Tundu Lissu ni mwanasiasa bora wa upinzani kwa sasa

Tundu Lissu ni mwanasiasa bora wa upinzani kwa sasa

Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za kitaifa na kimataifa kwa muda mrefu sasa.

Taifa letu la Tanzania limekuwa na siasa za uonevu mkubwa wa haki za msingi kutoka kwa watawala kwenda kwa watawaliwa.

Aina hii ya uonevu unao tendeka hapa nchini unao sababishwa kwa asilimia kubwa na watawala ambao ni CCM una hitaji aina ya siasa na wanasiasa watakao weza kukabiliana nao.

Tundu Lissu kutokana nami kumfahamu kwa muda mrefu kutokana na msimamo wake ni mtu sahihi kwa sasa kupambana na huu mfumo, kikwazo kikubwa kwa lissu kwa sasa ni chama alichopo na aina ya siasa ifanyazo kwa sasa haziendani na kaliba ya mwanasiasa kama Lissu.

USHAURI: Kwa sasa taifa lina hitaji aina ya wanasiasa kaliba ya Lissu waki ungana naye na kuweza kuanzisha chama kipya kitakacho endana na aina ya misimamo waliyo nayo ambayo ni sahihi kwa sasa katika kupambana na watawala [ CCM ] tofauti na misimamo ya kisiasa ya vyama vya upinzani vilivyopo nchini kwa sasa.

Tundu Antiphas Lissu hayupo mahali sahihi[ CHADEMA ]

: Haya ni maoni na ushauri wangu, vipi kuhusu wewe ndugu mwanachama mwenzangu wa jamiiforums katika jukwaa hili la siasa maoni na ushauri wako kwa lissu ni upi ? Karibu
Mh 🤔🤔 ngoja uvccm waje wakiongozwa na mbatizaji!!
 
Huyo Lissu wako ndio ana roho mbaya na chuki dhidi ya maendeleo ya Tanzania yule ni wakala wa Mabeberu
Tangu lini mwanasheria nguli na mwanasiasa mbobevu Tundu Antiphas Lissu kawa wakala wa mbuzi ?
 
Mwana harakati ni mtu wa namna gani na mwanasiasa ni mtu wa namna gani ?

Siasa za kistaarabu zipi ? Za wizi wa kura ? , Za kupiga, kujeruhi, kuua na kupoteza watu kutoka kundi la watawaliwa ?, Kuminya na kukanyaga haki za kikatiba kwa kundi la watawaliwa ? Za kutumia vyombo vya dola? Za kuiba na kufilisi mali za watu kutoka kundi la watawaliwa walio kinyume na watawala ?

Mimi sio mwanachama wa Chadema.
Uvccm wamepaniki sana tangu Rais atangaze uhuru wa siasa.
 
Ni kweli kabisa, Mbowe hastahili kabisa kuendelea tena kuwa mwenyekiti wa CDM, maana anaanza kugeuka kwa kasi kuwa kama akina Mrema, Shibuda, Cheyo nk. CDM wakiendelea kumuacha Mbowe kuwa mwenyekiti atakipasua chama. Mbowe ashauriwe kukaa pembeni, au atolewe kwa lazima kwenye uenyekiti.
Mbowe alishasema kuwa mwaka huu ndiyo wa mwisho kwake kuwa Mwenyekiti,na ataheshimika akisimamia ahadi yake hii. Ametoa mchango wa kutosha kwenye chama ni wakati sasa kijiti amkabidhi mwingine atakayekipeleka chama next level.
 
Anarudi kuwahi keki ya taifa kabla Mbowe hajaimaliza peke yake 😀😀
 
Ndio maana nasema wewe hujielewi uoni hapo nimemjibu nan
Kwa nini ulifanya hivyo toka awali, je ni nani hasa asie jielewa ? Je ni yule anaye tuhumuiwa na mwenzake kuto kujielewa ? Au ni yule anaye shiriki majibizano na yule asiye jielewa ?
 
Kichwa ngumu ni kipi unaweza kuelewa wewe? Hahahaha
Sawa, mimi kichwa changu kigumu wewe chako chepesi huo ndio utofauti uliopo kati yangu na wewe.

Kamwe vitu na mambo magumu kwa kichwa chako hayawezi kuwa upande wako hata siku moja, hivyo ni ngumu kwako kuya tafakari na kuya tatua katika njia iliyo bora.

Mfano: Mada/thread jadiliwa.
 
Back
Top Bottom