Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kujizolea zaidi ya kura milioni 16.7, ni za wanavyuo vikuu, graduates na wafanya kazi

Hakika mambo yanazidi kunoga. Wakati uko upande wa Lissu. Namba pia ziko upande wake. Lissu amejipambanua kuwa mkombozi wa Wanavyuo vikuu, waliomaliza vyuo vikuu na wafanya kazi kwani anania ya dhati ya kuwakomboa makundi haya muhimu ktk taifa letu.

Akitangaza nia ya kugombea Kiti cha urais mwanzoni mwa July 2020 kupitia bendera ya upinzani ameeleza kuwa anatambua maumivu, mateso, umasikini na kero zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano. Taarifa zinaonesha kitakwimu kuanzia 2000 hadi 2018 zaidi ya wanafunzi 16.7M wamemaliza vyuo. Hawa ni kundi la wanamabadiliko. Wanaounga mkono sera za maendeleo wanaopenda uhuru na siasa safi.

1. Serikali imeamua kuwanyonga na kuwakamu mpaka damu graduates ( waliomaliza vyuo vikuu) kwa kutunga sheria mbovu za makato ya mikopo asilimia 15 kinyume cha sheria iliyokuwepo kwenye mkataba cha asilimia 8 tu. Hali hii iliyotetewa na wabunge wa CCM huku bunge likiwa gizani imeleta umaskini badala ya kuboresha maisha ya wahitimu hawa mara wanapoajiriwa au kujiajiri badala ya kuleta nafuu.

Imefika mahali mwajiriwa anaona bora asipate ajira afanye udalali au hata umachinga tu.

Mfano ni kijana mmoja nimekutana naye kwenye ofsi za bodi ya mikopo aliyesomea nchini China. Baada ya kupata ajira mshahara wake yaani gross salary ni 1.2M baada ya makato ya kodi za kikoloni na 15% ya Bodi ya mikopo anabakiwa tu na laki sita. Hali ni tete

2. swala la ajira limekuwa mtihani mkubwa na sintofahamu. Waliomaliza wanasugua visigino huku hakuna taasisi inayotoa mikopo nafuu ili wajiajiri kirahisi .walioko vyuoni hawaoni future yao maana wanaona kaka zao na dada zao wanavyohaha mtaani

Kundi hili kubwa litapata nafuu tu litakapomchagua kiongozi sio tu mwenye uchungu na maisha ya watanzania bali pia yeye mwenyewe ni mhanga wa uchumi mbovu uliosababishwa na serikali ya Rais Magufuli.

Hima hima wanavyo, wafanya kazi twende na Lissu Mzalendo wa Kweli.

Upinzani tunajua hakuna kama Lissu kwa muda huu. Tupeni haki yetu kwa kutuletea Mgombea mwenye sifa, uwezo na weledi wa kutuongoza. Kama Mgombea siyo Lissu hatutaki kusikia akina Membe? Nyalandu wala Lipumba. Ni bora tubaki na huyu huyu mvurugaji tutamzoea hivyo hivyo.

Asalam aleykum.
Inapendeza sana na kuwa na maana kama utakuja na takwimu sahihi za waliomaliza vyuo kwa kipindi tajwa! Hiyo idadi hata waliomaliza darasa la saba hawafiki!
Tusipende kudanganya umma kwa takwimu za kupika tukiamini kila mmoja wetu hajui kimachoendelea na idadi ya watanzania wanaomaliza masomo ya vyuo mbalimbali nchini

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Lisu lofa mtihani wake wa Kwanza Ni kupitishwa na chadema Hana hell ya kampeni hata kutafuta wadhamini Homeboy Nyalandu ndie kahangaika kumlipia wakala wake!!!

Lisu is so poor ameshindwa Hadi kumgharimia wakala wake ikabidi Nyalandu aokoe jahazi la homeboy wake asionekane kamhujumu wakala wake kila akisema naomba nauli ya kungusha fomu Lisu anasema Hana . Wakala wake alitaka kuzira ndipo Nyalandu akaingilia Kati kumuokoa homeboy walau apate wadhamini
 
Chadema na upinzan hata wasiumize kichwa hoja kuu 2 zinatosha.

1. Ajira, Serkal haijaajiri watu kwa muda wa miaka 5 tena kuna taaluma ndo haijawah kabisa. Hata hizo chache walizoajir basi uje ajira hazifiki 10.

2.suala la uchumi mbovu kodi, biashara mbovu maisha nagumu.
 
MKUU MBAYA ZAIDI KILA MWAKA KUNA ONGEZEKO LA 6% YA DENI LA AWALI. NI UNYAMA MKUBWA HUU WANAOFANYIWA WAAJIRIWA. HALAFU ETI NIMPE KURA YANGU MNYONYAJI KAMA HUYO.
 
Uongo
 
Inashangashagaza sana. Waliomaliza vyuo wotw tunaujua ukweli huu na namna makato yanavyotia umaskini vijana. Haiuna maama yoyote kwa serikalo kukata makato 15% kwani hata ukikata pesa hizo wengine hawatayamaliza zaidi ya kuwatia umaskini tu.
 
Chadema na upinzan hata wasiumize kichwa hoja kuu 2 zinatosha.

1. Ajira, Serkal haijaajiri watu kwa muda wa miaka 5 tena kuna taaluma ndo haijawah kabisa. Hata hizo chache walizoajir basi uje ajira hazifiki 10.

2.suala la uchumi mbovu kodi, biashara mbovu maisha nagumu.
Sahihi kabisa. Jpm amefeli kila mahali.
 
labda wanafunzi wa nje ya nchi, kwa research yangu ndogo baadhi ya vyuo mpaka sasa sjaona kelele zozote za lissu hata uyu membe ni nyie tu ndo mnamkuza uku mtandaoni
UDOM, uchaguzi tu wa Bavicha mlipeleka hadi mapolisi. Unataka wakuimbie wazi wazi ??

Subiri utaona.
 
Kwa tume hii ya uchaguzi! Tayari wameanza kuweka mikwara kwa baadhi ya wangalizi wa ndani. Wangalizi mahili wa nje hawataalikwa au wataogopa Korona.
Covid-19. Kwanini wasiwaalike? After all hao waangalizi hawajawahi kuzuia wizi wa kura.
 
labda kura utampa wewe na rafiki zako lakini wasomi na wenye akili tutampa kura zote JPM haiingii akilini kumpa nchi msaliti wa nchi
Msaliti ni lugha na propaganda za Lumumba sio za wananchi. Nazo zimeshafeli kitambo sio nyimbo tena.
 
Hakika mambo yanazidi kunoga. Wakati uko upande wa Lissu. Namba pia ziko upande wake. Lissu amejipambanua kuwa mkombozi wa Wanavyuo vikuu, waliomaliza vyuo vikuu na wafanya kazi kwani anania ya dhati ya kuwakomboa makundi haya muhimu ktk taifa letu.

Akitangaza nia ya kugombea Kiti cha urais mwanzoni mwa July 2020 kupitia bendera ya upinzani ameeleza kuwa anatambua maumivu, mateso, umasikini na kero zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano. Taarifa zinaonesha kitakwimu kuanzia 2000 hadi 2018 zaidi ya wanafunzi 16.7M wamemaliza vyuo. Hawa ni kundi la wanamabadiliko. Wanaounga mkono sera za maendeleo wanaopenda uhuru na siasa safi.

1. Serikali imeamua kuwanyonga na kuwakamu mpaka damu graduates ( waliomaliza vyuo vikuu) kwa kutunga sheria mbovu za makato ya mikopo asilimia 15 kinyume cha sheria iliyokuwepo kwenye mkataba cha asilimia 8 tu. Hali hii iliyotetewa na wabunge wa CCM huku bunge likiwa gizani imeleta umaskini badala ya kuboresha maisha ya wahitimu hawa mara wanapoajiriwa au kujiajiri badala ya kuleta nafuu.

Imefika mahali mwajiriwa anaona bora asipate ajira afanye udalali au hata umachinga tu.

Mfano ni kijana mmoja nimekutana naye kwenye ofsi za bodi ya mikopo aliyesomea nchini China. Baada ya kupata ajira mshahara wake yaani gross salary ni 1.2M baada ya makato ya kodi za kikoloni na 15% ya Bodi ya mikopo anabakiwa tu na laki sita. Hali ni tete

2. swala la ajira limekuwa mtihani mkubwa na sintofahamu. Waliomaliza wanasugua visigino huku hakuna taasisi inayotoa mikopo nafuu ili wajiajiri kirahisi .walioko vyuoni hawaoni future yao maana wanaona kaka zao na dada zao wanavyohaha mtaani

Kundi hili kubwa litapata nafuu tu litakapomchagua kiongozi sio tu mwenye uchungu na maisha ya watanzania bali pia yeye mwenyewe ni mhanga wa uchumi mbovu uliosababishwa na serikali ya Rais Magufuli.

Hima hima wanavyo, wafanya kazi twende na Lissu Mzalendo wa Kweli.

Upinzani tunajua hakuna kama Lissu kwa muda huu. Tupeni haki yetu kwa kutuletea Mgombea mwenye sifa, uwezo na weledi wa kutuongoza. Kama Mgombea siyo Lissu hatutaki kusikia akina Membe? Nyalandu wala Lipumba. Ni bora tubaki na huyu huyu mvurugaji tutamzoea hivyo hivyo.

Asalam aleykum.
Lazima chadema wagawane kura na act
 
Back
Top Bottom