maybe this could be the end of despotic rule
Absolutely, YES..
There's a big lesson hehind this scenario for whoever is prepared to take the Magufuli's presidential seat...
And this lesson is: LOVE OTHERS EQUALLY OR MORE THAN YOU LOVE YOURSELF..
....kama wewe hupendi KUFA, usijaribu hata kuwaza tu kuua mtu mwingine!!
....kama wewe unapenda uheshimiwe, anza kwanza kuwaheshimu wengine!!
nk nk..
å Kiukweli mimi siogopi kuusema ukweli, kuwa, marehemu Magufuli alikuwa ni kiongozi mwenye kiburi, asiyejali, mwenye chuki, anayejipenda zaidi mwenyewe kuliko kuwapenda wengine, asiyependa kukosolewa akifikia hatua ya kujiweka level moja na Mungu muumba....
Hakuna tukio liliudhi na kukera watu wengi kama ushiriki wake direct or indirect kupanga na kutaka kumuua mkosoaji wake mkuu Mwanasheria Tundu Lissu mwaka 2017. Huo ulikua ujinga uliovuka mipaka ya ujinga wa kawaida. Huo ulikuwa mwanzo wa mandalizi ya KIFO CHAKE..
Alionywa, lakini hakusikia wala kuelewa. Madaraka yalimpa kiburi, akasahau kabisa kuwa madaraka hayo kapewa na Mungu na wakati wowote asipomsikiliza anaweza kuyachukua kwa namna apendavyo yeye. Akadhani hatakufa. Sasa Mungu kachukua madaraka ya kiti chake kwa kutumia KIFO CHA MWILI...
Haya yalikuwa ni mazingira aliyojitengenezea mwenyewe kufa vibaya na pengine kabla yq wakati..
å Honestly, kufa ni kufa tu. Na kila mtu hakika atakufa. Lakini tunakufaje hilo ni la muhimu sana. Na wakati mwingine watu wengi huwa tunajitengenezea mazingira ya kufa vibaya mwenyewe kwa kutotii sheria nzuri za Yehova, Mungu baba kwa manufaa yetu...
å Hopefully, awe alipata neema ya kutubu dhambi zake kabla umauti haujampata. Vinginevyo, atakutana na yule tajiri aliyemnyanyasa Lazaro kwa kula makombo ya chakula chini ya meza yake...
Hakutambua kuwa Lazaro pamoja na umasikini na unyonge wake, lakini kumbe alikuwa tajiri wa REHEMA na NEEMA tele ya Mungu...
Walipokufa wote tajiri na Lazaro, kila mmoja alienda na kuwekwa mahali anapostahili...
Lazaro akienda moja kwa moja katika pumziko la raha na furaha ya milele kifuani mwa Baba Ibrahimu...
Tajiri yule mwenye kiburi, jeuri, muuaji, mnyanyasaji, mzurumaji, mwizi na sifa zingine kama hizi, alitupwa ktk sehemu ya mateso pasipo na msaada wa mapesa na ufahari wake wa hapa duniani..
Mungu amweke aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli MAHALI ANAPOSTAHILI...
TUKUMBUKE HILI: Baada ya KIFO ni HUKUMU