Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Tundu Lissu: Mkataba wa bandari ni suala nyeti sana

Hapana.
Weka ushabiki pembeni.
Lissu anajulikana kuwa mpambanaji toka Bulyankhulu; hadi Nyamongo. Kachaniawa magwanda na polisi kabla hata Acacia hajazaliwa.
Huu ushabiki ndio wanaoutumia akina Samia sasa kutuuza kama punda. Unasahau kabisa adui wa nchi hii ni nani badala yake unatumia ushabki tu, uliouzoea na kuufanya kama utani wa Simba na Yanga.
Hata Ibilisi alikuwa Kiongozi mkuu mbinguni akabadilika! Kwa hiyo LISU akibadilika tusimseme?
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Antipas Lissu amesema mkataba wa kuwakabidhi bandari baina ya Tanzania na Dubai ni swala nyeti (very seriously) ndiyo maana limepelekwa bungeni.

Akiongea club house amesema kitendo cha mkataba huo kupelekwa bungeni kinaashiria unyeti wake na athari ya mkataba husika katika sheria za nchi. Mikataba ya kimataifa yenye athari ya kubadilisha sheria lazima ipite bungeni.

Kwa mujibu wa sheria Za kimataifa kwa mfumo wa Tanzania mikataba ya kimataifa (international treaties) haiwi na nguvu dhidi ya Tanzania mpaka ipitie bungeni na kutungiwa sheria ya bunge. Hatua hii ndiyo inayoitwa domestication /ratification, yaani bunge linapitia Masharti ya mkataba wa kimataifa na kuyapitisha upya kama sheria ya bunge na baada ya hapo mkataba husika unakuwa na nguvu nchini maana unakuwa ni sheria.

Kwa kawaida mikataba ya kibiashara (bilateral commercial agreements) huwa haipiti bungeni, ukiona umepita bungeni basi mkataba husika una athari kubwa Sana kwa sheria za nchi hivyo unahitaji kupita bungeni ili kubadilisha baadhi ya sheria za nchi kuendana na mkataba husika. Hivyo kwa mujibu wa Tundu Lissu mkataba huo ukiridhiwa na bunge unakuwa sheria na unakwenda kubadilisha sheria zetu.

Tundu Lissu ameeleza kuwa mkataba huo unaenda kukinzana na Sheria zetu za maliasili zilizopitishwa na Magufuli zinazolazimisha migogoro yote ya rasimali zetu baina ya serikali na wawekezaji iamriwe nchini na kwa sheria zetu, lakini mkataba wa bandari unataka migogoro yote iamriwe Johannesburg Afrika kusini kwa kutumia sheria za Uingereza

Kuhusu vipengele vya ukomo Tundu Lissu amesema mkataba huu hauna ukomo kwani unasema utakoma pale ambapo shughuli husika zilizomo kwenye mkataba zitakoma, shughuli za kuendeleza na kusimamia bandari hazina ukomo.

Dadavua faida na hasara
 
Vipi wale wabunge wenu wa CCM 300+ si ndio wamepitisha mktaba wa Bandari? Mbona huwalaumu? Una waza kwa kutumia kisamvu chako?
"Wabunge wangu"

Hivyo na wewe una wabunge wako.? Wewe subiri mada mserereko unazolingana nazo kiakili ili utukane vizuri, wewe bumunda huku hapakutoshi.
 
Huu mkataba una kila dalili ya umangungo ndani yake. Kwa nini migogoro ikaamuliwe, na kwa sheria za Uingereza!!

Yaani ni kwa sababu tunawahitaji sana hao Waarabu, au ni kwa sababu tayari rushwa imeshatembezwa kwa waganga njaa, na wachumia tumbo wetu?
Wanaitaka bandari ya dar ili waiue, kwasababu waanajua ikiboreshwa , Uchumi wa Dubai utakufa kwa sababu Dubai inategemea bandari. So wakiinunua watajua na udhibiti mkubwa.

Kumbuka Dubai na washirika wake USA walihakikisha bagamoyo haijengwi kwa sababu bidhaa zote za china zinapitia Dubai kuja Afrika, hivyo km bagamoyo ingejengwa bidhaa zote za Afrika zingetoka china na kuja bagamoyo Moja kwa Moja, na hivyo uchumi wa Dubai ungekufa.

Hii Ni Vita ya kiuchumi so uwekezaji.
 
Hata Ibilisi alikuwa Kiongozi mkuu mbinguni akabadilika! Kwa hiyo LISU akibadilika tusimseme?
Mbona hueleweki unasema kitu gani?

Ni sehemu gani umenisoma nikisema Lissu asisemwe?

Amebadilika vipi, kwa kutoa tafsiri tu ya taratibu za kisheria zinazofanyika? Mbona hajatoa maoni yake kuhusu swala hilo, wewe umejuaje kuwa "kabadilika" wakati hajatoa maoni yake juu ya swala lenyewe
 
Kwa hiyo ile miezi 12 (muda wa mkataba) iliyotajwa kwenye ufafanuzi wa TPA ni kiini macho?

Mbadili sheria kwa ajili ya mkataba wa miezi kumi na mbili?

Naona Zitto yeye anacharaza mapambio tu kwamba kwa mara ya kwanza mikataba inapitia bungeni.

Je International treaty (siyo Bilateral Commercial Agreement) iliyosainiwa hivi karibuni zaidi ni ipi?
 
Wezenu wanatafuta pesa za uchaguzi nyie mko ulaya sijui manafanya Nini huko na hamsemi

Ccm na serikali walivyosema hawako tayari kuomba msaada kimataifa kwajili ya uchaguzi walimanisha mno ....

Rudini mje makamatie inavyotakiwa
 
Hapana mkuu bandari haiendi popote.

Hachukui mtu.

Ni Matamanio ya Kila Mtu mtz kuwa Engine ya Inchi yetu(Bandari) ibaki mkononi mwa serikali hata kama tunasua sua potelea mbali , kuliko kuwaachia Mataifa mengine yenye interest tofauti na Inchi yetu.

Usalama wa Inchi yetu upo rehani
 
Ni Matamanio ya Kila Mtu mtz kuwa Engine ya Inchi yetu(Bandari) ibaki mkononi mwa serikali hata kama tunasua sua potelea mbali , kuliko kuwaachia Mataifa mengine yenye interest tofauti na Inchi yetu.

Usalama wa Inchi yetu upo rehani
itarejea tu.

Mungu ni mwema wakati wote.
 

WhatsApp-Image-2022-03-02-at-9.19.23-AM.jpeg
Unajua wengine tulijua tu hii mbungi inayochezwa hapa HATUTOBOI! Lazima kuna ajenda!

Akina Msigwa na Kijaji wakajitokeza na blah blah kibao! Kiko wapi?

Cha bure duniani kwa sasa ni salamu tu,nayo ukijichetua unailipia.
 
Wanaitaka bandari ya dar ili waiue, kwasababu waanajua ikiboreshwa , Uchumi wa Dubai utakufa kwa sababu Dubai inategemea bandari. So wakiinunua watajua na udhibiti mkubwa.

Kumbuka Dubai na washirika wake USA walihakikisha bagamoyo haijengwi kwa sababu bidhaa zote za china zinapitia Dubai kuja Afrika, hivyo km bagamoyo ingejengwa bidhaa zote za Afrika zingetoka china na kuja bagamoyo Moja kwa Moja, na hivyo uchumi wa Dubai ungekufa.

Hii Ni Vita ya kiuchumi so uwekezaji.

Aliepinga ujenzi wa bandari ya bagamoyo ni Magufuli kwa kigezo cha kwamba mkataba wake una masharti magumu.

Unataka kusema na yeye pia alitumika na mabeberu?!
 
Back
Top Bottom