Tundu Lissu: Kifo au ugonjwa wa kiongozi yeyote haufichiki. Tuambieni alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Tundu Lissu: Kifo au ugonjwa wa kiongozi yeyote haufichiki. Tuambieni alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Kuweka taifa zima kwenye suspense ni ushetani usiozungumzika.Yule ni kiongozi mkubwa sana. Familia haiwezi zungumza,marafiki na viongozi wa dini,serikali na mataifa aliohusiana nao nao wanapitia wakati mgumu. Crisis management ni ngumu hivi nchi hii? Msitupe vijisababu vya tunajipanga tunajipanga,you make this seem planned au ndio mnasubiria mpango ukamilike mnatuandaa kisaikolojia? Inaumiza sana.
 
Watu waliugua hadi korona na taarifa wananchi tulipata mzee wa msoga aliugua tezi dume na taarifa tulipewa lakini hili la Mzee mpango hakina kuna jambo la aibu lakini muda ndiye mwalimu wa kweli
 
Tundu Lissu kupitia akaunti binafsi ya mtandao wa X ameandika,

'Hivi Serikali hii ilijifunza chochote juu ya kifo cha Magufuli mwaka juzi? Kifo au ugonjwa wa kiongozi mkuu wa nchi havifichiki! Kufichaficha kunaleta hisia mbaya za mchezo mchafu dhidi yake. Jisafisheni! Tuambieni aliko Makamu wa Rais Phillip Mpango sasa!'

Pia soma > Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Makamu wa Rais, Philip Mpango yuko nje kwa majukumu
FB_IMG_1701962139076.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka Rais MOHAMEDI BUHARI wa NIGERIA alipokuwa mgonjwa mambo yaliwekwa hadharani kwa taifa na wananchi wake. BUHARI alikwenda UINGEREZA kwa matibabu kwa kipindi cha miezi sita.

Nashangaa hapa kwetu TZ kiongozi akiugua eti inakuwa "TOP SECRET" kwa nini?, Kuna shida gani? Miaka sitini ya kujitawala bado viongozi wetu hawajiamini, kuugua au kufariki kwa viongozi?

Kipindi cha msiba wa aliyekuwa Rais wetu JPM, wananchi hatukupewa taarifa yoyote ya kuugua kwake,na ghafla tukatangaziwa kifo chake, lilikuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha.

Hali kama hii inatia mashaka na sintofahamu juu ya mustakabali wa maisha, maradhi na vifo vya viongozi wetu wa ki taifa.

Rai yangu ni kwamba; seikali iwe inaweka wazi mwenendo wa ki maisha ya viongozi wa wetu ngazi ya kitaifa kwa sababu zifuatazo;

I.Viongozi ni waajiriwa wa wananchi kupitia sanduku la kura, na wanalipwa kutokana na kodi za wananchi.

II. Kuwaondolea wananchi wasiwasi kuhusu viongozi wao kutendewa ndivyo sivyo.

III.Kuwapa wananchi fursa ya kuwaombea viongozi wao kwa imani zao tofauti.

IV. Kuliweka taifa IMARA kwa hali yoyote itakayojitokeza.

Ikumbukwe kuwa, kila chenye uhai; Huzaliwa, Huishi na hatimaye Hufa.
Ukiona wanaficha ujue wamemdhuru wenyewe nafsi zinawasuta. Binadamu kuugua siyo dhambi wala jambo la aibu,kwa nini wafiche? WAMEMDHURU WENYEWE.
 
Tundu Lissu kupitia akaunti binafsi ya mtandao wa X ameandika,

'Hivi Serikali hii ilijifunza chochote juu ya kifo cha Magufuli mwaka juzi? Kifo au ugonjwa wa kiongozi mkuu wa nchi havifichiki! Kufichaficha kunaleta hisia mbaya za mchezo mchafu dhidi yake. Jisafisheni! Tuambieni aliko Makamu wa Rais Phillip Mpango sasa!'

Pia soma > Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Makamu wa Rais, Philip Mpango yuko nje kwa majukumu
Washasahau ajenda ya bandari
 
Kufuatia kuhoji kwake, maana yake yeye TAL ashajua mbivu na mbichi!!
Ana detail zote kuhusu makamu wa Rais!!
[emoji26][emoji26]
 
Back
Top Bottom