Nakumbuka Rais MOHAMEDI BUHARI wa NIGERIA alipokuwa mgonjwa mambo yaliwekwa hadharani kwa taifa na wananchi wake. BUHARI alikwenda UINGEREZA kwa matibabu kwa kipindi cha miezi sita.
Nashangaa hapa kwetu TZ kiongozi akiugua eti inakuwa "TOP SECRET" kwa nini?, Kuna shida gani? Miaka sitini ya kujitawala bado viongozi wetu hawajiamini, kuugua au kufariki kwa viongozi?
Kipindi cha msiba wa aliyekuwa Rais wetu JPM, wananchi hatukupewa taarifa yoyote ya kuugua kwake,na ghafla tukatangaziwa kifo chake, lilikuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha.
Hali kama hii inatia mashaka na sintofahamu juu ya mustakabali wa maisha, maradhi na vifo vya viongozi wetu wa ki taifa.
Rai yangu ni kwamba; seikali iwe inaweka wazi mwenendo wa ki maisha ya viongozi wa wetu ngazi ya kitaifa kwa sababu zifuatazo;
I.Viongozi ni waajiriwa wa wananchi kupitia sanduku la kura, na wanalipwa kutokana na kodi za wananchi.
II. Kuwaondolea wananchi wasiwasi kuhusu viongozi wao kutendewa ndivyo sivyo.
III.Kuwapa wananchi fursa ya kuwaombea viongozi wao kwa imani zao tofauti.
IV. Kuliweka taifa IMARA kwa hali yoyote itakayojitokeza.
Ikumbukwe kuwa, kila chenye uhai; Huzaliwa, Huishi na hatimaye Hufa.