Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,480
- 7,443
Akihojiwa na kituo cha KTN news cha Kenya Tundu Lissu amesema huu ni wakati wa kuanza na ukurasa mpya kama taifa la Tanzania. Maana tayari tumepoteza Kiongozi.
Tundu Lissu amesema kuwa mapema tarehe 7 mwaka huu alihoji kuwa yupo wapi rais Magufuli baada ya kutoonekana kanisani na mitaani. Vyanzo vyake vya uhakika toka serikalini vilimuambia kuwa anaumwa Covid 19.
Pia Lissu amesema kuwa marehemu alikuwa mkaidi juu ya hili gonjwa juu ya kuvaa barakoa, kupata chanjo na kutumia njia za kisayansi kupambana nalo badala yale aliamini zaidi njia za kienyeji.
Lissu ametoa pole kwa familia ya marehemu na Watanzania wote, na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuanza ukurasa mpya. Maana kwa miaka mi tano watu wameuwawa, wameteswa, wamepoteza kazi na wengine wamebomolewa nyumba zao.