Tundu Lissu kimataifa: Akutana na David Mcallister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashauri ya Kigeni ya Bunge la Ulaya

[emoji1787][emoji1787]Sasa David Mc Alister anahusika nini na SOVEREIGNTY ya Tanzania?!!!!!

Ujinga mwingine abaki nao huyu mzururaji anayetukuza WAZUNGU NA MAMBO YAO YOTE......

Mzungu alimtumia Saddam Hussein na Gaddafi na mwishowe wote ni mashuhuda kwa kilichotokea......Sasa Tundu Lissu atafika lini huko?!!!!

Dunia imejaa WANAHARAKATI.....maajabu hakuna.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Can you argue sensibly?
 
Hiyo CCM ni mali ya hao hao wazungu kupitia jamaa fulani pale Italy, wanapoona maslahi yao yanateteleka au kuna mtu anayabana na kuyahoji basi humtingisha kupitia the so called wapinzani wanaohitajo support kutoka kwao...

Mpaka pale tutakapoacha kutumia neno "upinzani", na kutumia neno "mbadala" ndipo tutakapokuwa vyama vyenye maono ya kweli kwa nchi zetu.
 
hii ndomana kila mama akikanyaga sehemu muhimu anakutana na Hali ngumu

Chadema international ni shida mwamba anaupiga kwelikweli
Hakuna anayejua nguvu ya TL zaidi ya marehemu Magufuli. Ni bahati mbaya kifo kilimwondoa mapema, wote mngeshuhudia jinsi ambavyo angeadhirika.

Milango ya Dunia kila siku ilikuwa inazidi kufungwa. Akabakia na frustrations za kila aina. Baada ya uchaguzi alikuwa amenyong'onyeshwa kabisa baada ya kuona hazina imekauka, na vyanzo vya mapato vikizidi kupotea.
 
Hakuna anayejua nguvu ya TL zaidi ya marehemu Magufuli. Ni bahati mbaya kifo kilimwonfoa mapema, wote mngeshuhudia jinsi ambavyo angeadhirika.

Milango ya Dunia kila siku ilikuwa inazidi kufungwa. Akabakia na frustrations za kila aina. Baada ya uchaguzi alikuwa amenyong'onyeshwa kabisa baada ya kuona hazina imekauka, na
vyanzo vya mapato vikizidi kupotea.

Kilicho fanywa milango kufungwa sio TL bali siasa zake dhidi ya mabeberu hasa kuwabana kwenye madini na gas.... mabeberu wanachojali ni maslahi yao haya mengine huwa ni tools za kurahisisha upatikanaji wa maslahi yao..
 
Mr belgiji kakenua meno utafikiri kamuona Mungu.

Hivi kinachofanya Lisu aendelee kukaa kwa beberu ni nini wakati mbaya wake alishakufa?
Marehemu alikuwa kiongozi mbaya, lakini mfumo aliouanzisha wa utawala ulikuwa mbaya zaidi. Mfumo ule japo umenyofolewa lakini haujafa.

Kwani huoni hata humu ndani kuwa bado kuna masalia? Hayo masalia ndiyo yaliyombambikia kesi Mbowe, na ndiyo yamemwua Lijenje. Ameondoka lakini mfumo ule wa uovu aliouanzisha, haujafa bado.

TL abakie huko huko kwaajili ya kuweka wazi maovu ya haya masalia.
 
Kilicho fanywa milango kufungwa sio TL bali siasa zake dhidi ya mabeberu hasa kuwabana kwenye madini na gas.... mabeberu wanachojali ni maslahi yao haya mengine huwa ni tools za kurahisisha upatikanaji wa maslahi yao..
Hizo habari za gas na madini ni ropaganda ambazo alizitengeneza marehemu kwaajili ya kuwaokota wasio na akili.

Ni mabeberu wa wapi walioathiriwa na masuala ya madini na gas?.

Kwenye dhahabu, mgogoro aliutengeneza marehemu dhidi ya Acacia. Kampuni ya Uingereza iliyokuwa na mwanahisa mkubwa Barrick, kampuni ya Canada.

Kwenye gas, hakuna kampuni iliyosimamishwa na serikali bali makampuni ya gas walipoona uongozi wa ovyo wa marehemu usiozingatia sheria, mikataba na katiba waliamua kusitisha mpango wao wa kufanya uwekezaji wa dola bilioni 30 katika ujenzi LNG, na kwenda kuwekeza Mozambique. Marehemu alituma ujumbe kuwabembeleza warudi, wakagoma.

Utawala wa marehemu ulitengwa zaidi na washirika wakuu wa maendeleo kama Germany, Finland, Dernmark, Sweeden, US na Japan. Hakuna kampuni ya madini toka kwenye mataifa haya iliyokuwa imewekeza kwenye sejta ya madini ya Tanzania.
 
Huwezi kuitoa CCM kwa kutegemea Wazungu ambao nao wanabenefit kwa CCM, kinachofuata watakutumia kuibana CCM kwa wao kupata maslahi zaidi... Nitajie nchi moja ambayo wazungu wameleta demokrasia na stabilization..

Wazungu walishindwa kuwasaidia weusi pale SA dhidi ya kaburu matokeo yake weusi wenyewe wakapambana kujikomboa huku wazungu wakipamban kimyakimya kusaidia kaburu..
Wazungu wakikutana na Samia,sifa zinakuwa kibao na vigelegele juu!Wapinzani wakikutana nao inakuwa nongwa na tunashuhudia vijembe vya namna hii!
Kama wazungu ni maadui wa mtu mweusi basi tutangaze hadharani kutoshirikiana nao na serikali ioneshe mfano!Kama sivyo basi tuufyate na kila mtu awe huru kushirikiana nao!
Sio tunawaita mabeberu kwenye mazingira haya,mazingira mengine tunawaita wadau!
 
Mfamaji lazima ajaribu kujiokoa,hao ndio chama chakavu.
 
Hizo habari za gas na madini ni ropaganda ambazo alizitengeneza marehemu kwaajili ya kuwaokota wasio na akili.

Ni mabeberu wa wapi walioathiriwa na masuala ya madini na gas?.

Kwenye dhahabu, mgogoro aliutengeneza marehemu dhidi ya Acacia. Kampuni ya Uingereza iliyokuwa na mwanahisa mkubwa Barrick, kampuni ya Canada.

Kwenye gas, hakuna kampuni iliyosimamishwa na serikali bali makampuni ya gas walipoona uongozi wa ovyo wa marehemu usiozingatia sheria, mikataba na katiba waliamua kusitisha mpango wao wa kufanya uwekezaji wa dola bilioni 30 katika ujenzi LNG, na kwenda kuwekeza Mozambique. Marehemu alituma ujumbe kuwabembeleza warudi, wakagoma.

Utawala wa marehemu ulitengwa zaidi na washirika wakuu wa maendeleo kama Germany, Finland, Dernmark, Sweeden, US na Japan. Hakuna kampuni ya madini toka kwenye mataifa haya iliyokuwa imewekeza kwenye sejta ya madini ya Tanzania.

Chief, hao watu wanapenda kula bila bughudha kitendo cha kuwaghasi na kuwaharibia image tayari kwao ni tatizo..

Kwenye investment zao hawapendi kuwa challenged, ukiwachallenge ndio shida inapoanzia...kuwachallenge haijalishi kivipi, iwe policy ya nchi, au chochote kile...wanataka mkae kimya wachimbe wawape watakacho hapo
uki challenge shida lazima itokee..

JPM aliwachallenge haijalishi alikuwa sahihi au sio lakini issue ni kuwachallenge hawataki...
 
Halafu tukishatandikana huko ndio CHADEMA imeingia ikulu?!!! Khaaa 😳😳
Wakati wa jpm chadema ilikuwa inaonekana kama takataka. Hata wakishinda mkurugenzi anaambiwa atangaze mwanaccm hivyo hivyo bila kujali ukifanya mikutano mkutano mzima unazungukwa na pilisi au mnapigwa mabomu tena riasi za moto. Sasa unaona viongozi wa kiafrika ni watu au mashetani. Si bora mzungu akutawale tu
 
Wazungu wakikutana na Samia,sifa zinakuwa kibao na vigelegele juu!Wapinzani wakikutana nao inakuwa nongwa na tunashuhudia vijembe vya namna hii!
Kama wazungu ni maadui wa mtu mweusi basi tutangaze hadharani kutoshirikiana nao na serikali ioneshe mfano!Kama sivyo basi tuufyate na kila mtu awe huru kushirikiana nao!
Sio tunawaita mabeberu kwenye mazingira haya,mazingira mengine tunawaita wadau!

Binafsi siwaamini kwenye pande zote, iwe kukutana na Samia au CDM...inapofika kuwaamini tu kwenye issue za Taifa letu tayari kwangu ni shida kwao....sijui wengine wanavyowaza....wapo kwa maslahi yao haijalishi wanakujaje...
 
Chief, hao watu wanapenda kula bila bughudha kitendo cha kuwaghasi na kuwaharibia image tayari kwao ni tatizo..

Kwenye investment zao hawapendi kuwa challenged, ukiwachallenge ndio shida inapoanzia...kuwachallenge haijalishi kivipi, iwe policy ya nchi, au chochote kile...wanataka mkae kimya wachimbe wawape watakacho hapo
uki challenge shida lazima itokee..

JPM aliwachallenge haijalishi alikuwa sahihi au sio lakini issue ni kuwachallenge hawataki...
Trilion 194 tulizipata?
 
Unaonaje sasa democrasia iliyopo Libya?

Nyie ndio mkimuona mzungu mnazuzuka kabisa

..Gaddafi alikuwa mjinga kutokuruhusu vyama vya siasa kuanzishwa Libya.

..Alitakiwa aige mfano wa Kenneth Kaunda wa Zambia ambaye walau aliruhusu vyama vya wafanyakazi ambavyo vilikuja kuwa mbadala wa chama tawala UNIP.

..Nchi yoyote ile lazima iwe na chama au vyama mbadala ili kuepusha nchi kusambaratika ikiwa wananchi watakuwa wamechoshwa na chama tawala.
 
..mabadiliko ya Afrika Kusini yalipatikana baada ya mabeberu kupunguza kwa kiwango kikubwa support yao kwa utawala wa makaburu.
Hapa tu Hangaya Asingepata Mkopo wa mabeberu 1.3T hata mshahara wa walimu angekosa. Ndio angejua dunia ikoje.

M7 na Pk hawawezi kusurvive hata Miezi mitatu bila sapoti ya Mabeberu
 
..Gaddafi alikuwa mjinga kutokuruhusu vyama vya siasa kuanzishwa Libya.

..Alitakiwa aige mfano wa Kenneth Kaunda wa Zambia ambaye walau aliruhusu vyama vya wafanyakazi ambavyo vilikuja kuwa mbadala wa chama tawala UNIP.

..Nchi yoyote ile lazima iwe na chama au vyama mbadala ili kuepusha nchi kusambaratika ikiwa wananchi watakuwa wamechoshwa na chama tawala.
Na hayo yaliyopo leo ni matokeo ya Upumbavu na Kibri chake Gaddafi
 
Kilicho fanywa milango kufungwa sio TL bali siasa zake dhidi ya mabeberu hasa kuwabana kwenye madini na gas.... mabeberu wanachojali ni maslahi yao haya mengine huwa ni tools za kurahisisha upatikanaji wa maslahi yao..
Kalale mtoto mdogo wewe
 
Back
Top Bottom