Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha, JF siku hizi imejaza mapunga kama wewe, waropokaji without ushahidi, FK you, hahahahahaNitakuwa najibizana na taahira aliyeathiriwa na ushoga. Ni wapi nimemtaja lisu kwenye maandishi yangu?
Au ndiye basha wako!
Anafikiri wote manyumbu. 😆😆😆Jamaa ana mikwara sana
Eti nitakanyaga Udongo...tehe tehe.
lema na wenje hawataki kuja?Lissu ni Shujaa
Wewe jamaa ni mkabila, na nakuapia ukabila hukaa mioyoni mwa majitu majinga majinga narudia majinga na sio mapumbavu. Mungu ibariki Tanzania!!Chadema ni chama wachaga wanamtumia tu Lissu kutafuta madaraka.
Uzuri watanzania wote wamestuka kasoro wanyaki na watu wa tarime ndio wanashobokea sana hao wachaga.
Jinga sana hili jamaa.Anafikiri wote manyumbu. 😆😆😆
Lissu kurudi ni jambo jema lakini sio kubwa Sana maana Tz ni kwao, ni nchi aliyopewa na Mungu wake...
God is greatIs it the start of the new era at chadema?.View attachment 2486385
Afya ya mama Janeth yenyewe ni ya mtu aliyetua mzigo! Yale mangumi mpaka mama wa watu analazwa JakYA hatosahauHumanity for Political gain! No way.
Mbona hawaonyeshi utu na matusi ya kaburini kila kukicha na hawakemei?
Kaburi la Hayati Raisi lisitumike kwa namna yeyoye ile na Wanasiasa wabezaji na wanafiki n.k
Hakuna hata mmoja amabye ametoka hadharani kukemea mambo yanaosemwa/ yanayosingiziwa kuhusu Hayati Raisi mengi ni ya Uwongo na yametengenezwa mahususi kudumaza nguvu zilizojengeka za kukataa ukoloni mamboleo.
Kutumiwa kama mpira wa kona, ilimradi tuu hapana.
Tundu Lissu akahutubie anao wahutubia. Mama Janeth asikubali hata CCM(anawajua ni wepi)na Viongozi wake kwenda huko na kujikomba mbele yake, ni wanafiki, wakitoka huko, na kugeuza mgongo wanaanza kumbeza mmewe, wanarusha vijembe hasi juu ya Hayati Raisi. Wakijuwa fika ni ya uwongo.
Amani ikulinde
Karibu nyumbani mtanzania mwenzetu, Mwenyezi Mungu akatangulize watanzania wake wakulinde na yeyote atakayejaribu tena kukudhuru akapigwe pigo takatifuMakamu Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Tundu Lissu ametangaza kurejea rasmi nchini January 25, 2023 saa 7 mchana baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.
View attachment 2479728
"Hatuwezi kuendelea kuishi uhamishoni bila ukomo. Hivyo basi, ninapenda kuwafahamisha kwamba, panapo majaliwa, nitakanyaga udongo wa ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano ya tarehe 25 Januari, 2023, majira ya saa saba na dakika 35 mchana." amesema
Ameongeza, “Kwa muda huo, ninatarajia kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia nikitokea Brussels, Ubelgiji, kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Nitafurahi sana kwa mapokezi yoyote siku hiyo."
Kuhusu suala la Katiba Mpya, Mhe. Lissu amesema “Kwa vyovyote itakavyokuwa, mwaka huu utakuwa mwaka muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Ni mwaka ambao, kama tukiamua kwa dhati ya mioyo yetu, tutapata Katiba Mpya na ya kidemokrasia, yenye mfumo huru wa uchaguzi, inayojali na kulinda haki za wananchi na inayoweka misingi imara ya uwajibikaji wa viongozi wetu kwa wananchi na wawakilishi wao.”
Anarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu wa 2023, anaamini kwamba, kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu kwa nchi yetu, tutaandika kitabu kizuri.
Mwanasiasa huyo machachari, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki ambae pia ni mwanasheria Nguli nchini alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi za moto na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 wakati vikao vya Bunge vikiendelea Jijini Dodoma.
Pamoja na kutangaza kurejea kwake, bado ameonesha wasiwasi juu ya mambo mbalimbali yasiyo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati huo. Hata hivyo, anaamini kuwa Mungu anaiwazia mema nchi hii.
"Ninafahamu kwamba, licha ya ahadi ya Mheshimiwa Rais na licha ya utayari wangu na wetu, siku zijazo hazitakuwa rahisi. Ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi."
“Mwenyezi Mungu anatuwazia sisi Watanzania “mawazo ya kutustawisha na wala sio ya kutuumiza, mawazo ya kutupa tumaini kwa siku zetu zijazo. Tukiweka nia ya dhati na kuitekeleza kwa dhati, tutayashinda majaribio na magumu yaliyo mbele ya safari yetu."
Chanzo: Twitter Spaces (Tundu Lissu)
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Tundu Lissu ametangaza kurejea rasmi nchini January 25, 2023 saa 7 mchana baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.