Tundu Lissu: Kufa kwa Magufuli ni 'Poetic Justice'

Tundu Lissu: Kufa kwa Magufuli ni 'Poetic Justice'

Kikomo cha kukosa ustaarabu ni kushangilia kifo cha kiumbe mwenzako hasa binadamu hata kama amekukosea kiasi gani. Alipofariki JPM makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu alikiita kifo cha JPM a poetic justice (a fitting or deserved retribution for one's actions).

Tunaamini huu pia ndio msimamo wa CHADEMA kwani hawajawahi kujitenga nao. Kwa vile sasa tuko kwenye maridhiano ni bora CHADEMA mliweke hili wazi na mna fursa hiyo 21.01.2023 kwenye mkutano wenu wa hadhara Mwanza na kanda ya ziwa- kanda ya kwao na JPM.
162033367_1330017047375929_831188534219967358_n.jpg
Unahangaika na mambo ya kawaida kabisa duniani. Kila mtu akifa wapo watakaofurahia na wapo watakaohuzunika na wengine hawatakuwa na hisia yeyote wakiona kuwa ni kawaida. Hata huko CCM kuna watu kibao tu walifurahia mioyoni na wengine wameshindwa kujizuia wameweza kuonyesha hisoa zao hadharani kwa namna moja au nyingine. Hayo maridhiano tayari yanathibitisha kuwa kulikuwa na tatizo ..... wenzako wameshakubali!!
 
Kikomo cha kukosa ustaarabu ni kushangilia kifo cha kiumbe mwenzako hasa binadamu hata kama amekukosea kiasi gani. Alipofariki JPM makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu alikiita kifo cha JPM a poetic justice (a fitting or deserved retribution for one's actions).

Tunaamini huu pia ndio msimamo wa CHADEMA kwani hawajawahi kujitenga nao. Kwa vile sasa tuko kwenye maridhiano ni bora CHADEMA mliweke hili wazi na mna fursa hiyo 21.01.2023 kwenye mkutano wenu wa hadhara Mwanza na kanda ya ziwa- kanda ya kwao na JPM.
162033367_1330017047375929_831188534219967358_n.jpg
Pia ni mzuri katika kipindi hiki cha maridhiano nanyi muombe msamaha kwa viroba vyote na kwa watu wote mliowateketeza wakati wa mwendazake
 
Lissu anayo haki ya kusema hivyo Kwani yeye anaamini kuwa chanzo cha yeye kutaka kuuawa ni Magufuli, ikumbukwe binadamu amezaliwa na roho ya kisasi hivyo kifo cha JPM kwake Lissu ni faraja na anguko la adui zetu ni faraja kwetu.

Hata Mimi kuna baba ndogo tunaendesha naye kesi anang'ang'ania nyumba ya baba yetu, kwangu Mimi huyu ni adui, nikisikia Leo hii kafa, wallah lazima nichinje mbuzi na kukesha baa nikikunywa bia, kwangu Mimi huyu baba ndogo ni adui yangu kifo chake furaha kwangu.

Maisha ndio yalivyo hapa dunia, mwacheni aseme ya moyoni
Huyo tayari keshatumbukia kwenye mtego!!! Kuna mambo binafsi na unapoamua kuwa kiongozi wa Chama kunakuwa na mambo ya Chama!

Keshajikaanga huyo...

CCM baba lao la Siasa....CCM wataibuka kumkemea Lissu ha ha haaa
 
Tundu Lissu itachukua muda sana kugundua watu gani walihusika kushambuliwa kwake, kuna siku atakuja muomba msamaha Hayati JPM.
Hahahha.. Nijichekee kwanza.
Amuombe msamaha kwa kutoonesha any sympathetic action kwenye hilo sakata? Na kuzuia asiruhusiwe kutibiwa nje ama?
 
Ba
Kikomo cha kukosa ustaarabu ni kushangilia kifo cha kiumbe mwenzako hasa binadamu hata kama amekukosea kiasi gani. Alipofariki JPM makamu mwenyekiti taifa wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu alikiita kifo cha JPM a poetic justice (a fitting or deserved retribution for one's actions).

Tunaamini huu pia ndio msimamo wa CHADEMA kwani hawajawahi kujitenga nao. Kwa vile sasa tuko kwenye maridhiano ni bora CHADEMA mliweke hili wazi na mna fursa hiyo 21.01.2023 kwenye mkutano wenu wa hadhara Mwanza na kanda ya ziwa- kanda ya kwao na JPM.
162033367_1330017047375929_831188534219967358_n.jpg
bado mnapambana na Tundu Lissu tu?
 
Unatoaje maoni kwenye kifo?! Ukitaka kujua hebu fikiria kila kwenye maziko ya waislam hutolewa tangazo la nani ana mdai marehemu- ulishaona watu wanijitokeza? Unadhani ni ujinga au uoga?
Sasa unataka awe kama wewe? Aamini unachoamini wewe? Atende unachotaka wewe atende?

Haipo hivyo..!!

Tundu Lissu anabaki kuwa yeye na wewe na wengine huko mnabaki nyie hivyohivyo....

Hayo yanabaki kuwa ni maoni yake Lissu unless useme amevunja sheria fulani ya nchi hii...

Lakini kama amekukera wewe tu na machawa wenzako huko, basi huo utabaki kuwa ni ujinga wako tu mwenyewe na wenzako..!!
 
Mirija kukaba, inauma sana kwa waliozibiwa na faraja kwa walionyonywa kwa muda mrefu.

Hata Kifo cha Malikia Elizabeth, wa Ufalme wa Uingereza na kwingine ambayo iliwanyonya, kuwaua, kuwateka, kuwabaka, na kuwafanya utumwa Waafrika, Wahindi, Wachina, Wa NewZealand, Waboriji wa Australia na wengine wengi Duniani Alipokufa, It was a Poetic Justice.

When you offend god, you die.!
 
Mwaka 2016 mpaka 2020 Tanzania iligubikwa na makelele ya Tundu Lisu aloyejiona yeye tu ndiyo mwenye haki ya kumshauri rais wa nchi wa wakati huo na ni lazima ushauri wake ufuatwe!

Hata hivyo hayati Magufuli alisimama imara na kupuuza makelele yote ya wakala wa mabeberu Tundu Lisu.

Kama hayati raisi Magufuli asingekuwa imara na akasikiliza makelele ya Lisu, haya hapa yangetokea Tanzania.

1. Tanzania tusingekuwa na bwawa la kufua umeme ambalo ni moja ya mabwawa makubwa barani Afrika. Urefu wa bwawa la Nyerere ni km100 yani sawa na urefu wa kutoka Dar mpaka Chalinze.

Tundu Lisu kwa kutumiwa na mbabeberu kwa ahadi ya kumlisha yeye na familia yake pamoja na kumpa hifadhi Ubelgiji alipinga sana ujenzi wa bwawa hili kwa kisingizio kwamba litasababisha uharibifu wa mazingira na mvua hazitanyesha tena Tanzania!. Leo mwaka 2023 bwawa linajazwa maji na Tanzania imegubikwa na mafuriko kila sehemu kwani mvua zinanyesha sana kinyume na utabiri wa Tundu Lisu.

2. Tanzania isingekuwa na ujenzi wa SGR.
Tundu Lisu alipinga sana ujenzi wa reli hii ya umeme na yenye kasi zaidi Afrika yote.

3. Serikali isingehamia Dodoma.
Tundu Lisu na Mbowe walipinga sana serikali kuhamia Dodoma wakisema huko ni kutesa watumishi na kwamba serikali ibaki tu Dares salaam kwa ndoto za mwl Nyerere zimepotwa na wakati. Hayati Magufuli aliziba masikio na leo serikali yote ipo Dodoma.

4. Kampuni ya madini ya Acacia ingekuwepo.
Licha ya kwamba Lisu amesoma kwa kodi za watanzania lakini aligeuka kuwa mwanasheria wa Acacia na akasema ataisaidia kutushitaki MIGA, kama tukiendelea kuwadai hela za wizi wa makinikia. Hayati Magufuli aliendelea mbele hadi kampuni ya Acacia ikafutwa na kuzaliwa kampuni mpya ya Twiga ambayo watanzania wapo kwenye management na Tanzania yakafunguliwa masoko ya madini kila sehemu, na watanzania wakanufaika na madini yao.

5. Kenya na India zingeendelea kuongoza kwenye uuzaji wa madini ya Tanzanite .
Kutokana na ukweli madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. Hayati Magufuli alichukua hatua kali sana za kudhibiti madini ya Tanzanite ikiwemo kujenga ukuta wa kuzunguka mgodi huo, hatua hizo zilipingwa mno na Lissu na akaita ni udikteta mkubwa kufanya hivyo
Ujinga pia ni mzigo, jitahidi kuutua!

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
You are quite right. Muuaji hata mtaani watu wakipata nafasi wanawachoma moto, sasa wanatofautiana nini na huyo aliyekuwa anatumia ofisi kuua?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Binafamu afanye makosa mengine yote, anaweza kusamehewa lakini siyo uuaji. Huyo bwana, alipofikia kuua watu, nilipata uhakika kuwa Taifa lipo chini ya utawala wa shetani.

Tunashukuru kwa watu wa Mungu, walioomba usiku na mchana, na leo tupo katika mazingira ambayo uhai wa binadamu umepata thamani tena.
 
Binafamu afanye makosa mengine yote, anaweza kusamehewa lakini siyo uuaji. Huyo bwana, alipofikia kuua watu, nilipata uhakika kuwa Taifa lipo chini ya utawala wa shetani.

Tunashukuru kwa watu wa Mungu, walioomba usiku na mchana, na leo tupo katika mazingira ambayo uhai wa binadamu umepata thamani tena
wewe ni nani unaejua dhambi ya uuaji haisamehewi????? ila binadamu mna shida sana ya kujitolea hukumu msizozijua
 
Back
Top Bottom