Tundu Lissu: Kifo au ugonjwa wa kiongozi yeyote haufichiki. Tuambieni alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Tundu Lissu: Kifo au ugonjwa wa kiongozi yeyote haufichiki. Tuambieni alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Utawala wa Kimafya wa Sirikali Kuna kitu tunafichwa na Serikali lakini baadae tutakuja kuelewa kuna mchezo mbaya unatendeka hapo. Picha ya kutisha bado ina endelea tunaingojea mwisho wake itakuwaje? Nchi yetu haina amani kwa Raia wake mpaka viongozi wake. Kuna watu wachache wabaya aidha wapo ndani ya Serikali ya mama wetu au hawapo ndani ya Serikali ndio wanaofanya huo mchezo mbaya tungojee matokeo yake yatakuwaje?
Na kwanini vifo viwe vya wakristo peke yake? Kuna nini hapo je waislam wana agenda ya kujitwalia dola au
 
Huwa sionagi faida serikali inapata kwa kukaa na tarifa mhimu ziwahusuzo viongozi kwa faida ya wananchi wao

Nchi hii ya watu wapooole kiasi hata uwapitishie unyasi jichoni wanacheka, mtu unaogopa kutoa tarifa za kiongozi wao iwe ni mgonjwa ama Mungu kampenda zaidi

Basi viongozi wetu wao ndio waoga wa kuondolewa madarakani, yawezekana wanajua kuwa hawana jema kwa wananchi wao, wanaogopa kutolewa Ikulu na ndiyo maana mambo kama haya uakitokea, hukaa na kujiandaa saaana kwa hofu ya kufurushwa
 
Utawala wa Kimafya wa Sirikali Kuna kitu tunafichwa na Serikali lakini baadae tutakuja kuelewa kuna mchezo mbaya unatendeka hapo. Picha ya kutisha bado ina endelea tunaingojea mwisho wake itakuwaje? Nchi yetu haina amani kwa Raia wake mpaka viongozi wake. Kuna watu wachache wabaya aidha wapo ndani ya Serikali ya mama wetu au hawapo ndani ya Serikali ndio wanaofanya huo mchezo mbaya tungojee matokeo yake yatakuwaje?
Duh 🙄 !
 
unapoficha kifo cha mtu maana yake kuna walakini juu ya kifo chake.hii inalte taharuki kubwa .yani maana yake kifo kimepangwa au ? why ufiche? watu wanasababisha mwaswali yasikuwa na maana.
if someone is sick that is natural .why ufiche then uje kutuambia eti bahati mbaya amekufa .it is not fair at all for the public interest and for spiritual interest. watu watakuona muongo na kuona wewe unahusika na kifo chake kumbe siyo kweli.sasa kwa nini uwalazimishe watu kukuwazia isivyo?
 
Nakumbuka Rais MOHAMEDI BUHARI wa NIGERIA alipokuwa mgonjwa mambo yaliwekwa hadharani kwa taifa na wananchi wake. BUHARI alikwenda UINGEREZA kwa matibabu kwa kipindi cha miezi sita.

Nashangaa hapa kwetu TZ kiongozi akiugua eti inakuwa "TOP SECRET" kwa nini?, Kuna shida gani? Miaka sitini ya kujitawala bado viongozi wetu hawajiamini, kuugua au kufariki kwa viongozi?

Kipindi cha msiba wa aliyekuwa Rais wetu JPM, wananchi hatukupewa taarifa yoyote ya kuugua kwake,na ghafla tukatangaziwa kifo chake, lilikuwa ni jambo la kushangaza na kusikitisha.

Hali kama hii inatia mashaka na sintofahamu juu ya mustakabali wa maisha, maradhi na vifo vya viongozi wetu wa ki taifa.

Rai yangu ni kwamba; seikali iwe inaweka wazi mwenendo wa ki maisha ya viongozi wa wetu ngazi ya kitaifa kwa sababu zifuatazo;

I.Viongozi ni waajiriwa wa wananchi kupitia sanduku la kura, na wanalipwa kutokana na kodi za wananchi.

II. Kuwaondolea wananchi wasiwasi kuhusu viongozi wao kutendewa ndivyo sivyo.

III.Kuwapa wananchi fursa ya kuwaombea viongozi wao kwa imani zao tofauti.

IV. Kuliweka taifa IMARA kwa hali yoyote itakayojitokeza.


Ikumbukwe kuwa, kila chenye uhai; Huzaliwa, Huishi na hatimaye Hufa.
 
Binafsi sidhani kuwa Serikali ina nia ovu yo yote kuhusu kutoa au kutotoa taarifa iliyosahihi na iliyoyonyooka. Tatizo hapa ni viongozi kutojua kinachotakiwa kufanywa kwenye masuala haya katika Serikali inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Ni suala la kutokujua au kutenda Serikalini kwa mujibu wa utawala bora. Kama vile viongozi wetu kutoonesha kwa vitendo kuwa wao wameomba uongozi ili watumikie wananchi kwa hiyo wanawajibika kwa wananchi na hao wananchi wana haki ya kupewa taarifa sahihi kuhusu viongozi wao. Kwenye Usultani mambo ni tofauti.
 
Back
Top Bottom