Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

1. Hapana siyo consistent, alitunga list ya shame na kumkabidhi Dr Slaa kisha kwa pamoja wakatuaminisha kuna watanzania ni mafisadi. Lakini baadaye wakawasafisha mafisadi hao bila maelezo na kuwapa nafasi za kuongoza harakati zao za kupora madaraka kwa hila.

2. Hapana anapigania ridicule reforms: Ni kupitia matamshi yake aliwaaminisha watanzania kuwa kulifanyika utafiti. Soma hapa alichokieleza wakati akihojiwa kuhusu uchaguzi 2015."....Hayo yalisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akihojiwa na Global TV Online leo ambapo alisema pamoja na Lowassa kuongoza wagombea wote katika utafiti huo, suala la ufisadi lililokuwa linadaiwa kumhusu, halikuwa kipaumbele cha mamilioni ya wapiga kura nchini...." Yaani anatuona watz hatuna fikra siyo? Source:Lissu: Utafiti Ulionyesha Lowassa Alibeba 18% ya Kura Zote

3. Nina wasi wasi na hili. Inasemekana kesi zilizo nyingi anazosimamia zinafanikiwa kwa masuala ya ki-ufundi ya kimahakama si kwa hoja za ki-haki (sina takwimu halisi).

4. Ndiyo, hasa pale anapokuwa jambo ambalo halina maslahi kwa jamii pana ya kitanzania (mfano kususiwa kwa TZ kisiasa, kidplomasia, na kiuchumi)

5.Bahati mbaya kuna kipindi muda ukifika anaitumia 'hovyo hovyo'.
-----
Scrutiny your choice, you may come up with different choice at the end.
 
Amja muelewa tu Magufuli hivi ndio raisi anatakiwa kuendesha nchi kila mtu afanye kazi yake, mapungufu yake tu binafsi yana overshadow uongozi wake especially visasi na mtazamo wake wa social issues una mapungufu sana. Lakini Magufuli ni raisi bora na anaionyesha nchi Ina kasoro zipi.

Tusipojirekebisha kama taifa jinsi mambo yanavyofanywa sijui tutaweza kwa nani Magufuli katoa hiyo autonomy watu waonyeshe ufundi wao yeye yupo kuwakinga kama wataingiliwa, sasa tena tupewe nini.
 


"Hako kabunge ka chadema" jee hi ni lugha yenye staha?
 
Ha ha ha ha.. Lissu ni mzuri sana, ana akili sana, ni mpambanaji sana, na anaijua sheria sana.. Kwa kifupi yuko vizuri sana..
Ila kwa uraisi kwa maoni yangu hapana..
Uraisi anaweza pewa yoyote Tanzania, alimradi umiliki mfumo,, hicho ndicho kitakachomnyima... Uthubutu anao na hoja anazijua pasi na shaka na anasimamia utawala wa sheria.. Mwenzie.....mmmh
 
Tundu Lissu ni sawa na Obama au clinton.Wanasheria waliobobea.akigombea urais mpaka saa 5 asubuhi tutakuwa tumemaliza kazi ya kuindoa ccm madarakani.Hata ukiangalia, Lissu ndo mpinzani pekee wa ukweli,ambae haogopi.Ni muda muafaka sasa.
 
MsemajiUkweli,

Tundu Lissu kama atagombea ubunge na akashinda nipo tayari to donate $1500 to Pascal's chosen charity or cause!!

Atakimbilia kwenye kugombea urais ili kuondokana na aibu ya kushindwa ubunge lakini mwenye chama kashaanza kula tizi kuonyesha yupo fiti 2020 sioni chance yoyote ya yeye kupeperusha bendera!
 
Hivi ni kwa nini jamaa anamuogopa Tundu Lissu sana?
 
Ila bila tume Huru ya uchaguzi, kwakweli itakuwa ni mtihani sana,, tusije tukamkosa Mtoto na maji ya moto,,,maana akiteuliwa kugombea urais, ,itabidi kule kwenye uBunge aachanenako nadhani ,na kwenye urais bila Tume huru na hawa wezi wa kura, mmmmh
 
Hata mimi niliwaza hiki kitu, kuna uwezekano akateuliwa kuwa mgomea urais!! Angalia viashiria...

1. Kila siku utasikia lissu lissu, kwenye media sasa hivi niLissu na sio mbowe wala lowassa!!

2. Huyu ni mtu amekua anaongea na kuwa front peji kushinda katibu mkuu wa chama!!

3. Ukienda kigali nairobi kila mahali wanamtaja Lissu!!

Haya yote sio bahati mbaya... Nadhani anaandaliwa, na hata kama asipogombania 2020 basi 2025 tutamuona akigombea urais!!

Najua watu watakuponda ila time will tell!!
 
Kwani serikali nzima itaendeshwa na Lissu? Vp RCs, DCs, mawaziri pamoja na nafasi zingine za kisiasa zinazopaswa kishikwa na wanachadema wenyewe are they elite enough to run the government?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…