Njia aliyoipitia Tundu Lisu na mateso aliyoyapitia, hakuna ajuaye, zaidi ya Yeye na Mungu wa Kweli tunayemwabudu.
Hapo zamani kila upatanisho au mkataba ulifungwa kwa damu. Na baadaye Masihi wetu akaitoa damu yake kwaajili ya wote, ili yeye awe wa mwisho kwenye kutoa sadaka ya damu.
Lakini shetani amelazimisha umwagaji damu uendelee kuwa njia ya kuwakomboa wanadamu.
Tulikuwa kwenye utumwa wa mtu mweupe, tukapambana mpaka tukapata uhuru wa bendera. Taratibu tumerudishwa utumwani. Watu hawaruhusiwi kufikiri, kupinga, kukosoa, kujadili, kuamua na kupanga. Mambo yote yapangwe na mtu mmoja asiyehojiwa! Huu ni ukoloni mbaya kuliko ule wa Mwingereza ambaye aliwapa nafasi machifu kuamua baadhi ya mambo kwenye maeneo yao.
Wakati wa kupigania uhuru, watu hawakuongelea uchumi. Maana uchumi kwa mtumwa hauna maana. Watu walipigania uhuru. Na safari hii tutapigia uhuru wetu wa mawazo, wa kukosoa, kuamua, kuhoji na hata kukataa, ikilazimu.