Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Yaani wakishindwa mnasema wameibiwa,walishinda

Wakishinda mnasema tena hawajashinda.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Samahani wapinzani wa tz
Hivii mligetemea wabunge gani wa upinzani ambao wangeweza kuibuka kidedea?

Hai kashindwa kihalali
Arusha pia kashindwa kihalali
Mbeya nako kihalali
Tarime nako vilevile
Musoma hivo hivo
Sijui mikumi
Kawe
Kibamba hali ni ile ile
Kwa maana kama ni wizi umetendeka kwa kuonewa wapinzani
Vibe lingeanzia majimboni kwao
Lakn cha kushangaza watu wapo cool kwa maana wamelizka na matokeo hayo na ni halali kabisaaa

Sasa kwanini mlipanga kuja kulinukisha jiji la Dar ili hali sio jimbo lenu?'
Halafu mlijionea wenyewe kabisa kwenye kampeni za Mh TAL jinsi raia wa Dar es salaam hawana time naye?
Acheni lawama zisizo kuwa na mashiko.kabisa
Maana dalili ya mvua ni mawingu
Na imenyesha kweli kweli hadi mmeanza kutafta pa kujibanza kwa aibu

Hapakuwa na mbunge yeyote yule aliekuwa na uwezo wa kuingia bungeni uchaguzi huu 2020, kutoka upinzani na jinsi JPM alivojinadi kupitiankazi yake na hatimaye kuwabeba wagombea ubunge wake,

Na kila aliyejuwa amelitambua toka mapema kuwa 2020 akipata upenyo tu wa kupitishwa na NEC ya CCM lazima atatinga bungeni iwe jua iwe mvua na ndio maana watia nia walikuwa wengi kama nn kupitia CCM

hivyo CCM imejitahidi na kujibeba yenyew kama yenyew kuupata ushindi huu wa kishindo
 
Aibu hii kwa CDM waache huu ujinga wa kumnyanyapaa Aida eti asiende bungeni
 
Kweli kabisa ,hata mm nimewashangaa , nimeamini Chadema Ni wabinafsi, hata huruma nao Kwa walichofanyiwa inaanza kuniondoka

Wanamuonea wivu Aida sababu wao wamekosa , Je Mbowe angeshinda wangesusa ?
Hata Mimi nawaza
Hivi huyo lisu angeshinda,halafu wabunge na madiwani wake wote washindwe..je angekubali kuachia nafasi?

Wanaiponda CCM kuwa wabinafsi huku wao ni wabinafsi wa kwanza.
Kweli nyani haoni kundule[emoji1787]
 
Aibu hii kwa CDM waache huu ujinga wa kumnyanyapaa Aida eti asiende bungeni
CHADEMA ni wabinafsi sana...
Yaani cha ajabu huwa wanaona ubinafsi wa CCM tu ila wao hawajioni[emoji1787]

Wanahubiri na kulaani ufujaji mali huku wao tu rukuzu yao wanakula wachache

Na ni chama kinachotaka tukipe dola.
Mi ntakuja kushabikia upinzani unaojielewa ila si huu wa kijinga na kibinafsi.
 
Hiki ni nini
 

Attachments

  • 123771577_998398397337436_8536500735324451822_n.mp4
    1,020.6 KB
Yaani Lissu hakuibiwa kura hata zero ukweli ni kuwa watanzania wengi waliona kazi nzuri ya JPM ,,yaani Lissu kuwaza kumshinda JPM ilikuwa ni zaidi ya maigizo
 
Wamezidi ubinafsi kwanini ushindi wa Aida wamwambie asiende bungeni kisa wao hawajashinda, mbona mbowe, lisu na wengine walioshinda walienda bungeni Ina maana walishinda chini ya tume tofauti na hii. Nadhani CDM Wana kimfumo dume Cha kijinga na hawaheshimu wanawake in short wanadharau hapo wanataka kuwanyima Hadi viti maalumu ambavyo viko kikatiba kabisa na ni swala la kidunia.
CDM kwa hii tabia ya kumsema Aida imeonyesha Hawa watu Ni wabinafsi Sana na hawafai
 
Ndio hawataki sasa, wanasema uchaguzi batili, lkn mmekuwa mkisema ni batili since kitambo, mbona hamkususia ubunge wenu, hadi leo hii mmekosa ndio mwenzenu naye akose.
Ubinafsi tu
 
Wao 2015 walienda bungeni
Hawakutaka kuwaunga mkono wenzao waliokosa kwa kuachia nafasi zao za Ubunge.
Hawakutaka kukosa wote.

Sasahivi zamu yao kukosa wanataka wenzao wawaunge mkono kwa kuachia nafasi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wanataka wakose wote
Tume ni ile ile [emoji1787]
CHADEMA hovyo kabisa.

Sema huyo dada ana akili.
 

Not with constitution and Electoral comitee. This shameful and horrible election result, caused by our poor and outdated constitution fullstop.
 

Hilo bunge ni rubber stamp ya serikali, ujadili usijadili kila kitu serikali itafanya kibabe. Huko bungeni kumebaki kituo cha kulia fedha za wananchi kisheria na sio kihalali.
 
Leo yamewakuta then wanasema tume si huru wenzao wakilalamika kuibiwa waliweka pamba maskioni hawaskii Ila baada ya kukosa wanataka wote wasiende, hicho ni kiwango Cha juu Sana Cha ubinafsi, tena wanaume wanalazimisha Aida na viti maalumu wasiende bungeni so selfish na aibu wallah, waache ubinafsi bwana
 
Hilo bunge ni rubber stamp ya serikali, ujadili usijadili kila kitu serikali itafanya kibabe. Huko bungeni kumebaki kituo cha kulia fedha za wananchi kisheria na sio kihalali.
Nakuuliza hao unao waita wenye akili bunge lililopita walijadili nini Cha maana?
 
Nakuuliza hao unao waita wenye akili bunge lililopita walijadili nini Cha maana?
Ni kipi cha maana kilichojadiliwa bunge lililopita? Labda tuanzie hapo kwanza.
 
Kabisa mkuu,CHADEMA waache hizo
 
Ha Hakuna mtu aliyeibiwa kma wameibiwa wapeleke ushahidi mahakamani, maana wanavyo vielelezo,
Na mahakimu waliandaliwa mapema ilinwatoe haki haraka kwa wale watakao lalamika.

Wanajua wamepigwa kihalali ndo maana wanataka wengine nao waumie kwa upuuzi wao.
 
Ni kipi cha maana kilichojadiliwa bunge lililopita? Labda tuanzie hapo kwanza.
Walichojadili bungeni ndio kiliwafanya watu wachague ccm, wakati wale wazee wa akili kubwa wakitoka bungeni na kususia vikao ndipo wenzao wakapitisha budget.

Bora wasiwemo kabisa Mana watakuwa wanalipwa mishahara ya bure huku bungeni hawakai kazi yao ni kulewa tu hadi wanaporomoka ovyo kwenye ngazi wanavunjika miguu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…