Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Narudi kama Mwananchi huru tarehe 27 Julai 2020, Serikali inipe Ulinzi. Kesi zangu 6 zina dhamana, sitakamatwa

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Narudi kama Mwananchi huru tarehe 27 Julai 2020, Serikali inipe Ulinzi. Kesi zangu 6 zina dhamana, sitakamatwa

Lumumba matumbo moto hamtalala mnaendelea kupanga njama zenu; ila mjue hakuna kisichokuwa na mwisho. Ukiua kwa upanga utauawa kwa upanga! Nyote mnaobeza yaliyompata Lissu mtalipa, na mara nyingine Mola akiamua, malipo ni hapa hapa duniani. Mwogopeni Mungu!
 
Hiyo safari anatokea mbinguni.....maana story nyingi mwisho wa siku atasema anaahirisha kwa sababu cdf hajamuhakikishia usalama wake.

Lisu ni mtata mtata sana.
baba chupa ongelea ya kigamboni mengine hayakuhusu
 
Akitua tu Segerea, hilo ajiandae tu anasubiriwa kwa hamu .Kutia nia ya uraisi hakuondoi hatia aliyonayo.Hilo ajiandae na akae analijua kuwa milango ya Segerea iko wazi inamsubiria na Court order ziko mikononi 24/7 za kumdaka awaishwe Segerea

Hilo ni yeye tu kujipanga kisaikolojia kuwa from Belgium to Segerea prison na uzuri hajasumbua interpol wala nini anakuja mwenyewe kwa nauli yake
Ana hatia gani mwenzetu, hebu tusaidie!
 
Ana hatia gani mwenzetu, hebu tusaidie!
Hapa sio mahakamani subiri atue nchini ndipo atajua vizuri akishadakwa.Maelezo yote mahakamani sio Jamii forums.Akidakwa akifikishwa Segerea siku kesi ikipangwa ndipo atajua makosa yake.Anakaribishwa Segerea
 
HATA UKIJA UNAKUJA KAMA MSAFIRI MWINGNE TU ..................HUNA JIPYA LAKUTUAMBIA..............USHAPOTEZA DIRA YA SIASA.......KAWAONGOZE NG'OMBE NA FAMILIA YAKO TU.
 
Hivi hujisikii aibu kusema anazungumza na watanzania? Kama Nani kwamfano, sema atazungumza na wanachama wa Sacco's ya mtaa wa ufipa

Huna haja ya makasiriko kama wewe hutaki kusikia panda pantoni kaungane na yule jasusi mwenzako ambaye jana wamemwonyesha kwamba yeey si lolote si chochote b.weg...e yule
 
Hapa sio mahakamani subiri atue nchini ndipo atajua vizuri akishadakwa.Maelezo yote mahakamani sio Jamii forums.Akidakwa akifikishwa Segerea siku kesi ikipangwa ndipo atajua makosa yake.Anakaribishwa Segerea
Watu wenye uwendawazimu, na roho za shetani naona bado mpo wengi. Mtu mwenye Roho wa Mungu huwezi kufurahia mateso au shida ya mtu mwingine. Ni ibilisi ambaye kazi yake kuu ni uharibifu, ndiye mwenye hulka hizo.

Lakini siyo jambo la ajabu, maana ni lazima tuishi pamoja na shetani mpaka mwisho wa dahari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amn
M/Mkiti wa CHADEMA Taifa(B), Mhe. Tundu Lissu, Julai 21, 2020 saa 7.00 mchana atazungumza na Watanzania, atakapohutubia taifa kuhusu safari ya kurejea nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi takriban miaka 3 kwa matibabu, tangu aliponusurika jaribio la mauaji, Sep' 7, 2017, Dodoma-Tumaini Makene on twitter.





SHUKRANI
Michango, maombi na sala zenu ndiyo zilizosababisa leo nazungumza habari za kurudi nyumbani.

Nimekaa Ubelgiji kwa miaka miwili na nusu. Niwashukuru majirani na wananchi wenzangu kwa kunihifadhi kwa miaka hii miwili kwa mapenzi na upendo mkubwa, kwa kuniwezesha kujiona sehemu ya maisha yao kwa kipindi hiki cha miaka miwili na nusu.

Nikisema nashukuru ni kwa niaba ya familia yangu, mke wangu watoto wangu na ndugu zangu popote walipo.

USALAMA WANGU
Waliokuja kuniua hiyo siku na waliowatuma au waliowaelekeza bado wanaitwa watu wasiojulikana. Maana yake ni kwamba hao watu bado wapo, na kwasababu bado wapo na hawajasema kama lengo lao la kuniua wameliacha, bado natafakari juu ya maisha yangu. Kwahiyo narudi nchini kwangu katika mazingira ambayo hatari dhidi yangu bado haijaondoka, lakini narudi tu, ni nyumbani kwetu – inabidi nirudi.

Katika hii miezi 6 iliyopita, Uongozi wangu wa Chama, Mwenyekiti wangu wa Taifa Mh. Mbowe ameandika barua kwa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi yetu ili kuomba nipatiwe ulinzi nitakaporudi nyumbani. Hadi sasa tunasubiri majibu ya wakuu wa vyombo vyetu vya usalama ambao ndiyo wana jukumu la kuhakiksha nipo salama nitakaporudi nyumbani. Hata kujibu tu barua hawajafanya hivyo

Naomba niseme hivi kwa ajili ya kumbukumbu, mimi sina na siwezi kuwa na jeshi binafsi la kunilinda. Sina na siwezi kuwa na rafiki au taasisi au nchi itakayotoa jeshi la kunilinda mimi nitakaporudi nyumbani.

Wajibu wa kunilinda mimi kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ni Jeshi la Polisi la Tanzania. Siyo jeshi la Polisi la Ubelgiji au la Kenya au la nchi nyingine – ni wajibu wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Ninarudi, nafahamu nikiwa mmojawapo wa wanaoomba kuteuliwa na chama change kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa sheria zetu za Uchaguzi, Jeshi la Polisi lina wajibu kisheria wa kuwapatia ulinzi wale ambao wamejitokeza kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Narudi nyumbani, natazamia, kuna kipindi nilisema knafuatwa fuatwa, polisi waingilie kati na wakapuuza na matokeo yake nikashambuliwa. Sasa narudi nyumbani, natarajia mara hii Jeshi la Polisi la Tanzania litatekeleza wajibu wake wa kunilinda na kulinda maisha yangu dhidi ya wale wanaowaita "watu wasiojulikana”

KESI MBALIMBALI (6) ZILIZOPO KISUTU
Nimeulizwa ulizwa sana na nimetishwa tishwa sana kwamba nikirudi nitakamatwa, nitakamatwa aidha kwa kesi ambazo zipo au pengine nitafunguliwa kesi nyingine. Naomba hili nalo jilizungumze for the record, kwenye kumbukumbu.

Nina kesi za jinai 6 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Na kesi zote hizi zinahusu kitu kimoja tu; maneno au kauli ambazo nimezitoa ambazo zinaikosoa au kuipinga au kutokukubaliana na sera, matendo au mipango ya Serikali ya Tanzania.

Kwa mijibu wa sheria za Tanzania kwa kadiri ninzavyozifahamu, yote niliyoyasema na kushitakiwa nayo, siyo makosa ya jinai.

Katika kesi hizo zote 6 zilizopo mahakamani, nilikuwa nje kwa dhamana ya mahakama na sijawahi kukimbia wala kuruka dhamana hiyo. Dunia inafahamu, Watanzania wanafahamu na Mahakama inafahamu sababu na mazingira yaliyofanya niondolewe nchini, na ambayo yamenifanya nibaki nje ya nchi hadi hapa ninapozungumza. Ndiyo maana katika kipindi chote hiki, katika kesi zote hizo 6, Mahakama haijafuta dhamana katika hata kesi moja.

Kwahiyo, narudi siyo kama mfungwa aliyekimbia dhamana; narudi siyo kama mhalifu aliyefutiwa dhamana; narudi kama raia huru – ambaye kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanzania anahesabiwa kuwa huru na kuwa hana hatia hadi hapo Mahakama itakapoamua vinginevyo.

Sasa, hivyo vitisho na kelele kuwa ukija utakamatwa, nitakamatwa kwasababu gani? Nitakamatwa kwa kosa lipi? Mahakama haijafuta dhamana kwa kesi hata moja kati ya hizo 6 nilizozisema.

Kama kuna agenda nyingine ya kunikamata ili kunizuia nisishiriki katika mchakato wa uchaguzi, sasa hilo ni linguine na tutalizungumza endapo litajitokeza.

Kwahiyo niseme tu kwamba, narudi kama raia huru wa Tanzania asiyekuwa na kosa lolote au jinai yoyote.

KUSHIRIKI MCHAKATO WA UCHAGUZI
Narudi ili kushiriki katika mchakato wa kuipatia nchi yetu viongozi wapya kwa miaka mitani inayokuja kuanzia tarehe ya uchaguzi mkuu.

Nawaombeni wananchi, nawaombeni wananchi mujitokeze kwa wingi wenu, kwa mamilioni yenu kila mahali nchini ili mwaka huu tuweze kuamua hatma ya nchi yetu.

Uchaguzi huu utakuwa uchaguzi muhimu kuliko uchaguzi mwingine wowote katika historia ya nchi yetu tangu uhuru.

Uchaguzi huu utaamua kama Tanzania itaendelea kuwa nchi ya vyama vingi vya siasa; kuwa nchi inayoheshimu haki za binadamu; kuwa nchi inayoheshimu utu. Au, uchaguzi huu utaamu tuwe nchi itakayorudi katika zama za giza za utawala wa chama kimoja cha mfumo wa utawala usiojali haki za binadamu ambako neon la mkuu wa nchi ndiyo sheria ya nchi.

Nawaomba, nawaombeni kwa mamilioni yenu katika vyama vyenu, kila moja wenu ajitokeze na ajiandae kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi.

Baada ya haya, naomba niwashukuruni sana. Naomba tukutane siku ya Jumatatu ijayo mchana, nitakapokuwa narejea nyumbani kwetu kuja kukutana na nyie na kuja kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu mbele.

Nawashukuruni na Mungu awabariki.

Ahsanteni sana!
amina tunakutakia safari njema na Mungu akubariki.
 
Jamani mimi simuelewi huyu mtu kwani alishasema anarudi nyumbani na atasindikizwa na walinzi kutoka UN sasa leo anaomba ulinzi wa polisi wa bongo jee wale wa Un wameahirisha?
 
Hiyo safari anatokea mbinguni.....maana story nyingi mwisho wa siku atasema anaahirisha kwa sababu cdf hajamuhakikishia usalama wake.

Lisu ni mtata mtata sana.
hapa kwenye viunga vya Lumumba naona watu wana pace up and down simu masikioni hazibanduki....

sura zao zimejaa hofu tupu maana kuna kila dalili yaliyotokea Kigamboni jana yatatokea pia kwenye kinyang'anyiro cha urais October. imagine kurejea kwa Lissu - ndiyo kabisaa jambajamba tu hapa!!
 
Jamani mimi simuelewi huyu mtu kwani alishasema anarudi nyumbani na atasindikizwa na walinzi kutoka UN sasa leo anaomba ulinzi wa polisi wa bongo jee wale wa Un wameahirisha?
Kikwetu mgeni aija kwako ukaona anaaga aga mara mbili mbili kuwa naondoka unajua huyo hataki kuondoka kanogewa na kwako hataki kuondoka kwako

Lisu kutwa kwenye vyombo vya habari ohhh narudi narudi kumbe muongo

Lisu kutwa anatangaza kurudi angalia matapeli hawa wakidanganya Chadema wenzao kuwa Tundu Lisu anarudi tarehe 7 mwezi wa tisa mwaka jana 2019!!

Msikie mwenyewe Mbowe na Lisu wakidanganya Chadema wenzao!! Mbowe naona kachoka usanii wake Lisu hataki tena kuonekana kituko kwenye vyombo vya habari kamwachia mwenyewe ona hii ambayo ndio imefanya Mbowe asitoe tamko tena kuhusu kurudi Msanii LISU kamwachia mwenyewe

 
Back
Top Bottom