chief swetu
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 240
- 246
Pole yetu wananchi wenzangu ya kuondokewa na kiongozi wetu mkuu wa nchi hayati MH. JOHN JP MAGUFULI. Binafsi nmeguswa na kifo hiki ingawa sikua na nasaba nae kivyovyote zaidi ya utanzania wetu, Ndani ya kipindi kifupi Tumepoteza viongozi wengi sana na wenye nyadhifa tofauti tofauti bara/visiwani.
Katika hii iliokua serikali ya awamu ya 5 chini Hayati Magufuli na mengi yalisemwa lakini kwanini Magufuli? ikumbukwe msiba huu umeanza kwa tabiri tabiri nyingi kabla hata haujatokea na tunataarifa za baadhi ya waliotangaza msiba kabla ya wakati kushikiliwa na vyombo vya usalama machungu yao yataisha vipi ikiwa walisema iliokuwa kweli?
Wahanga wa kisiasa na waliopoteza wapendwa wao kwenye mazngra tatanishi itakuaje? Wananchi wa kawaida na uwakilishi wa kero zetu barabarani nani atatuckia? Tunamshukuru MUNGU Watanzania wenzangu tuungane kwa hili kulinda Amani, Upendo na Mshikamano wetu!
Kwa wale wanaofurahia msiba huu wakiamini Mungu kamuadhibu, niwakumbushe hatufi kama adhabu, hatufi kwa kuombewa dua mbaya na adui zetu, hatufi kwa maradhi, hatufi kwa umaskini au mamlaka! Tunakufa na tutakufa siku zetu za kuishi duniani alizotupangia mola wetu mlezi zitakapo kamilika!
Mungu ailaze roho ya Mh. Magufuli mahali panapo stahili amina