Hizo habari za gas na madini ni ropaganda ambazo alizitengeneza marehemu kwaajili ya kuwaokota wasio na akili.
Ni mabeberu wa wapi walioathiriwa na masuala ya madini na gas?.
Kwenye dhahabu, mgogoro aliutengeneza marehemu dhidi ya Acacia. Kampuni ya Uingereza iliyokuwa na mwanahisa mkubwa Barrick, kampuni ya Canada.
Kwenye gas, hakuna kampuni iliyosimamishwa na serikali bali makampuni ya gas walipoona uongozi wa ovyo wa marehemu usiozingatia sheria, mikataba na katiba waliamua kusitisha mpango wao wa kufanya uwekezaji wa dola bilioni 30 katika ujenzi LNG, na kwenda kuwekeza Mozambique. Marehemu alituma ujumbe kuwabembeleza warudi, wakagoma.
Utawala wa marehemu ulitengwa zaidi na washirika wakuu wa maendeleo kama Germany, Finland, Dernmark, Sweeden, US na Japan. Hakuna kampuni ya madini toka kwenye mataifa haya iliyokuwa imewekeza kwenye sejta ya madini ya Tanzania.