Tundu Lissu ni mwanasiasa bora wa upinzani kwa sasa

Lisu yupo sehemu sahihi kwasababu nguvu waliyoitumia kukifikisha chama kilipo itamchukua miaka mingi iwapo atahama. Labda chair wa chama anatakiwa ku step down harakati ziendelee. Kwasiasa za DJ hawajitofautishi na CCM maana ni masifu na mapambio.
Acha kubeza Mwenyekiti wetu. Ndiye aliyewalea hao akina Lissu, akima Zitto na wengine woote unaoona ni bora.
 
Wana hitajika wanasiasa wengi wenye kaliba ya Lissu kupambana na huyo aliye madarakani kwa msaada wa nguvu za dola.
Nguvu ya Lissu ya ujasiri na hoja ilichangia sana afya ya yule bwana kuwa sio dhaifu. Ingawa kufariki tumeandikiwa na Mungu lakini Lissu alimtia stress sana
 
Hatupaswi kuzikatia tamaa mkuu, ndizo zinazo amua hatima ya maisha yetu yaweje. tunapaswa kuzi rekebisha mahali zinapo enda ndivyo sivyo.
Watu waliofanikiwa ktk jambo lolote hawakati tamaa no matter what.
 
Hatutaki siasa za visasi. Mbowe kwa sasa anapigania nchi ipate tume huru ya uchaguzi na katiba mpya kabla ya uchaguzi na haya ni makubaliano kwenye maridhiano. Huko mnakotaka tuanzishe ugomvi na serikali hatutakwenda huwezi kushindana na dola. Siasa hasa ya upinzani inahitaji busara na akili ya hali ya juu kutimiza malengo mbona kama mmeshasahu kwa muda mfupi tulipotoka?
 

Bora tusifanye siasa kuliko kufanya siasa za kuendeshwa kwa utashi wa CCM. Kwa taarifa yako siasa za kuongozwa na CCM ni bora wote mjiunge CCM.
 
Huyu si mwanasiasa bali ni mwana harakati. Alianza kama mwana harakati, anaendelea kama mwanaharakati na ataishia kama mwanaharakati.

Hana jipya, hasa katika zama hizi za siasa za kistaarabu. CHADEMA MSIFANYE KOSA 2025 KUMPITISHA MWANAHARAKATI KUGOMBEA URAIS AU UENYEKITI/chadema.
 
Busara na akili ipi ya kunyenyekea watawala wanao wamumiza watawaliwa pamoja na wao vyama vya upinzani ?
 
Huyu si mwanasiasa bali ni mwana harakati. Alianza kama mwana harakati, anaendelea kama mwanaharakati na ataishia kama mwanaharakati.
Mwana harakati ni mtu wa namna gani na mwanasiasa ni mtu wa namna gani ?
Hana jipya, hasa katika zama hizi za siasa za kistaarabu.
Siasa za kistaarabu zipi ? Za wizi wa kura ? , Za kupiga, kujeruhi, kuua na kupoteza watu kutoka kundi la watawaliwa ?, Kuminya na kukanyaga haki za kikatiba kwa kundi la watawaliwa ? Za kutumia vyombo vya dola? Za kuiba na kufilisi mali za watu kutoka kundi la watawaliwa walio kinyume na watawala ?
CHADEMA MSIFANYE KOSA 2025 KUMPITISHA MWANAHARAKATI KUGOMBEA URAIS AU UENYEKITI/chadema.
Mimi sio mwanachama wa Chadema.
 
Bora tusifanye siasa kuliko kufanya siasa za kuendeshwa kwa utashi wa CCM. Kwa taarifa yako siasa za kuongozwa na CCM ni bora wote mjiunge CCM.
Hakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…