Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, ilani yako na CHADEMA itahitaji msaada zaidi ya asilimia 90, tutarudi utumwani

[SUB] [/SUB]
Kwenye HESLB, bado toa maelezo kidogo, maana kabla ya 15% ilikuwa 7% nadhani bado watanzania walipa fursa ya kusoma CHADEMA wamesema itakuwa 3% aidha mbona serikali inatoa mikopo Yenye isiyokuwa na riba yaidi ni 3% service charge na 1% bima kwa watumishi unaiongeleaje hii maana nayo ni revolving fund chief?
 
Hao jamaa wakifuta kodi watajenga vipi miundombinu. Hao wanashabikia tu ila hali halisi sisi tunajua uku mtaani kukoje.

Maendeleo ya watu hayawezekani bila maendeleo ya vitu.

Chadema wamefeli. Mwaka 2015 walikuwa wana utashi wa kusikilizwa. Mwaka huu wamerudi hatua 10 nyuma.
 
Mngefanya jitihada za kupaka rangi ofisi za chadema kwanza tungejua kama mnaelewa maana ya kuboresha miundombinu
Sasa naona unaishiwa pumzi kwa kukosa hoja na kuingiza vijembe kitu kinachokufanya uonekane wa vijiweni kabisa. Kumbe huna maana kabisa.

You're just like any other cretin.
 
Kuna kitu kinaitwa Debt/GDP ratio, kwa Tanzania bado deni la Taifa ni himilivu kwani ratio ipo chini ya asilimia 50.

Elewa,acha kupotoshwa bila maendeleo ya vitu (miundombinu) hakuna maendeleo ya watu
Hiyo hisabati ya darasa la saba tutolee hapa kawadanganye ccm wenzio mliwapakia kwenye malori na matrekta jana kuwapeleka Dodoma kwenye ile fiestra, himilifu kwa kiasi gani na bado mipango yote ya ccm inategemea mikopo. Lakini nyie si mnasema nchi hii ni tajiri? si mko uchumi wa kati nyie? Kwa nini deni la taifa linapaa kila siku? hebu fikiria an addition of other 5 years in power with this borrowing rate!!
 
Hivi Maandamano yameisha!?, na alichokisema jana kawe ni maandamano ya kudai haki kwa walioenguliwa au ndiyo ilani!? Wanatuchanganya wananchi.
 
Mkuu joint ventures na private partnership alizifanya Raisi Mkapa tukaambulia kapa.
Hata huu ukosefu wa ajira umetokana na ubinafshaji ulioletwa na Mkapa akauza kila kitu kwa bei poa,akaambulia mabua.

Uliyemquote kaongea mengi ya msingi, mbona umebeba sehemu tu ya maelezo yake?
 
Kwa wale tunaoelewa ni kwamba uchumi wetu uko pabaya kwa sababu inaonekana unakuwa kwa asilimia chini ya nne tu tukiachilia mbali zile takwimu za kughushi zitolewazo mara kwa mara na serikali.

Sasa Lissu anapoongelea kupunguza utitiri wa kodi ni katika kutaka kuukwamua huu uchumi uliyodorora yaani anaanzisha Economic Stimulus.

Huu utaratibu ambao Lissu anataka ku-adopt unatumika sana kwa nchi zile zenye watu wanaojitambua na tuliona wakifanya hivyo hata kwenye aftermath of the WW II na hata kwenye Economic Depression ya mwaka 2007-2008.

Sasa kwa wale watu "Boot Lickers" wenye upeo mdogo katika maswala ya uchumi hawawezi kuelewa hili kwani wao hoja yoyote inayotolewa na mpinzani wanaitazama ktk mtizamo finyu ili waweze kuikosoa kama walivyozoea.

Serikali hii ina matumizi mabaya sana ya pesa za umma ambazo matumizi yake hayaidhinishwi na bunge kiasi kwamba tukipata serikali yenye kuheshimu nidhamu ya pesa za umma (Fiscal Discipline), hayo anayoyazungumzia Lissu yanawezekana kabisa.
 
Tayari Ni watumwa, tuna deni la tshs53.tril. Ambako tumekopa kujenga sgr, utumwa upo tu utaendelea, lissu atatumia diplomasia ya uchumi kupunguza utumwa
 
Mambo ya msingi Kama haya Ni Mara chache Sana kuona maccm yanayajadili, yako bize kuchungulia mikutano ya cddm imejaza kiasi gani,
 
Idadi ya wanafunzi ilikuwa ndogo
 
Sera yao haitekelezeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…