Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kujizolea zaidi ya kura milioni 16.7, ni za wanavyuo vikuu, graduates na wafanya kazi

Hakika mambo yanazidi kunoga. Wakati uko upande wa Lissu. Namba pia ziko upande wake. Lissu amejipambanua kuwa mkombozi wa Wanavyuo vikuu, waliomaliza vyuo vikuu na wafanya kazi kwani anania ya dhati ya kuwakomboa makundi haya muhimu ktk taifa letu.

Akitangaza nia ya kugombea Kiti cha urais mwanzoni mwa July 2020 kupitia bendera ya upinzani ameeleza kuwa anatambua maumivu, mateso, umasikini na kero zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano. Taarifa zinaonesha kitakwimu kuanzia 2000 hadi 2018 zaidi ya wanafunzi 16.7M wamemaliza vyuo. Hawa ni kundi la wanamabadiliko. Wanaounga mkono sera za maendeleo wanaopenda uhuru na siasa safi.

1. Serikali imeamua kuwanyonga na kuwakamu mpaka damu graduates ( waliomaliza vyuo vikuu) kwa kutunga sheria mbovu za makato ya mikopo asilimia 15 kinyume cha sheria iliyokuwepo kwenye mkataba cha asilimia 8 tu. Hali hii iliyotetewa na wabunge wa CCM huku bunge likiwa gizani imeleta umaskini badala ya kuboresha maisha ya wahitimu hawa mara wanapoajiriwa au kujiajiri badala ya kuleta nafuu.

Imefika mahali mwajiriwa anaona bora asipate ajira afanye udalali au hata umachinga tu.

Mfano ni kijana mmoja nimekutana naye kwenye ofsi za bodi ya mikopo aliyesomea nchini China. Baada ya kupata ajira mshahara wake yaani gross salary ni 1.2M baada ya makato ya kodi za kikoloni na 15% ya Bodi ya mikopo anabakiwa tu na laki sita. Hali ni tete

2. swala la ajira limekuwa mtihani mkubwa na sintofahamu. Waliomaliza wanasugua visigino huku hakuna taasisi inayotoa mikopo nafuu ili wajiajiri kirahisi .walioko vyuoni hawaoni future yao maana wanaona kaka zao na dada zao wanavyohaha mtaani

Kundi hili kubwa litapata nafuu tu litakapomchagua kiongozi sio tu mwenye uchungu na maisha ya watanzania bali pia yeye mwenyewe ni mhanga wa uchumi mbovu uliosababishwa na serikali ya Rais Magufuli.

Hima hima wanavyo, wafanya kazi twende na Lissu Mzalendo wa Kweli.

Upinzani tunajua hakuna kama Lissu kwa muda huu. Tupeni haki yetu kwa kutuletea Mgombea mwenye sifa, uwezo na weledi wa kutuongoza. Kama Mgombea siyo Lissu hatutaki kusikia akina Membe? Nyalandu wala Lipumba. Ni bora tubaki na huyu huyu mvurugaji tutamzoea hivyo hivyo.

Asalam aleykum.
Atakayebisha yoyote yule basi hana akili au akili zake ni kama za mbuzi tena beberu
 
Mkuu mbona umetujumuisha wanavyuo wote? Sie wengine tunajielewa hivyo tunaweza kuchanganua mambo.

ebu nipe sababu kuntu ni kwann raisi wako haongezi mishahara ya watumishi?na kwann haajiri wahitimu wa vyuo vikuu kama ilivokuwa kwa kikwete JM?ukichanganua hilo ntajua kweli unajielewa
 
Acha zako wewe!!! Tundu mwenyewe midomo imejaa matusi tu!! Labda akaongoze genge la wahuni huko!!!

Alway graduates tunajua nini tunafanya ondoa hiyo generalization yako!!
Mkuu usiwasemee graduates wenzako jisemee wewe kama wewe,,,mbona mm n graduate lakin nipo kinyume nawewe
 
Hakika mambo yanazidi kunoga. Wakati uko upande wa Lissu. Namba pia ziko upande wake. Lissu amejipambanua kuwa mkombozi wa Wanavyuo vikuu, waliomaliza vyuo vikuu na wafanya kazi kwani anania ya dhati ya kuwakomboa makundi haya muhimu ktk taifa letu.

Akitangaza nia ya kugombea Kiti cha urais mwanzoni mwa July 2020 kupitia bendera ya upinzani ameeleza kuwa anatambua maumivu, mateso, umasikini na kero zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano. Taarifa zinaonesha kitakwimu kuanzia 2000 hadi 2018 zaidi ya wanafunzi 16.7M wamemaliza vyuo. Hawa ni kundi la wanamabadiliko. Wanaounga mkono sera za maendeleo wanaopenda uhuru na siasa safi.

1. Serikali imeamua kuwanyonga na kuwakamu mpaka damu graduates ( waliomaliza vyuo vikuu) kwa kutunga sheria mbovu za makato ya mikopo asilimia 15 kinyume cha sheria iliyokuwepo kwenye mkataba cha asilimia 8 tu. Hali hii iliyotetewa na wabunge wa CCM huku bunge likiwa gizani imeleta umaskini badala ya kuboresha maisha ya wahitimu hawa mara wanapoajiriwa au kujiajiri badala ya kuleta nafuu.

Imefika mahali mwajiriwa anaona bora asipate ajira afanye udalali au hata umachinga tu.

Mfano ni kijana mmoja nimekutana naye kwenye ofsi za bodi ya mikopo aliyesomea nchini China. Baada ya kupata ajira mshahara wake yaani gross salary ni 1.2M baada ya makato ya kodi za kikoloni na 15% ya Bodi ya mikopo anabakiwa tu na laki sita. Hali ni tete

2. swala la ajira limekuwa mtihani mkubwa na sintofahamu. Waliomaliza wanasugua visigino huku hakuna taasisi inayotoa mikopo nafuu ili wajiajiri kirahisi .walioko vyuoni hawaoni future yao maana wanaona kaka zao na dada zao wanavyohaha mtaani

Kundi hili kubwa litapata nafuu tu litakapomchagua kiongozi sio tu mwenye uchungu na maisha ya watanzania bali pia yeye mwenyewe ni mhanga wa uchumi mbovu uliosababishwa na serikali ya Rais Magufuli.

Hima hima wanavyo, wafanya kazi twende na Lissu Mzalendo wa Kweli.

Upinzani tunajua hakuna kama Lissu kwa muda huu. Tupeni haki yetu kwa kutuletea Mgombea mwenye sifa, uwezo na weledi wa kutuongoza. Kama Mgombea siyo Lissu hatutaki kusikia akina Membe? Nyalandu wala Lipumba. Ni bora tubaki na huyu huyu mvurugaji tutamzoea hivyo hivyo.

Asalam aleykum.

UPUMBAVU NA UJINGA WA HAL IYA JUU KIWANGO CHA LAMI.
 
Nani kamjari mnyonge zaidi ya JPM hata upinzani mnajua hilo,

ubabe, jeuri na ukatili ni kwa wale wasiolitakia mema taifa wahujumu wa nchi na wasio tii sheria za nchi!!

Namwamini sana huyu jamaa JPM
anawajali wanyonge kvp,, akati kuna wanyonge kule mtwara wamekaa miaka miwili bila kulipwa pesa zao za korosho billion 23,,Leo hii uchaguzi unafika ndo mnaanza kuleta propaganda za kuwalipa wakulima wa korosho sh billion 20..aya hizo billion 3 zinazobaki atalipa lini au ndo mwasubiri uchaguz wa 2025...
 
Sema ACT wanatakiwa kuwaunga mkono CHADEMA
Shida n mzee Membe, amekuja kuwa kikwazo kwa wanaupinzani kwasabu. Membe amekuja upinzani na lengo la kugombea uraisi na saiz naona anataka kuwaconvice chadema waungane ili wamsimamishe yeye kwenye kiti cha uraisi
 
Hizo ni Hesabu za kilimo cha matikiti kutoka kwa Motivational speakers.
 
labda wanafunzi wa nje ya nchi, kwa research yangu ndogo baadhi ya vyuo mpaka sasa sjaona kelele zozote za lissu hata uyu membe ni nyie tu ndo mnamkuza uku mtandaoni
 
Back
Top Bottom