Tundu Lissu ni mwanasiasa bora wa upinzani kwa sasa

Tundu Lissu ni mwanasiasa bora wa upinzani kwa sasa

Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za kitaifa na kimataifa kwa muda mrefu sasa.

Taifa letu la Tanzania limekuwa na siasa za uonevu mkubwa wa haki za msingi kutoka kwa watawala kwenda kwa watawaliwa.

Aina hii ya uonevu unao tendeka hapa nchini unao sababishwa kwa asilimia kubwa na watawala ambao ni CCM una hitaji aina ya siasa na wanasiasa watakao weza kukabiliana nao.

Tundu Lissu kutokana nami kumfahamu kwa muda mrefu kutokana na msimamo wake ni mtu sahihi kwa sasa kupambana na huu mfumo, kikwazo kikubwa kwa lissu kwa sasa ni chama alichopo na aina ya siasa ifanyazo kwa sasa haziendani na kaliba ya mwanasiasa kama Lissu.

USHAURI: Kwa sasa taifa lina hitaji aina ya wanasiasa kaliba ya Lissu waki ungana naye na kuweza kuanzisha chama kipya kitakacho endana na aina ya misimamo waliyo nayo ambayo ni sahihi kwa sasa katika kupambana na watawala [ CCM ] tofauti na misimamo ya kisiasa ya vyama vya upinzani vilivyopo nchini kwa sasa.

Tundu Antiphas Lissu hayupo mahali sahihi[ CHADEMA ]

: Haya ni maoni na ushauri wangu, vipi kuhusu wewe ndugu mwanachama mwenzangu wa jamiiforums katika jukwaa hili la siasa maoni na ushauri wako kwa lissu ni upi ? Karibu
Sikusoma content,ila tittle ya uzi tu imetosha kunifanya nikwambie huna akili

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Sawa, mimi kichwa changu kigumu wewe chako chepesi huo ndio utofauti uliopo kati yangu na wewe.

Kamwe vitu na mambo magumu kwa kichwa chako hayawezi kuwa upande wako hata siku moja, hivyo ni ngumu kwako kuya tafakari na kuya tatua katika njia iliyo bora.

Mfano: Mada/thread jadiliwa.
Over
 
Back
Top Bottom