Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, ilani yako na CHADEMA itahitaji msaada zaidi ya asilimia 90, tutarudi utumwani

Joka,hili la wamachinga kutozwa au kutotozwa linahoja lakini muda mwingine mtu akilipia Kodi inampa haki ya kudai huduma bora zaidi hususani kutoka serikalini

..TRUE.

..mimi ningependa wamachinga wapungue kwa kuwa integrated ktk ajira za kudumu ktk sekta nyingine.

..sasa hivi tuna wamachinga mpaka wenye elimu ya chuo kikuu, halafu tunategemea walipe mikopo ya elimu ya juu.

..hapa kwa kweli tuweke vyama pembeni, tu-demand toka kila kampeni[ccm,act,cdm,cuf..] waeleze jinsi gani watasaidia kupunguza wamachinga.

NB:

..asante kwa kuanzisha mjadala huu.

..umepelekea tuka-strike a common ground.

..this is a culture that we need to encourage ktk siasa zetu, badala ya kuchukuliana kama maadui na kuitana majina mabaya.
 
Hilo la wamachinga kuwa integrated kwenye ajira (white colour job) ni mtazamo tu kwani ajira ipo katika mfumo wa ofisini na usio wa ofisini.

Hawa wamachinga walio wengi wanaingiza fedha nyingi kwa siku/wiki/mwezi kuliko hata walio maofisini.

Hoja kubwa ni kuboresha mazingira yao ili waweze kuwa endelevu.
 
Unataka kusema pesa yetu ya ndani kazi yake ni kununua ndege harafu za pesa za kuwapatia watoto wetu elimu bora kwa maana ya ujuzi na maarifa ili waweze kujiajiri na kuongeza tija kwenye shughuli za ujenzi wa taifa lao inabidi tusubirie msaada,kweli ccm akli zenu mnazijua wenyewe Ila samahani sijasoma post yako,nimesoma tu heading
 
ndugu muandish katika hoja yako ya LOAN BOARD nakubaliana na wewe huu ni mfuko unaopashwa uwe na mzunguko.Mzunguko unapatikana vipi? mzunguko lazima upatikane kwa wanufaika kurudisha fedha za mikopo.na hili linafanyika hata katika nchi za wenzetu.Mfano ulaya na marekan kila mhitimu wa chuo asilimia kubwa ni walikopa.
 
Umeongea kiuhalisia bila chenga 100% mkuu.
Ukiangalia kale ka kitabu ka sera za ilani alikoshikilia Lissu ni kama kametungwa na kuchapishwa ndani ya siku mbili.
Bila kufanyiwa tafiti za kiuhalisia, kwa ujumla ile sio sera bali hasira na uchonganishi mtupu.
 
Said kubenea pamoja na elimu yake ya kuunga unga anamzidi Magu phD maarifa kwa mbali sana.Said Kubenea aliwahi kuwaambia wananchi wa kimara na ubungo kuwa serikali haiwezi kushindana na wananchi wake,kwa lugha nyingine ni kuwa nyumba haiwezi kushindana na mmiliki wake.Serilali ni nyumba na wamiliki wa nyumba ni watanzania.ulikuwa ni uvivu wa kufikiri wa Magu kudhani serikali ni mshindani wa wananchi,ndo maana WB ilimnyima pesa
 
Mzunguko si lazima iwe 18% toka kwenye mishahara,kule REA tunalipa asilimia ngapi na kazi ya kusambaza umeme ikoje vijijini? Kama ustawi wa maisha ya mtanzania ungekuwa muhimu kwa ccm na chato boy tungetafuta vyanzo vingine vya mapato kwa ajiri ya loan board na si kufukarisha watanzania
 
Chapa kazi najua unapenda sana kutawaliwa na wazungu.Uhuru upi unataka?ndoa ya jinsia moja?kutembea uchi?
Ukoloni/ubeberu/ ukaburu siyo rangi. Kwa miaka 5 tumekuwa chini ya beberu mweusi. Rangi yake ndo imewafanya baadhi yenu mshindwe kutambua?
 
1. Lissu anataka kuchochea tax base expansion kwa kuwa na friendly taxing environment

2. Pesa zinazokusanywa zipelekwe wapi, ni suala la vipaumbele (kupanga ni kuchagua).
Mathalani badala ya kutumia matrilioni kwa matrilioni kwa miaka 15 mizima kujenga SGR na Stiegler's Gorge ambavyo havina immediate impact katika kuchochea microeconomy, pesa hizo zitakuwa directed kwenye sekta zinazochoea ukuaji wa kasi wa microeconomies ambazo ni building blocks kuelekea kwenye uchumi mkubwa.

Model ya uchumi chini ya awamu hii itawafanya watoto wetu in the next 10 years waishie kuwa kama Waethiopia (kuikimbia nchi yao iliyosheheni midege lukuki na miundombinu mingi, vitu ambavyo havina immediate and direct trickle down effect).

3. Umeongelea double standard kwenye bomoa bomoa. Culprit number one kwenye hili ni hii serekali ya sasa ambayo iliwabomolea wakazi ambao hawakumpigia kura rais na waliompigia kura kutoguswa.

Yapo mengi.

So, yote aliyoystaja Tundu Lissu ni achievable 100% kwa kutumia internal resources. It's a question of where to prioritize, that's all!
 
Mkuu joint ventures na private partnership alizifanya Raisi Mkapa tukaambulia kapa.
Hata huu ukosefu wa ajira umetokana na ubinafshaji ulioletwa na Mkapa akauza kila kitu kwa bei poa,akaambulia mabua.
 
Tunaongelea "bodi ya mikopo endelevu" na sio elimu ya bure.
 
Karibu sana
 
Huyo ni mtoto hajui jinsi ambavyo TRC na ATC yalivyochoshwa na joint ventures
Mkuu joint ventures na private partnership alizifanya Raisi Mkapa tukaambulia kapa.
Hata huu ukosefu wa ajira umetokana na ubinafshaji ulioletwa na Mkapa akauza kila kitu kwa bei poa,akaambulia mabua.
 
Naunga mkono hoja.
 
mara juzi mkapost hapa kuwa Chadema hawana ilani, sasa hii unayozungumzia ni ya wapi> huu ni uwendawazimu
 
Kwa lahaja hii utakuwa mtu wa kule inshomile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…