Tundu Lissu na wenzake waachiwa kwa dhamana

Tundu Lissu na wenzake waachiwa kwa dhamana

Nilijua tu lazima wamuachie, polisi na anayewatuma wote hawajielewi, ni wajinga tu.

Huwezi kumkamata Lissu kwa kuvunja sheria, wakati kimsingi ni wao ndio wamevunja sheria kumzuia Lissu kumfanya mkutano wake.

Naamini na ule ujumbe wa Mbowe utakuwa umewafikia haraka sana.
 
Screenshot_2023-09-10-21-24-44-1.png
 
hivyo walivyomkamata ndio wamempaisha zaidi kisiasa na ndivyo anavyozidi kueleweka zaidi na mabeberu pamoja na wananchi wasioipenda DP WORLD.
 
Tunashukuru kuwa huru! Kazi za siasa haswa ikiwa upinzani ni ngumu sana , kukamatwana kuachiliwa ni sehemu ya kadhia za siasa.
 
tundu.jpg

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limempatia dhamama Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na viongozi wengine wa chama hicho waliokamatwa muda huu saa 2 usiku jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amesema viongozi hao wametakiwa kesho saa tatu asubuhi kuripoti polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo iliyotolewa leo Jumapili Septemba 10, 2023 ilisema kuwa Lissu na wenzake watatu walishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia polisi kufanya kazi zao.

Mwandishi wa Habari kutoka Jambo TV, Oscar Kasubi aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo naye ameachiwa usiku huu.

===[/B]

Pia soma:

Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu

Jeshi la Polisi: Tunamshikilia Tundu Lissu kwa kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia Polisi kufanya kazi yake
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limempatia dhamama Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na viongozi wengine wa chama hicho waliokamatwa muda huu saa 2 usiku jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amesema viongozi hao wametakiwa kesho saa tatu asubuhi kuripoti polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo iliyotolewa leo Jumapili Septemba 10, 2023 ilisema kuwa Lissu na wenzake watatu walishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia polisi kufanya kazi zao.
Kweli unabii wa Ian Ndlovu kuhusu kukamatwa kwa prominent leader atakayetoka nje ya nchi imetimia. Alitabiri mwaka jana wakati hali ikiwa shwari kabisa ya maridhiano.
 
Back
Top Bottom