wameshindwa kumpata angewatumia Interpol kumkamata na kumrudisha nchini.

kwanini itumike nguvu,wakati mlalamikaji kagoma hata kufungua kesi!!!
 
Huyo mwanaharakati aache kugeuza tukio Lake kuwa mtaji wa kisiasa, mtu yoyote akitendewa kinyume na sheria hasa kijinai anajukumu la kutoa taarifa kituo cha polisi cha jirani yake na pia ana jukumu la kutoa ushirikiano wa kutosha kuwezesha upelelezi na kumpata aliyemtendea uhalifu huo...
Lissu ajaongelea hili Jambo IGP ndio kafukua makaburi
 
Mtu anakwambia anafatiliwa wewe unapuuza

Walinzi wanaondolewa kwenye makazi yake alafu anapigwa risasi eneo ilo ilo...
Sijui kwa nini, lakini baada ya kushindwa kumwua TL, nilikuwa naona Mag angetangulia kufariki kabla ya TL. Ilistahili TL ashuhudie kifo cha aliyetaka kumwua. Na yote, ni ili ukuu na utukufu wa Mungu upate kushuhudiwa na wengi waliojaliwa macho ya kiroho.

Marehemu amemaliza safari yake, lakini kubwa zaidi ni kwa tuliobakia nyuma, kujiuliza kama kuna kitu chochote tulichojifunza katika dhamira zetu.

Uweza wa Mungu ni mkuu, tuishi kwa kuhofu kutenda kinyume na maagizo yake. Tunaweza kuwa dhaifu na wadhambi, lakini tusikufuru na kujiona ni wenye uweza kama wake hata wa kuamua nani aishi na nani asiishi, nani afurahie na nani ateseke, nani apendelewe na nani aonewe.

"Mungu wetu kwa maisha ya huyu mwenzetu uliyemwita kwako, imekuwa ni injili inayoishi. Injili hii iyaguse maisha yangu, japo mimi siyo Rais, lakini kwa nafasi yangu natambua nina wajibu wa kutenda haki, wajibu wa kuwasaidia wenzangu wapate haki uliyoitoa wewe mwenyewe, haki ya kuishi, wapate maisha ya furaha, wapate kilicho haki yao, maana najua ni katika wao, uMungu wako unaishi, na katika mema ninayowatendea wenzangu ikawe sababu ya kupata msamaha wangu pale nitakapopungukiwa, siku utakaponiita kwako. Tunaomba uwape faraja ya pekee wale ambao ndugu zao waliuawa, ndugu zao walipotezwa, ndugu zao walitekwa.

Faraja yao inaweza kupatikana kutoka kwako tu, na wala siyo kutoka kwa mwanadamu yeyote maana majonzi yao hayapimiki wala kuhesabika. Wayapokee yaliyotokea kama sadaka yao kwaajili ya uovu wa Ulimwengu. Naomba wakati wote unijalie moyo wa kuyaona maovu yangu kabla ya kuyaona ya wengine"

Ni upendo gani unaozidi ule wa mtu kuyatoa maisha yake kwaajili ya rafiki zake? Maneno haya yadumu moyoni mwangu na kwa yeyote anayetaka kuuona ukuu wako.
 
Kama kuna wasiojulikana walifanya umafia siku zao zinahesabika watajulikana tu ni kina nani hawa. Utumishi wao ulitumika vibaya.
 
Huyo mwanaharakati aache kugeuza tukio Lake kuwa mtaji wa kisiasa, mtu yoyote akitendewa kinyume na sheria hasa kijinai anajukumu la kutoa taarifa kituo cha polisi cha jirani yake na pia ana jukumu la kutoa ushirikiano wa kutosha kuwezesha upelelezi na kumpata aliyemtendea uhalifu huo...
Risasi ulizomrushia hazikufua dafu sembuse haya maneno yako tu ?
 
IGP anaalikwa kipindi...medani za siasa.... Mkuu wa polisi amekuwa mwanasiaa!!
 
IGP alivuka hadhi ya nafasi yake. Angeishia kusema alimpigia Lissu simu hakwenda wenye akili wangemwelewa lakini alipoongeza kwamba Lissu anafurahia/anatumia hali aliyonayo kujipatia fedha, hata wasio na akili wakaona IGP ni ndugu yao.
Kwani uongo?

Niambie kinachomuweka Lisu kwa amsterdam mpaka muda huu ni nini wakati kapona
 
Haya si maneno yangu, bali ni maneno ya Kamanda wetu alieko ughaihuni aliyoyatoa leo kupitia twitter akimjibu kibosile fulani aliebua upya sakata hili.

Kamanda kadai kuwa alipata taarifa kuwa Bwana Yule aliagiza amalizwe mara baada ya uchaguzi kwisha.

Hakika Bwana Yule alikuwa na tatizo tena sio dogo.
 
Back
Top Bottom