Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Narudi kama Mwananchi huru tarehe 27 Julai 2020, Serikali inipe Ulinzi. Kesi zangu 6 zina dhamana, sitakamatwa

Hivi hujisikii aibu kusema anazungumza na watanzania? Kama Nani kwamfano, sema atazungumza na wanachama wa Sacco's ya mtaa wa ufipa
Mkuu kwa ili mtu anayepaswa kuzungumza na watanzania anapaswa kwanza kuwa nani?na je hao watu uliowataja ni watu wa taifa gani?
 
M/Mkiti wa CHADEMA Taifa(B), Mhe. Tundu Lissu, Julai 21, 2020 saa 7.00 mchana atazungumza na Watanzania, atakapohutubia taifa kuhusu safari ya kurejea nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi takriban miaka 3 kwa matibabu, tangu aliponusurika jaribio la mauaji, Sep' 7, 2017, Dodoma-Tumaini Makene on twitter.

SHUKRANI
Michango, maombi na sala zenu ndiyo zilizosababisa leo nazungumza habari za kurudi nyumbani.

Nimekaa Ubelgiji kwa miaka miwili na nusu. Niwashukuru majirani na wananchi wenzangu wa mji wa kwa kunihifadhi kwa miaka hii miwili kwa mapenzi na upendo mkubwa, kwa kuniwezesha kujiona sehemu ya maisha yao kwa kipindi hiki cha miaka miwili na nusu.

Nikisema nashukuru ni kwa niaba ya familia yangu, mke wangu watoto wangu na ndugu zangu popote walipo.

USALAMA WANGU
Waliokuja kuniua hiyo siku na waliowatuma au waliowaelekeza bado wanaitwa watu wasiojulikana. Maana yake ni kwamba hao watu bado wapo, na kwasababu bado wapo na hawajasema kama lengo lao la kuniua wameliacha, bado natafakari juu ya maisha yangu. Kwahiyo narudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu bado haijaondoka, lakini narudi tu, ni nyumbani kwetu – inabidi nirudi.

Katika hii miezi 6 iliyopita, Uongozi wangu wa Chama, Mwenyekiti wangu wa Taifa Mh. Mbowe ameandika barua kwa vyombo vya ulinzi na usalama wan nchi yetu ili kuomba nipatiwe ulinzi nitakaporudi nyumbani. Hadi sasa tunasubiri majibu ya wakuu wa vyombo vyetu vya usalama ambao ndiyo wana jukumu la kuhakiksha nipo salama nitakaporudi nyumbani.

Alisema hana imani na vyombo vyetu vya usalama. Iweje awaombe ?
 
Tangu aondoke sasa ni miaka ni miaka mitatu, Tanzania haijawahi kusimama Wala kuwa na upungufu wowote wa rasilimali watu,

Na zaidi Sana Tanzania bila yeyote, bila Lisu, bila CCM Wala Chadema haitasimama

Lisu, Lisu, Lisu, Lisu, ndo Nani?
 
Sio lisu tu,hata wewe.Dunia haijawai kusimama hata kabla ya Adamu
 
Hiyo safari anatokea mbinguni.....maana story nyingi mwisho wa siku atasema anaahirisha kwa sababu cdf hajamuhakikishia usalama wake.

Lisu ni mtata mtata sana.
Usalama wa Lissu kikatiba unahakikishwa na serikali, sio chama chake! Naamini serikali itahakikisha anakuwa salama
 
Lissu namkubali sana ila inasikitisha chadema imeshajifia kwa tamaa binafsi za Mbowe
 
Akitua tu Segerea, hilo ajiandae tu anasubiriwa kwa hamu .Kutia nia ya uraisi hakuondoi hatia aliyonayo.Hilo ajiandae na akae analijua kuwa milango ya Segerea iko wazi inamsubiria na Court order ziko mikononi 24/7 za kumdaka awaishwe Segerea

Hilo ni yeye tu kujipanga kisaikolojia kuwa from Belgium to Segerea prison na uzuri hajasumbua interpol wala nini anakuja mwenyewe kwa nauli yake
 
Tunamsubiria kiongozi wetu kipenzi cha watanzania wote
M/Mkiti wa CHADEMA Taifa(B), Mhe. Tundu Lissu, Julai 21, 2020 saa 7.00 mchana atazungumza na Watanzania, atakapohutubia taifa kuhusu safari ya kurejea nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi takriban miaka 3 kwa matibabu, tangu aliponusurika jaribio la mauaji, Sep' 7, 2017, Dodoma-Tumaini Makene on twitter.

SHUKRANI
Michango, maombi na sala zenu ndiyo zilizosababisa leo nazungumza habari za kurudi nyumbani.

Nimekaa Ubelgiji kwa miaka miwili na nusu. Niwashukuru majirani na wananchi wenzangu wa mji wa kwa kunihifadhi kwa miaka hii miwili kwa mapenzi na upendo mkubwa, kwa kuniwezesha kujiona sehemu ya maisha yao kwa kipindi hiki cha miaka miwili na nusu.

Nikisema nashukuru ni kwa niaba ya familia yangu, mke wangu watoto wangu na ndugu zangu popote walipo.

USALAMA WANGU
Waliokuja kuniua hiyo siku na waliowatuma au waliowaelekeza bado wanaitwa watu wasiojulikana. Maana yake ni kwamba hao watu bado wapo, na kwasababu bado wapo na hawajasema kama lengo lao la kuniua wameliacha, bado natafakari juu ya maisha yangu. Kwahiyo narudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu bado haijaondoka, lakini narudi tu, ni nyumbani kwetu – inabidi nirudi.

Katika hii miezi 6 iliyopita, Uongozi wangu wa Chama, Mwenyekiti wangu wa Taifa Mh. Mbowe ameandika barua kwa vyombo vya ulinzi na usalama wan nchi yetu ili kuomba nipatiwe ulinzi nitakaporudi nyumbani. Hadi sasa tunasubiri majibu ya wakuu wa vyombo vyetu vya usalama ambao ndiyo wana jukumu la kuhakiksha nipo salama nitakaporudi nyumbani.
 
Kazi itakuwa kule kwa kina Agwe maana watu watateseka sana
Bila shaka atakuwa anaweka wazi ratiba kamili ya ujio wake kuanzia muda wa kuwasili na ndege atayosafiri nayo, bila kusahau alivyojipanga kiusalama ingawa hawezi kuweka wazi kila kitu.

Nafikiri Lumumba kesho kutakuwa hamna kazi, na hata Magogozi zitasimama kwa muda.
 
Naona upo lindo leo
FB_IMG_1592833724511.jpeg
 
Ndiyo maana mlitaka kumuondolea haki yake ya kuishi?

Back
Top Bottom