Tundu Lissu: Kisasi changu kitalipwa na Mungu

Tundu Lissu: Kisasi changu kitalipwa na Mungu

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Antipass Lissu amesema kisasi chake kitalipwa na Mwenyezi Mungu na si vinginevyo.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya Wananchi wa Kijiji chake Ikungi Singida Mashariki hapo Jana Tundu Lissu aliwaambia ndugu zake na watu wa Damu yake kulipa kisasi kwa Yale yaliyompata kamwe si agenda yake kwa Sasa.

Lissu alisema katika kipindi cha wiki mbili za mwanzo akiwa matibabuni nchini Kenya tangu apigwe risasi alikuwa anasikia maumivu makubwa kila mahali katika mwili wake kiasi kwamba ni vigumu kwa mwanadamu kuweza kuhimili.

Huku watu wakiangua kilio cha majonzi na matumaini Lissu alisema kwa mateso yale aliyopata hatamani mwadamu mwingine yeyote aliyezaliwa na mwanamke kupitia mateso yale tena.

Lissu amewaambia wananchi hao kwamba kuna watu wana hofu ya kulipiziwa kisasi pale atakapoapishwa kuwa Rais. Amesema watu hao wote waondoe hofu wakae na Amani ya Bwana.

Lissu amesema baada ya mateso yale kila kitu alikabidhi kwa Mwenyezi Mungu kwani kamwe hakuponywa na Mwanadamu bali Mungu.

Lissu amesema kisasi chake kitalipwa na Mungu kwa njia atakayoona Inafaa.

Umati huo uliitikia maneno hayo mazito kwa kutamka maneno "Amina" kama ishara ya kusema na Iwe hivyo.

Lissu Jana alipokewa kijijini kwake huko Ikungi Singida kwa kulakiwa na umati mkubwa wa watu kuwahi kushuhudiwa eneo hilo tangu Tanzania ipate Uhuru.

Kutokana na hali halisi inavyoonekana mpaka sasa mgombea huyo wa Chadema ana uwezekano mkubwa wa kushinda nafasi hiyo ya Urais kutokana na kuungwa mkono na wananchi walio wengi.
 
Njia aliyoipitia Tundu Lisu na mateso aliyoyapitia, hakuna ajuaye, zaidi ya Yeye na Mungu wa Kweli tunayemwabudu.

Hapo zamani kila upatanisho au mkataba ulifungwa kwa damu. Na baadaye Masihi wetu akaitoa damu yake kwaajili ya wote, ili yeye awe wa mwisho kwenye kutoa sadaka ya damu.

Lakini shetani amelazimisha umwagaji damu uendelee kuwa njia ya kuwakomboa wanadamu.

Tulikuwa kwenye utumwa wa mtu mweupe, tukapambana mpaka tukapata uhuru wa bendera. Taratibu tumerudishwa utumwani. Watu hawaruhusiwi kufikiri, kupinga, kukosoa, kujadili, kuamua na kupanga. Mambo yote yapangwe na mtu mmoja asiyehojiwa! Huu ni ukoloni mbaya kuliko ule wa Mwingereza ambaye aliwapa nafasi machifu kuamua baadhi ya mambo kwenye maeneo yao.

Wakati wa kupigania uhuru, watu hawakuongelea uchumi. Maana uchumi kwa mtumwa hauna maana. Watu walipigania uhuru. Na safari hii tutapigia uhuru wetu wa mawazo, wa kukosoa, kuamua, kuhoji na hata kukataa, ikilazimu.
 
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Antipass Lissu amesema kisasi chake kitalipwa na Mwenyezi Mungu na si vinginevyo.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya Wananchi wa Kijiji chake Ikungi Singida Mashariki hapo Jana Tundu Lissu aliwaambia ndugu zake na watu wa Damu yake kulipa kisasi kwa Yale yaliyompata kamwe si agenda yake kwa Sasa...


Jr[emoji769]
 
Imagine aliyetoa go ahead dhidi ya shambulio ya Lisu Tundu akisikia haya maneno. Ila kuna watu roho zao zinateseka japo tunawaona wanatembea mwili ukiwa mzima.
Umenena vema sana
 
Mungu aendelee kuweka mkono wake kwa ulinzi wako maana aliruhusu upone ili uje useme hii habari njema ya msamaha maana yeye ndie muweza wa yote na utakuwa raisi maana watanzania wanachotaka ni matumaini mapya baraka za bwanaziwe juuya kichwa chako na muujizaukaende kutimilika.
 
Back
Top Bottom